PerfectTz
Senior Member
- Jun 27, 2019
- 108
- 206
Namshukuru Mungu kwa kuzaliwa Tanzania pia kwa kunipa nafasi ya leo kusema na Watanzania, viongozi wa Umma na Jamii kwa ujumla, Makala hii itahusisha mada kuu Tatu zenye Tija ya Elimu, mada zote tatu zina mchango mkubwa sana kwa jamii yetu pendwa ya Tanzania ikiwa serikali kwa kushirikiana na asasi mbalimbali, Raia wema na mashirika binafsi vitashirikiana basi imani yangu ni kua maendeleo ya Nchi na watu yatafika kwa haraka na kwa kasi pia Uzalendo na Maendeleo bora nianze na Mada ya kwanza;
Mfumo wa kwa Mujibu wa Sheria;
Mfumo huu umewekwa na Serikali kwa ajili ya kuwafundisha vijana wanaohitimu kidato cha sita kuhudhuria mafunzo ya awali ya kijeshi kwa wiki kadhaa, Ni jambo jema na lenye lengo la dhati kwa maslahi ya Serikali na Jamii lakini ningependekeza badala ya vijana kuhudhuria mafunzo ya kijeshi uwekwe utaratibu wa vijana wote wanaohitimu kidato cha sita na wanaoishi maeneo ya karibu na shule hizo bila kujali ikiwa ni wanafunzi au sio wanafunzi, wanakijiji walio vijana wapewe mafunzo ya ufundi stadi wa vitu mbalimbali ikiwemo ufundi umeme, ufundi uashi, mabomba ya maji, magari na kadhalika kwa muda ule ule ambao wangetumia kwenda jeshini kwa mujibu wa sheria
Ili kulipa nguvu suala hili basi Serikali iongeze mchango wa shilingi elfu 5 au zaidi kidogo kadiri ya idadi ya wanafunzi na gharama za uendeshaji wa mafunzo hayo kwenye michango ambayo mwanafunzi anayefika kidato cha tano na sita ili kufanikisha masuala ya malipo kwa walimu maalumu wa ufundi stadi na nyenzo zao zingine.
Na kwa kupendekeza zaidi, wale ambao hawatakuwa wanafunzi wa kidato cha sita (vijana wanakijiji, kidato cha nne, wanachuo wanaosubiri ajira mtaani) wawekewe utaratibu wa kuhudhuria mafunzo hayo kwa gharama zile zile ambazo zitapangwa ambazo kimsingi nategemea zitakuwa za chini sana kwa msaada wa Serikali + michango kidogo kutoka kwa wanafunzi na vijana wengine niliowataja hapo juu.
Kwa kufanya hivi serikali kwanza itakuwa imepunguza gharama kubwa za uendeshaji wa mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria kwa vijana ambao wengine huwa hawahitaji mafunzo hayo, pia Serikali itajihakikishia kupunguza tatizo la ukosefu wa Ajira kwa sababu vijana wengi watakua na mwanga na utaalamu utakaowasaidia kujipatia kipato na kujiajiri, pia uhalifu mitaani utapungua kwa kuwa vijana wengi watakuwa na kitu cha kufanya badala ya kukaa makundi makundi kushauriana kufanya uhalifu.
Siku Ya Kitaifa Ya Upendo na Uzalendo;
Napendekeza kuanzishwa kwa kwa siku maalum ya Kitaifa kwa ajili ya kuenzi na kukumbushana juu ya kuoneshana upendo baina ya Serikali na jamii, jamii kwa jamii, mashirika ya Umma na ya binafsi, mfano Polisi kwa wananchi, Taasisi za Fedha kwa wananchi, Taasisi za Serikali kama vile TRA na walipa kodi. Hii itahusisha siku hiyo kutoa fursa maalumu kama vile mikopo nafuu isiyo na riba, punguzo kwenye kodi za kila siku, bidhaa kuuzwa kwa bei isiyo na kodi kwa siku hiyo nchi nzima, kushushwa gharama za nauli kwa siku hiyo pamoja na Rais kuongea na jamii moja kwa moja kwa njia ya Televisheni na simu ya mkononi.
Jamii iliyokosa uhuru kama vile wafungwa kutembelewa na Rais, mawaziri na wabunge, kutembelea wagonjwa na kutoa misaada na fursa kwa makundi maalumu, mfano kupata leseni za biashara kwa gharama nafuu siku hiyo, leseni za udereva kwa vijana pamoja na bima yenye bei punguzo kwa siku hiyo, punguzo la gharama za upigaji simu na matumizi ya mtandao, Hii itaongeza ari ya uzalendo, itapunguza matukio ya ukatili kwani jamii yenye upendo haiwezi kutendeana maovu, itaongeza furaha ndani ya nchi, itaongeza urafiki baina ya jamii na Serikali mfano Polisi na Raia, Jeshi la wananchi na Jamii, Raia huru na wafungwa, pia itatoa hamasa kwa watu kusaidiana kupeana fursa kwa upendo pasipo kuiachia serikali jukumu lote. Na sasa nimalizie na mada ya tatu.
Kuanzishwa kwa Taasisi ya usuluhishi Wa Kesi Kabla ya kwenda Mahakamani kwa Njia ya Amani na Mazungumzo;
Iko wazi kuwa saikolojia ya mwanadamu wakati mwingine inakua na hofu inapoona mazingira ya kesi ni vituo vya polisi au mahakamani na wakati mwingine hakukua na sababu kubwa za kufika huko kote, pia mtu kutokana na mapungufu yetu kiuumbaji baadhi yetu tunakosa uhuru na amani ya moyo kujielezea au kushauriwa namna bora ya kumaliza kesi ambazo nyingine zinahitaji ushauri tu na mazungumzo, Nashauri Serikali ipachike Taasisi hii kwenye wizara mojawapo ambapo serikali inaweza kutumia ofisi za Serikali ya mitaa kuwa kama ofisi za usuluhishi na upatanisho kwa Wananchi wenye migogoro mbalimbali mfano madeni na kufarakana, kwa kufanya hivi serikali itakuwa imepunguza idadi ya kesi nyingi mahakamani ambazo hazina ulazima wa kuwepo huko, pia Serikali itapunguza Gharama za uendeshaji wa magereza kwani idadi ya wafungwa itapungua kwa sababu kesi nyingi zitasulushishwa na Taasisi hii ya upatanisho na usuluhishi na hivyo kuongeza idadi ya nguvukazi itakayokua Huru Uraiani.
Mwisho; Andiko hili halipo tu kwa ajili ya kushinda shindano hili bali kwa manufaa ya Nchi yetu ikiwa wenye Nchi (Wananchi na Serikali) Tutaona inafaa kufata yaliyopo humu, Hata kama halitashinda basi ninaomba Serikali ilipitie huenda kuna mawazo mengine yatazaliwa kutokea humu au haya yakibadilishwa kidogo yaweza leta tija kwa Taifa na Jamii, Asanteni Sana na Mungu Awabariki.
MUSHI5
Email; shukurucyprianjr5@gmail.com

Upvote
1