Elimu ya bima.

Tasia I

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2010
Posts
1,223
Reaction score
193
Wakuu nawasalimu.
tafadhali mwenye kujua vyema juu ya bima- conprehensive na thirdparty anifafanulie.
faida na hasara na maelezo mengine muhimu.
na pia hatua zinafuatwa ili kukata bima hizi.
nawashukuru.
 
kwa haraka haraka tu kuna aina kama nne za hii kitu ambayo umeulizia
1: Ordinance
Hii ilikua inatolewa zamani hapo miaka ya nyuma na NIC na ilikua inahusisha compensation ya ajali zote zitakazotokea kwenye public roads tu. Ukipata ajali kwenye feeder roads au mitaani kwenu hulipwi.

2: Third Party
Hii inahusisha compensation kwa body injury, material damage and fatal accident. Kiwango cha premium hutofautiana toka kampuni moja hadi nyingine depending on how they charge whether kwa cc au kwa thamani ya gari. Hailipwi gari moja kwa moja isipokua damage ambayo hiyo gari itafanya kwa mfano gari yako ukiikatia third party ikagongana na gari ingine, ile gari iliyogongwa ndo itakayolipwa na sio gari yako wala wewe. Ndo maana halisi ya third party aka mtu wa tatu. Viwango pia vinatofautiana vya malipo. Makampuni mengine hulipa mpaka milioni 60 kwa third party.

3: Third Party Fire & theft
Tofauti ya hii na hapo juu ni kilichoongezeka tu hapo fire and theft, yaani gari ikiungua na kuibiwa inalipwa. Premium yake pia inatofauti kwa mfano kama third party ya kawaida ni 60,000/- then utatakiwa kuongeza 2% ya thamani ya gari kwenye hiyo elfu 60.

4: Comprehensive Insurance
Aina hii ya bima ukikata gari yako inamaanisha gari yako ikigongwa ama kugonga italipa na kulipwa na isistoshe wewe binafsi kama utakua umepata nayo ajali ukaumia utapata personal accident compensation. The only thing ambayo itakufanya usilipwe comprehensive ni kama umesababisha damage kwa gari makusudi kwa kukusudia wanaita malicious damage kwa lugha ya ki-bima bima.

Need you say more.
Thanks
 
I second on your post hekimatele..

Faida ya kuwa na comprehensive japo ni ghali kulinganisha na third party mtu unakuwa more secured na usafiri wako na pia wewe binafsi kwa maana ya kwamba usalama wa mali yako ni guaranteed kwani ina-cover risk mbalimbali..

Third party unakua na usalama mdogo endapo utasababisha ajali kwani hutalipwa chochote kutoka kwenye kampuni yako.

Mimi nakushauri kama unanunua gari lipya kabisa ni vyema ukajikaza ukakata comprehensive!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu heshima kwanza kwenye signature yako, :focus: Comprehensive ina madaraja? Yani kwa mfano gari mpya na chakavu (used) zinakatwaje bima zake hizi?
 
Mkuu heshima kwanza kwenye signature yako, :focus: Comprehensive ina madaraja? Yani kwa mfano gari mpya na chakavu (used) zinakatwaje bima zake hizi?

Mkuu comprehensive inategemea na gari lako kama ni private (shughuli binafsi) au ni commercial (shughuli za biashara) hapo ndio kuna madaraja lakini kuhusu gari kuwa lipya au chakavu iyo haina madaraja isipokua bei inachajiwa kulingana na thamani halisi ya gari..

Mfano: gari lako ni mil40 na bima comprehensive ni 3%, hapo utazidisha rate (3%) na sum insured (40mil)

Ni vizuri kupita kwa mabroker wa insurance kwani wao wanaweza ku-bargain na makampuni ya bima na pia wanauzoefu wa mambo hayo esp kipindi cha claims..
 
Hivi kuna kikomo cha gari kukatiwa bima? Nimeenda kata bima kubwa naambiwa gari yangu muda wake wa kukatia bima umeisha, nimepewa ya kawaida tu! Msaada kwa anaejuwa
 
Hivi kuna kikomo cha gari kukatiwa bima? Nimeenda kata bima kubwa naambiwa gari yangu muda wake wa kukatia bima umeisha, nimepewa ya kawaida tu! Msaada kwa anaejuwa
Kuna baadhi ya Makampuni ya yanakwepa risk ya kutoa bima kwa magari yenye umri mrefu. Kenya hivi karibuni baadhi ya makampuni yalikataa kutoa comprehensive kwa aina flani ya magari kwa sababu spea zake ni ghali.

Ila nenda kwa brokers watakupa muongozo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa magari ya biashara mf. haice gharama ya bima comprehensive rate yake inaendaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…