Elimu Picha: Yatakayokufanya uzidi kuwa dereva mzuri

Elimu Picha: Yatakayokufanya uzidi kuwa dereva mzuri

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2018
Posts
358
Reaction score
675
1. Angalia Mbele: Hapa tunazungumzia madereva waopenda kuendesha gari huku wakiwa wanatumia sim au kugeuka geuka nyuma au maongezi na abiria wako. Mambo hayo na yanayofanana na hayo yanaweza kumtoa dereva kwenye utulivu wa barabara na hivyo inapotokea dharula kama watumiaji wengine kukatiza ghafra mbele yake huweza kusababisha ajali.

B2A533FC-E865-4AF1-8137-3884368D67F1.jpeg


2. Usiisogelee sana gari ya mbele yako. Zaidi tunaongelea gari inapokua kwenye mwendo, ambapo imekua jambo la kawaida kwa madereva wengine kuwasogolea sana wenzao bila kujali dharula inayoweza kumpata huyo wa mbele kama kufunga break za ghafra au kupasukiwa tairi jambo linaloweza kusababisha ajali hiyo ikukumbe na wewe kwa kua uwezekano wa kukimudu chombo ukiwa kwenye mwendo na karibu zaidi ya mwenzio wa mbele ni mdogo.

F113800A-1D67-4F2C-8DF0-78C5BFA53CAA.jpeg


3. Epuka Break za ghafra. Matumizi ya break za ghafra iwe ni chaguo la mwisho, lakini muhimu ni kuhakikisha unakadiria barabara yako na hivyo ushike break taratibu. Iwapo utashika kwa ghafra huku gari ya nyuma yako ikiwa imekufata kwa karibu kuna uwezekano wa kutokea ajali. Mara nyingi hili linatokea kwa madereva wanapoamua ghafra kusimama kwenye zebra ili watembea kwa miguu

10125DC0-4654-4B27-B7BC-BC25FEB1BC15.jpeg


4. Gia ya Manual. Watanzania walio wengi tunaotumia gari binafsi hatufahamu namna ya kutumia gari zenye gia ya manual, badala yake tumezoea Automatic, lakini dereva mzuri ni yule anayejifunza kutumia gia za aina zote yaani Manual na Automatic kwa kua faida ya Manual ni kua inachangia kwenye matumizi madogo ya mafuta, lakini pia humuongezea dereva ujuzi zaidi awapo barabarani kwa kua kila kitu anakifanya yeye mwenyewe manually. Zaidi wakati wa dharula dereva hatohitaji aje dereva mwingine kutoka mbali aendeshe hilo gari manual bali yeye mwenyewe ataingia na kuendesha gari hilo.

1C6D2A04-BEAC-4343-9470-BA948A8882FC.jpeg


5. Usikae upande uwapo kwenye usukani. Baadhi ya madereva hukaa upande kwenye magari yao jambo linalowafanya kujisahau na kukanyaga mafuta badala ya break au break badala ya mafuta au mda mwingine kujikuta akikanyaga vyote kwa pamoja hali inauoweza kusababisha ajali. Na kwa safari ndefu mkao wa upande utamfanya dereva ahisi maumivu ya mgongo au kiuno. Inaushiliwa kukaa kwa kunyooka kwenye usukani na kurelax mwili huku ukiwa makini na watumiaji wengine wa barabara.

E5C2E984-BFB5-4E3E-8538-1FF23327E46A.jpeg


6. Kurudi nyuma. Hili ni tatizo kubwa kwa akina mama wengi na baadhi ya wababa pia. Ni muhimu kujifunza kwa kufanya mazoezi ya kurudisha gari yako nyuma bila kuhitaji msaada kwa kua kuna siku utahitaji msaada utakosa na hivyo unaweza kuligonga gari lako kwa kushindwa kufanya makadirio mazuri kwa kutumia vioo vyako ya pembeni na ndani, unapoona unashindwa kabisa kutumia vioo basi geuza shingo ili kuweza kufanya hayo makadirio na kuona vizuri nyuma.

929002FE-9106-4A85-BFE4-3AC19D5F4036.jpeg


7. Kuegesha gari. Kwa sasa kwenye miji mikubwa kuna majengo ya kisasa ya parking ambazo zinakua zimebanana na hivyo kuwapa uoga baadhi ya madereva kupaki gari katikati ya magari mengine kwa kuhofia kugonga. Hili nalo tunashauliwa tuweke uoga pembeni tujiamini na kufanya mazoezi taratibu na kwa tahadhari mpaka tutazoea. Haipendezi unaingia kupaki unaomba msaada kwa mtu mwingine akuingizie gari hiyo kwenye parking husika.

A99D61D1-C29A-4A25-8386-DE6EF701C5A1.jpeg


8. Kuegesha gari katikati ya gari zinafuatana. Hili ni tatizo kubwa kwa madereva wengi kwa kua kukadiria kwetu ni tatizo na hali ya kutojiamini. Njia nzuri ya kupaki gari katikati ya gari zilizofuatana ni kuingia kwa rivasi. Ikiingia kwa rivasi uwezekano wa kupaki gari ikiwa imenyooka ni mkubwa kuliko kuingia kwa mbele inaweza kusababisha sehem ya nyuma ibaki upande wa barabarani.

A816C0E9-268A-4F79-98C9-A496FB9BBA66.jpeg


9. Uvumilivu. Tunatakiwa kua wavumilivu kwenye uzurmbe unaofanywa na madereva wengine kwa kua ukiruhusu hasira ikutawale unaweza kujikuta unafanya mambo ya ajabu na ukapata matatizo hapo barabarani. Mfano umekwazuraza na gari ya pembeni yako inatakiwa uelewe kwamba ajali zipo kwa mtu yoyote anayetumia barabara hivyo iwapo mtu kakugusa bahati mbaya lazima utumie busara kuzungumza naye na kuyamalizq badala ya kutumia nguvu na matusi. Hii piq kwa wale ambao kukiwa na foleni kidogo wanapiga honi akiona haitoshi anamfaya mwenzie kumtukana, hili pia si jema na unaweza kupata matatizo ambayo hukuyategemea iwapo utakutana na mtu mkorofi zaidi yako.

6249AFA3-C7AA-42DA-A2FC-3882D4A89307.jpeg
 
Namba 8 na namba 7 unaweza kuaibika maana sio mchezo
 
Hilo la uvumilivu muhimu sana, yani ukiwa barabarani inabidi u assume kila dereva ni chizi na hapo utakuwa salama
 
Back
Top Bottom