Elimu ya Biashara: Mnafiki na Unafiki

Elimu ya Biashara: Mnafiki na Unafiki

mojax

Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
13
Reaction score
23
ELIMU BIASHARA

MNAFKI NA UNAFKI

Unafki ni ile hali ya nafsi ya mtu fulani katika harakati za kukubali maneno au hali na kutotenda makubaliano ya maneno hayo au kuyatenda kivingine na kuyakanusha maneno na matendo husika. Unafki unaweza kuwa hali ya mtu fulani kutopenda maendeleo ya mwingine au kuchukizwa na maendeleo ya mtu mwingine pasipokua na sababu maalum au ya msingi. Mnafki ni mtu ambaye ana nafsi yenye hali ya Unafki ndani yake. Mnafki hutumia Fitina, kuyabadilisha maneno na kuyakanusha kanakwamba si yeye alihusika wala kuyasema.

Mnafki ni mtu ambae haoni tabu Kukutia hasara au kukurudisha nyuma au kukudidimiza licha ya kujua umetumia nguvu nyingi kufika hapo ulipo au hata kama nayeye amechangia 60% ya wewe kuwa hapo ulipo au ya mafanikio yako, ila ukididimia atafurahi kwa sababu mtakua sawa au atakua amekupita. Mtu mnafki hana sura maalum yenye kuonyesha kama ni mwongo katika maneno au matendo yake au kuonyesha anakufitini, bali mtu mnafki dalili zake zinaonekana au zinatambulika kutokana na kauli ya nafsi yake na matendo yake.

Katika Maisha kuna watu huwa hawapendi kuona wamepitwa (wamepigwa gepu), hivyo hupandwa na hali ya wivu wa chuki juu ya maendeleo ya mwingine ambaye hapo mwanzo walikua sawa au alikua amempita au alimsaidia yeye alafu akaja kumpita. Kuna mwanagospel aliimba, "Unapoianza safari wanakutia moyo, unapoonyesha mafanikio wanaibua vikwazo, maadui ni wengi katika maisha yako, sio wote wafuraiao mafanikio yako". Hata nyota ndogo aliimba kuna watu na viatu, kina "viatu" ndo hawa wanafki.

"Shetani anaweza akawa amerelax zake Beach anakunywa Dafu huku Binadamu tupo busy tunafanya kazi yake (tunafanya ushetani)". Jiangalie, Haujazungukwa na Wanafki?

JIKUNG'UTE, JIPANGE, ANZA.

By Man Dea
Instagram account: Elimu_biashara
 
Back
Top Bottom