Complicater
Member
- Jul 28, 2022
- 16
- 31
UTANGULIZI
Katika ulimwengu huu wa tatu au miongoni mwa nchi zinazoendelea, hususani Tanzania vijana wengi wanao hitimu Vyuo vikuu wamekuwa wakikosa dira ya maisha, mtaani baada ya kuhitimuelimu ya juu. Na hii imekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya taifa la Tanzania.
Hii ni kutokana na aina ya masomo yanayotolewa na vyuo vingi hapa nchini Tanzania kutokuwa na dira ya kwenda kumkomboa muhitimu. Dhana ya kuhitimu elimu ya juu imekuwa ikimjengea imani muhitimu kupata ajira zinazotolewa na serikali na si kujiajiri yeye binafsi (muhitimu).
Dhana hii imekuwa kikwazo katika utekelezaji wa malengo ya taifa ya kutaka muhitimu kutumia ujuzi na ufahamu alioupata chuoni (elimu ya chuo) na kuleta mabadiliko halisi ya maisha, mtaani. Kukosekana kwa maarifa, (miongoni mwa wahitimu) kunaweza kusababisha kuongezeka kwa wimbi la jamii iliyojaa uvivu, wizi na uharifu unaoweza kupelekea maisha yao kuwa hatarini na wakati mwingine kupelekea vifo.
Lengo la andiko hili ni kutaka kuonesha namna ambavyo vijana wahitimu wanaweza kutumia elimu ya chuo kama fursa ya maendeleo ya jamii na Tanzania kwa ujumla pasipo kutegemea Zaidi ajira kutoka serikalini na kuonesha namna serikali inavyoweza kuwaunga mkono pindi wanapokuwa na huitajia wa kupata mitaji/ rasilimali fedha katika kujikwamua kiuchumi na kijamii. miongoni mwa shughuli ambazo muhitimu anaweza fanya na zikamfanya asitegemee ajira kutoka serikalini, ni pamoja na;
Kushona na kuuza nguo.
- Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano
-Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.
-Kufungua steshenari, kuuza vitabu (kusambaza) na vifaa mbalimbali katika shule na vyuo.
-Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza bisi na kuziuza.
-Kusajili namba za simu na kuuza vocha
-Kuuza Mitumba
-Kufungua banda la chakula na chips
-Kuuza baiskeli
-Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe, vijiko,
-Kuuza marumaru
-Kuuza kokoto
-Kuuza mchanga
-Kufundisha Tuisheni
-Biashara za bima
-Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
-Biashara za kitalii
-Kampuni ya kuchimba visima
-Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wakujitegemea
-Kuuza mkaa
-Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
-kuanzisha Kampuni ya kupima ardhi
- Kuchapa (printing) magazeti
-Kuuza magazeti
-Kuchimba mafuta
-Kiwanda cha kutengeneza mabati
-Kiwanda cha kutengeneza samani za ndani
-Kiwanda cha kutengeneza matairi
-Kutengeneza vitanda vya chuma
Hizo hapo juu ni baadhi ya shughuli zinazoweza kufanywa na wahitimu wa vyuo katika kujiingizia kipato kitakachoweza kuwasaidia kuendesha maisha ya kila siku, pamoja na kukuza kipato katika kutekeleza dira ya taifa kimaendeleo.
Katika hilo, Serikali haijaacha mtu, hususani wahitimu katika kuwasaidia kupata mikopo kulingana na uhijataji wa shughuli wanazofanya. Selikali kupitia Sera ya Taifa ya kuwezesha Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004, Sera ya Huduma Ndogo za Kifedha ya Taifa ya mwaka 2017 (NMP, 2017) na Sheria yake ya Mwaka 2018 (MPA, 2018). Katika kuhakikisha hili Baraza limeratibu mifuko ipasavyo, na kufanikiwa kuigawa katika makundi makuu manne ambayo ni Mifuko inayotoa mikopo moja kwa moja kwa walengwa, Mifuko inayotoa ruzuku na Programu za Uwezeshaji.
Mifuko hiyo hutoa dhamana kwa kushirikiana na Taasisi za fedha. Ilikuwezesha kupata fedha za kujikwamua kiuchumi na kijamii kwa wote wenye uhitaji hasa wahitimu wa vyuo.
MIFUKO INAYOTOA MIKOPO MOJA KWA MOJA KWA WALENGWA
Vikundi vifuatavyo vinaweza kumuongoza muhitaji kupata mkopo wa kifedha, wa moja kwa moja ambavyo pia vipo chini ya umiliki wa serikali.
1.Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (Youth Development Fund – YDF)
2. Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (Women Development Fund – WDF)
3. Mfuko wa Taifa wa Kuendeleza Wajasiriamali Wananchi (National Entrepreneurship Development Fund – NEDF)
4. Mfuko wa Kutoa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo (SELF Microfinance Fund)
5. Mfuko wa Mzunguko katika mikoa (SIDO RRF)
6. Mfuko wa Taifa wa Watu Wenye Ulemavu
KUMBUKA: Mifuko yote iliyo orodheswa hapo juu inapatikana kuanzia ngazi ya wilaya, manispaa na Mkoa kote nchini
HITIMISHO
Mifuko muhimu iliyo orodheshwa hapo juu ipo chini ya umiliki wa serikali na haina maana kuwa imekaa pasipo kufanya kazi au kutokuwa na fedha lahasha! bali imekosa waombaji wa kutosha wa huduma.
Ni wakati sasa kwa vijana na wananchi wote wa Kitanzania kutumia mifuko hiyo ya maendeleo kujipatia mikopo kwa maendeleo yao binafsi na Tanzania kwa ujumla bila kuwa na mitazamo ya kidhanifu kwamba mifuko hiyo ipo tu na haifanyi kazi, hii ni kwasababu serikali hutenga karibu asilimia 10 ya fedha, kila mwaka wa serikali unapoanza kwaajili ya maendeleo ya vijana, Kupitia vijana wahitimu ambao ni kama nguvu kazi ya taifa wanatakiwa kuamka kifikra katika kuchangamkia fursa za maendeleo pasipo tegemea ajira kutoka serikalini kwa kutumia ujuzi mdogo waliopata kutoka chuoni na kuufanya wenye kuleta tija katika jamii inayo wazunguka na Tanzania kwa ujumla, vijana tuamke, tuibue miradi iliyokufa, tuunde taasisi binafsi zitakazoleta maendeleo pia tuunde makundi ya uzalishaji yatakayo turahisishia kupata mikopo kwa urahisi zaidi.
Pia Serikali inatakiwa iendeshe mafunzo yatakayo wawezesha kung’amua fursa zilizopo na namna ya kuzitumia kwa wanafunzi wahitimu pamoja na wananchi wote wanaotaka kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo ya kifedha inayotolewa na serikali, hii ni mbadala wa elimu inayotolewa na vyuo. Ili iweze kuwasaidia kuendana na hali ya maisha ya sasa.
Karibuni wadau kwa maoni

Attachments
Upvote
1