SoC04 Elimu ni Ukombozi

SoC04 Elimu ni Ukombozi

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
May 21, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Taifa lolote lile Ili liweze kuendelea halina budi kuimarisha sekta ya Elimu Kwani ndiyo ukombozi wa binadamu na uchumi kwa ujumla.

Tunaposema kuimarisha sekta ya Elimu inatakiwa kupata na kuwaandaa walimu Bora vyuoni,mitaala inayoendana na wakati uliopo Karne ya 21.

Tukianza na mitaala jinsi ya kuandaa inatakiwa kushirikishwa walimu,jamii na wadau mbalimbali wa Elimu na kupata namna Bora ya Nini kifanyike katika masuala ya UFUNDISHAJI na ujifunzaji shuleni.mathalani Elimu ya msingi ilenge Mtoto kupata ujuzi na maarifa yatayomuwezesha kumudu MAISHA yake pindi atakapomaliza shulé mfano,awe na ujuzi katika kilimo,ufugaji,uwindaji n.k.

Vilevile walimu wanaoandaliwa vyuoni wawe ni wale wenye ufaulu mzuri kidato Cha nne na sita kama vile division one mpaka three na pia kwa walimu wa shule za msingi waandaliwe walimu kulingana na umahiri wa masomo wanayoyamudu mfano sayansi na arts Ili walimu Hawa baadae wataenda kuwatengeneza wanafunzi wazuri na kuondoa tatizo la Mtoto kutokujua hisabati na kiingereza ambayo yamekuwa ni tatizo kwa sasa.
Pia katika eneo la KKK ni vizuri nchi ikaweka utaratibu wa kuwaandaa walimu mahiri vyuoni watakaokuwa wamejikita katika ufundishaji wa watoto wa darasa la kwanza na la pili vilevile wale wa Elimu ya awali,Ili kuondoa tatizo la watoto kutokujua KKK.

Pia nashauri motisha kwa walimu wanaofundisha masomo ya awali na darasa la kwanza Ili iwape morali na kujituma zaidi katika kuwafuatilia kwa ukaribu katika suala ujifunzaji na UFUNDISHAJI.

Maslahi,hatuna budi kuboresha maslahi ya walimu Ili kuweza kufanikisha na kuinua kiwango Cha ELIMU nchini, haiwezekani mwenye bachelor ya afya akampita kwa kiwango kikubwa Cha mshahara yule mwenye bachelor degree ya Elimu ilihali wote viwango vyao vya Elimu ni sawa tofauti ni sekta ambazo zote Zina umuhimu katika jamii.

Miundombinu ya Elimu kwa kiasi kikubwa serikali inajitahidi sana kuboresha mazingira ya miundombinu ya Elimu kama vile madarasa,vyoo,nyumba n.k ila baadhi ya maeneo ya pembezoni Bado Kuna changamoto hasa makazi ya watumishi wanaishi katika mazingira magumu na hakúna nyumba Bora za kupanga na pia serikali Ione namna Gani ya kutoka posho katika mazingira magumu pengine itatoa morali ya walimu kujituma na kupunguza Hali ya uhamaji VIJIJINI na kukimbilia mjini.

Ajira za walimu,serikali Ione tija ya kusajiri walimu kwa wingi kwani Kuna uhaba sana hasa vijijini shule kuwa na walimu 3,2,4, ni kawaida,hapomwalimu mmoja ana masomo mpaka 14,12,17 usitegemee watoto watapata vipindi vya kutosha kwa masomo yote.

Usimamizi wa mitihani ya taifa,nashauri Baraza la mitihani la taifa likawa na mfumo mzuri wa usimamizi Ili kudhibiti udanganyifu katika mitihani ya darasa la 7 la 4 kidato Cha pili,nne na sita mfano vyumba vyote vya mtihani vifungwe kamera maalumu zinazoweza kukaa na chaji saa 12 Ili iweze kutumika mpaka kijijini panapokuwa na changamoto ya umeme,kuwe na adhabu Kali Ili kuondoa kabisa suala la udanganyifu kwa wasimamizi na viongozi wa shule.

Serikali iongeze bajeti ya ruzuku shuleni Ili kurahisisha mahitaji ya vifaa vya UFUNDISHAJI na ujifunzaji na pia ziingizwe kwa wakati Kila mwezi.

walimu wafuatiliwe kuandaa zana za ufundishaji na ujifunzaji Kila somo na Kila kipindi Ili kumwezesha Mtoto kuwa na uelewa zaidi na kulupenda somo na hii itawezekana ikiwa mwalimu ana masomo 1 au 2 itasaidia kuwa na muda zaidi wa kuandaa zana,nukuu na mbinu Bora za ufundishaji.

Stahiki za likizo nazo zilipwe kwa wakati Ili ilete morali kazini,kuwe na warsha za mara kwa mara zitakazosaidia kubadilishana uzoefu na changamoto mbalimbali kazini.

Vilevile walimu wakuu wawe na somo Moja tu la kufundisha Ili awe na muda mwingi wà kufuatilia masuala ya taaluma shuleni na mambo ya kiofisi.

Katika masuala ya ujenzi ningeshauri serikali utengeneze namna ya watu wa kusimamia shughuli za ujenzi shuleni Kwan walimu wanapoteza vipindi vingi panapokuwa na mradi wa ujenzi shuleni na kwa vile hawana utaalamu nayo hivyo kupelekea kujengwa chini ya kiwango na kutoka milka vizuri.

Ruhusa za masomoni,ni vizuri serikali iweze kuwalipia gharama za masomo watumishi wake Ili iweze kuchochea walimu kwenda masomoni kujiendeleza na kuongeza kiwango Cha maarifa na hata wanaporudi masomoni iweze kuwapatia promotion kwa haraka Ili iwe ni kichocheo kwa wengine kwenda kujiendeleza na kuwa na walimu Bora zaidi.

Mitaala ya Elimu sekondari nayo iweze kumfanya mwanafunzi amalizapo aweze kuwa na ujuzi mbalimbali na kujitegemea pamoja na kujiajiri,wajifunze zaidi kwa vitendo kama vile kilimo, ufugaji, sanaa, teknolojia, mapishi, ushonaji n.k Ili kuweza kuondoa tatizo la uhaba wa ajira na kupata dhana ya Elimu ni ukombozi.

Asante
By karama mohamedi lusewa.
0747917979
 
Upvote 2
Vilevile walimu wanaoandaliwa vyuoni wawe ni wale wenye ufaulu mzuri kidato Cha nne na sita kama vile division one mpaka three na pia kwa walimu wa shule za msingi waandaliwe walimu kulingana na umahiri wa masomo wanayoyamudu mfano sayansi na arts
Hii imekaa poa sana, tunaitaka ile 'cream' wale watu majiniazi ndio wakafundishe wengine....... kitu kidogo tu cha kujiuliza ni je? Soko linawavutia, maslahi marupurupu?

ujifunzaji na UFUNDISHAJI
Nafurahi unavyoandika ujifunzaji na ufundishaji. Umeweka wazi kuwa ni jukumu la wote wawili.

Serikali iongeze bajeti ya ruzuku shuleni Ili kurahisisha mahitaji ya vifaa vya UFUNDISHAJI na ujifunzaji na pia ziingizwe kwa wakati Kila mwezi.
Yaaas, kaka. Mawazo murua
 
Back
Top Bottom