Elimu: Sio kila mbio ni Marathon, waandaaji waaswa

Elimu: Sio kila mbio ni Marathon, waandaaji waaswa

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
Waandaaji wa mbio za Barabarani nchini Tanzania, wameaswa kuacha kutumia ne no “MARATHON” kwa kila mashindano wanazoanzisha, kwa kuwa zipo tofauti; Marathoni ni kilomita 42, wakati wanaoanzisha mbio za kilomita 21 pia wanaziita Marathon badala ya Nusu Marathoni (half marathon); kupitia ukurasa wa Shirikisho la Riadha Tanzania ; Wameandika hivi;

“……Marathon, ni Mbio Ndefu za Barabarani zenye kukimbiwa kwa umbali wa kilometa Arobaini na Mbili na pointi kama mbili (42.195 Kilometa) , mara nyingi tunafupisha kwa kuandika 42K , hivyo tupate elimu hiyo.

Half Marathon, ni mbio zenye kukimbiwa kwa urefu wa kilometa Ishirini na moja na pointi moja hivi, ( 21.0975 Kilometa) , mara nyingi tunafupisha kwa kuandika 21K, hivyo tupate Elimu Hiyo.

Mwenye rekodi ya Muda bora Tanzania wa Marathoni kwa Sasa ni Gabriel Gerald Geay, (2:03:00)….”
 
Back
Top Bottom