Bongo porojo nyingi sana .Siasa kwenye elimu ndio inapelekea Elimu kushuka ubora kila kukicha.Hao wanaosema India ,China, Malaysia sijui kama mnatakwimu sahihi.Tanzania chuo kinachoongoza kwa Ubora ni UDSM ambapo Kwa East Africa ni chuo cha 3 kwa ubora baada ya Makerere na University of Nairobi.UDSM kwa africa ni chuo cha 38 ambapo Hakuna chuo kingine cha Tanzania kwenye 100 bora za vyuo vya Africa.Kwa dunia nzima UDSM ni chuo cha 3,438 kwa ubora.
Sasa sizani kama kuna mikakatii madhubuti ya kuboresha Elimu ,Ndio maana wengi wanaosoma vyuo vya nje(Haswa kwa vyuo vya Malaysia,China,Japan,nd Korea , Indonesia,Philipines and Russia ) wakirudi wanakuwa na uwezo (wamepanuka kimawazo/fikra ) hii ni kutokana wengi wanaoenda kusoma vyuo vya katika nchi hizo wanapata Scholarship na wanakwenda kusoma kwenye vyuo vyenye ubora .
Sasa turudi huko UK ,watanzania wengi wanaenda kusoma vyuoka kama Mwana FA alisoma chuo kinaitwa Coventry ambacho ni chuo cha 1,713 kwa ubora duniani ( Kuna vyuo Africa vinakizidi kwa Ubora hata East africa-Makerere ni cha 1,256 duniani ),vyuo vingine ni kama London Business School 1,524 na University of London -1,683.Ukilinganisha ni kwamba Watanzania wanaoenda Asia wanasoma vyuo bora kuliko wanaoenda UK ambako kusoma kwenye vyuo vyenye ubora wa juu zaidi kwa UK ni gharama kubwa hata qualification zinazohitajika ni za juu kwa baadhi.Wengi hawawezi kwa sababu wanakuwa wanajilipia wenyewe ama wazazi wao.
Wapo watanzania wachache sana wanaosoma/waliosoma kwenye vyuo vilivyopo kwenye 100 USA na kwingineko ,ila kwa miaka mingi watanzania wengi wanasoma vyuo vya UK,Russia na Asia kwa wingi ukilinganisha na USA na kwingineko.Bila kusahau Kenya na Uganda wapo wengi pia.
Rank ya vyuo bora kwa Tanzania
Jina nafasi kwa dunia
1.UDSM 3,438
2.SUA 8,427
3.Hubert Kairuki Memorial University 8,819
4.Open University of Tanzania 9,335
5.Mzumbe University 10,107
6.Muhimbili University College of Health Sciences 11,191
source
Ranking Web of World universities: Top Africa