Elimu ni uti wa Mgongo

Elimu ni uti wa Mgongo

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
ELIMU NI UTI WA MGONGO


Wanaccm tunapojielimisha kwa hiari zetu Mambo mbalimbali ni wazi tunakuza UWEZO WETU KIFIKRA NA KIMITAZAMO.

Pia tunaitendea haki Katiba ya CCM 1977 toleo 2020 ambamo tuna AHADI NA WAJIBU kwa kila Mwanaccm kuuondoa UJINGA kila Mmoja wetu kwa kadri anavyojaaliwa na Mola wetu kufanya hivyo.

Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2020 ibara 15(3)(6) na uk 151 kifungu cha (3)(6)

Niliwahi kusoma kitabu Cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 152

Mwl JK Nyerere aliwahi kusema,

Ninamnukuu,

" Ahadi Moja ya Mwana TANU inasema, Nitajielimisha kwa kadri ya Uwezo wangu wote na kuitumia Elimu yangu kwa faida ya wote."

Mwisho wa kunukuu

Wanaccm wenzangu ,
Elimu haipatikani tu kwenye vineno vichache.

Tukiwauliza WATAALAMU WALIOSOMEA FANI MBALI MBALI utagundua walisoma vitu vingi ndiyo maana WASOMI WA UKWELI HUWA HAWAPENDI MAJIBIZANO YASIYO NA TIJA KWANI UELEWA WAO NI MPANA.

HATA HIVYO SISI KAMA CCM TUNAO WAJIBU WA KUVISOMA VITABU VYOTE VYA CCM ILI VITUSAIDIE KUACHA KUISHI KWA MAZOEA NA KUISHI KWA UHALISIA WA YALE TUYOKUBALIANA KUYAFUATA. NA MTAZAMO HUU UTASAIDIA KUONDOA MIGOGORO NA MIGONGANO MIONGONI MWETU AMBAYO HUPELEKEA BAADHI MIONGONI MWETU KUPINGA HATA MAMBO YENYE UKWELI NA FAIDA KWA JAMII KISA TU BAADHI YETU WSMEJIWEKA REHANI FIKRA NA MAWAZO YAO KWA AJIRI YA KUCHUMIA TUMBO.

Tusome Ilani ya CCM 2020 - 2025 uk 01 kifungu cha 04.

Tukisoma Kitabu cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 154

Mwl JK Nyerere anatukumbusha,

" Kila Mmoja aliyepata nafasi ya kujifunza kitu awe tayari na DHAMIRA ya kuwafunza wengine."

Mwisho wa kunukuu

Wanaccm wenzangu ,
Sote tunatambuwa Uongozi wa nchi yetu HAUNA DINI ila watu wake Wana Dini.

Ndiyo Maana kila tunapowaapisha VIONGOZI WETU HUMALIZIA VIAPO VYAO KWA KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU KILA MTU KWA IMANI YAKE KUONYESHA NGUVU , UTUKUFU NA UWEPO WA MUNGU.
NI WAZI IPO HAJA YA SISI SOTE WANACCM KUELIMISHANA KILA MTU KWA kile anachokijuwa KWA MAPANA YAKE PASIPO KUWEKEWA MIPAKA KWANI BINADAMU HAKIKA TUNATOFAUTIANA MAPOKEO YA MAMBO.
HIVYO HAKUNA ELIMU ISIYOFAA.

Niliwahi kusoma Kitabu cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 147

Mwl JK Nyerere aliwahi kusema

" Hakuna Elimu isiyofaa, Wala hakuna mafunzo yasiyokuwa na faida."

Mwisho wa kunukuu

Katika CCM tupo watu wengi WENYE UELEWA TOFAUTI.
Wapo wenye kiu ya kujuwa Mambo mengi ya KIELIMU na wapo waliolizika NA HALI WALIZO NAZO .

Tunapopewa TALANTA NA MWENYEZI MUNGU ya kuwaelimisha watu , mara nyingi tunaangalia UHITAJI WA KUNDI KUBWA NA SIO KUNDI DOGO LILILO POTEZA UELEKEO.
Binafsi nikifanya Jambo langu la kuwaelimisha watu huangalia uhitaji wa kundi kubwa NA SIO UHITAJI WA WAKATISHA TAMAA KWANI HAWA WANAHITAJI MAOMBI MAALUMU KWA MWENYEZI MUNGU ILI AWABADILISHE KIMITAZAMO NA KIUELEWA.

Naikumbuka Tarehe 29/May 2021
Dkt Hussein Mwinyi
Rais wa Zanzibar
Akiwa ziarani kaskazini Unguja ya kutoa Shukrani kwa Wanaccm ,
Alisema,

" Mimi nasema Kama alivyosema Mheshimiwa Mwakilishi hapa,
HAKUNA BINADAMU HAPA atakayependwa na watu wote,
HAKUNA BINADAMU atakaye ungwa mkono na watu wote."

