Papaa Kinyani
JF-Expert Member
- Feb 25, 2013
- 1,459
- 699
ELIMU SHULENI NA KUFELI WANAFUNZI
Mitaala ya Elimu ambayo ndio inayounda uendeshaji wa elimu shuleni imezungumzwa sana kipindi hiki. Bahati mbaya wakati hili likiendelea wanafunzi nchi nzima wamefeli sana. Kwa fikra ya kawaida, ni rahisi kuunganisha kufeli kwa wanafunzi na mitaala hiyo ambayo inaitwa mibovu.
Wadau wengi wa elimu wamesema mitaala hailingani na maisha ya siku hizi. Maisha ya siku hizi ni yapi? Kwa mfano katika umbile la binadamu ambalo wanafunzi wanajifunza, ni hilo hilo halibadiliki, je kuna umbile jipya?
Mtaala wa Tanzania utalingana na maisha ya Tanzania na sio maisha ya Australia au kwingineko. Maisha ya jamii yetu na viwanda vyetu vitabadilisha mitaala yetu ili wanaohitimu mitaala hiyo wawe na manufaa kwa maisha hayo. Maisha yetu yatabadili mitaala na sio mitaala ibadili maisha yetu.
Mitaala ambayo ni kila kitu kinachofanyika shuleni ipo na inahusisha ratiba ya vipindi kwa siku, kwa wiki, kwa mihula katika mwaka na kwa miaka.
Mitaala hiyo imeandikwa kwa urahisi kwa kuwekwa katika kila mwanzo wa kila muhtasari ili kurahisisha matumizi yake. Kama mitaala hiyo ni mibovu na wanafunzi wakafundishwa kwa mitaala hiyo na mitihani ikatungwa kwa mitaala hiyo hiyo mibovu, wanafunzi wangefaulu mitihani ila taaluma yao isingeendana na maisha ya sasa. Hivyo, kufeli kwa wanafunzi mwaka huu hakuna uhusiano wa moja kwa moja na mitaala.
KUFELI mitihani kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka huu kwa maoni yangu kunatokana na jinsi mtihani huo ulivyoendeshwa. Hasira inayotokana na wanafunzi kufeli kutokana na uendeshaji wa mitihani mbovu ni sawa kabisa na ile inayotokana na mitihani kuvuja. Kuna mdau wa elimu alichangia kuwa kufeli kunatokana na kutovuja mitihani. Hii si kweli kabisa. Je waliofaulu wachache waliiba mitihani ambayo haikudhibitiwa? Mitihani lengo lake ni kuchambua walioelewa na wasioelewa.
Ni muhimu Tume iliyoundwa ichunguze usahihishaji, uchambuzi wa alama za watahiniwa hadi utoaji wa matokeo pale NECTA. Vile vile tume ikachunguze shughuli za kielimu katika Wizara ambazo zinapelekea udhaifu katika utoaji wa elimu ikiwa ni pamoja na uingizaji wa vitabu vibovu shuleni japo vimepata ithibati ya EMAC.