" Lakini mara zote huwa najiuliza ,
Wanao litaka hili ni wengi au ni WACHACHE,
Jambo hili ninalo lifanya lina maslahi kwa nchi yetu au halina.
" Nikipata majibu hayo kwamba ninachokifanya
kina maslahi kwa nchi yetu na wengi wanaliunga mkono Basi naendelea nalo."

Mwisho wa kunukuu

Tujitahidi kuwa na FIKRA, Maoni na Mitazamo chanya na siku zote tujielewe tuna jukumu la kuiongoza SERIKALI YETU ili iyafikie malengo ya Utekelezaji wa ilani kwa kiwango kikubwa.
Tunao wajibu WA KUKATAA MITAZAMO HASI NA KUISHI KWA MAZOEA BILA KUJISUMBUA KUPATA ELIMU YA KUTUONDOLEA UJINGA.
Madhara ya kufuga Mitazamo hasi ndani ya mioyo yetu hutudharirisha mbele ya Jamii kwani nyakati zingine tunalazimika KUAMUA KUBISHA TU HATA KWA MAMBO YA MSINGI YANAYOONEKANA KWA UWAZI NA YA MUHIMU KWA JAMII.

Dkt Joseph Murphy Ph D, DD
Katika Kitabu chake cha The Power of Your Subconscious mind uk 47
Anatukumbusha,

" If you think negatively, Destructively, and viciously, these thoughts GENERATE DESTRUCTIVE EMOTIONS which must be expressed and find an outlet.
These emotions being of a negative nature are frequently expressed as ulcers, heart trouble, tension and anxieties."

Tunao uwezo WA KUACHANA NA UJINGA MIONGONI MWETU IKIWA TU TUTAAMUA KWA DHATI KUFANYA HIVYO KWANI MARA NYINGI TUNAYAWEZA MAMBO MENGI KWA KUYAAMULIA KUTOKA MIOYONI NA SIO KIJUU JUU KWA kuziendekeza njaa zetu ili tusifiwe na WAFADHILI WA MUDA WA NJAA HIZO ZINAZOTUFANYA TUJIKOMBE KWAO NA KUWA WAUMINI WA KULAMBA VISIGINO KWA KILA JAMBO HATA KAMA HALINA TIJA KWA JAMII.

Dkt Norman Vincent Peale
Katika Kitabu chake cha The Amazing Results of Positive thinking uk 143
Anatukumbusha,

" When you believe that a difficulty can be overcome, You are more than half way to victory over it already,
One of the greatest of all principle is that men can do what they think they can do."

Mwisho wa kunukuu

Inavunja moyo sana kuona UNAUMIZA KICHWA KUELIMISHA JAMII HALAFU ANATOKEA MTU BILA YA RESEARCH YOYOTE anakomaa kubishana bila points zenye mashiko na pasipo kuzingati wajibu na kiapo chake ndani ya CCM.
Anyway tusichoke.

Robert Schuller ,
Katika Kitabu chake cha Tough Time Never Last, But Tough People Do uk 147 - 148
Anatueleza,

" The Biggest people with the Biggest IDEAS can be shot down by the smallest people with the smallest minds."
" Think big Anyway"

" Give the World the Best you have and you'll get kicked in the teeth."
" Give the world the Best you have got Anyway."

Mwisho wa kunukuu

Tukisoma Kitabu cha TUJISAHIHISHE uk 16

Mwl JK Nyerere anatukumbusha,

" Japo baadhi ya Madhumuni ya Chama chetu ni kumpatia Elimu kila mtu,
Baadhi ya Wanachama wetu huwa na Mashaka na Wanachama wenye ELIMU.
SIYO kwa sababu ya Makosa yanayojulikana,
Lakini kwa sababu ya Elimu."
" Tabia inaleta mazoea ya kusema na KUKASHIFU ELIMU NA UJUZI kana kwamba ni Dhambi "
" Na hasa kwa sababu WAKOLONI WA ZAMANI walikuwa wanatuambia hatuwezi hili Wala hatuwezi lile kwa sababu hatuna ELIMU na ujuzi wa kutosha."

" Ni dhahiri kwamba Chama chochote ambacho KIMETAJA UJINGA , yaani UKOSEFU wa Elimu au ujuzi kuwa ni baadhi ya MAADUI WAKE,
HAKINA BUDI KUHESHIMU ELIMU NA KIITUMIE "

" Ni dhahiri kwamba yule ASIYETAMBUA UBORA WA ELIMU na ujuzi ni MJINGA ambaye chama (CCM) hakina budi kimsaidie kumwondolea huyo adui anaye msumbua yaani UJINGA"


Mwisho wa kunukuu








Kidumu Chama Cha Mapinduzi.






Mathias Mugerwa Kahinga
🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿
 
Back
Top Bottom