SoC04 Elimu ya chuo wabadilishe system ya kufundisha

SoC04 Elimu ya chuo wabadilishe system ya kufundisha

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
May 28, 2024
Posts
8
Reaction score
12
Ninaguswa sana na jinsi ya elimu yetu Tanzania, vitu tunavyofundishwa darasani sio vitu unavyokutana navyo kazini. Kuna umuhimu wa kuboresha ufundishaji wa elimu ya chuo kikuu.

Ninaamini elimu tunayopewa chuo inatupa maarifa lakini tukiangalia baadhi ya vitu nadhani kuna haja ya kubadilisha baadhi ya mambo kwa kubadilisha mfumo wa kufundisha na pia kuwe na kitengo maalumu kila baada ya somo kiwe kinafanya tathimini kitasaidia kufanya walimu wajitahidi kufundisha vizuri zaidi maana wanajua wanakaguliwa.

Mimi ninashauri mambo yafuatayo yafanyiwe kazi ili tuweze kuwa na elimu bora zaidi na kuwa na wahitimu bora.
  • Walimu ambao wanapaswa kufundisha baadhi ya masomo mfano biashara, uchumi , uwekezaji, bajeti, sheria n.k. Walimu wawe wanachaguliwa kutoka kwa watu ambao wamesoma na wamefanya uwekezaji au ni wafanyabiashara wakubwa auwa kati na wadogo ili wakati anafundisha atufundishe vitu ambavyo viko kwenye soko halisi ili mwanafunzi akitoka chuo aweze kwenda mtaani na kumudu kupambana kutokana na soko.
  • Walimu waache kufundisha kwa kuwafanya wanafunzi wawe wanakariri handhouts zao na wawe wanafundisha vitu venye hualisia. Mwanafunzi awe na uwezo wa kujibu maswali sio kwa kukariri handhouts lakini kwa kuelewa.
  • GPA isiwe kigezo cha kuchagua kuwa mwalimu wa chuo, waangalie pia uwezo wa kufundisha na kuchukua watu ambao wamebobea katika kazi fulani maana kikubwa wanafunzi wanapaswa kuelewa vitu ambavyo wataenda kufanyia kazi. Unakuta chuo kilichukua mwalimu ambaye ana GPA lakini uwezo wake wa kufundisha sio mkubwa pia unakuta mwalimu aliye na GPA kubwa alichukul;ia akaenda masters then akafanya PhD na akabaki kufundisha lakini hana exposure ya kitu ambacho anafundisha Zaidi ya shule yake. Mwisho wa siku anakuwa anafundisha kutokana na vitabu alivyosoma lakini hana uzoefu wa kazi au kujua changamoto ambazo ziko katika hiko kitu anachofundisha.
  • Chuo kipunguze kufundisha nadharia zaidi na wawekeze katika kufundisha vitu kwa vitendo kwa hiyo wakati wanafanya baadhi ya masomo kuwe na case studies ambazo kwa sasa zinaendelea kwenye duniani na waweze zileta katika darasa na kudiscuss na kuona jinsi gani watu waliokazini wangefanyia kazi ili kujenga uwezo wa wanafunzi ambao watakuwa waajiriwa wa baadaye.
  • Vitabu vya kozi viwe vinavyoendana na mazingira yaani tekinologia imebadilika na system ya kufundisha ibadilike. Sio mwalimu anakuwa na handhouts zake za miaka 10 au 20 ambazo unaweza kuchukua kwa mtu aliyesoma hata miaka iliyopita.
  • Pia wanafunzi wawe na uhuru wa kufanya evaluation ya kila mwalimu na ile valuation itumike kuangalia ubora wa mwalimu, yaani chuo kiwe na kitengo maalimu cha evaluation na kufanya uchunguzi kwa walimu ambao wanao na ikionekana kwamba uchunguzi uko sahii mwalimu aondolewe kwenye chuo husika na aangalie kufanya mambo mengine au awekwe kwenye vitengo vingine kama vitamfaa.
  • Pia vyuo vya Tanzania wanaweza wakawa na walimu hao hao wenye GPA kubwa lakini wakaongeza tu kuwaarika watu wanaofanya kazi wanazozifundisha kufanya case study ambayo inaendelea kwenye soko la sasa. Mfano mwalimu anayefundisha Uwekezaji anaweza kualika watu waliofanya uwekezaji mbalimbali wakaweza kuelezea walianza vipi kuwekeza na kuonyesha changamoto anazozipata katika uwekezaji na baadhi ya njia za kutatua changamoto. Wawekezaji wanaweza kualikwa 3 kwa kila somo ili wanafunzi wapate kujifunza au saa nyingine somo usika likafundishwe kwa mwekezaji husika wanafunzi waende kujifunza kwa wiki moja iwasaidie kupata motivation za kutosha ili wajue na wao wakitoka chuo watawezaje kuwekeza.
  • Chuo kwa kila course kuwe na vitabu ambavyo viko updated, kuwe na case studies na baadhi ya papers bora ambazo angalau kumi mwanafunzi awe anasoma ili kupata maarifa zaidi.
  • Pia kuwe na course ambazo ziko sawa na uwitaji wa soko la duniani yaani ikiwezekana baadhi ya course kubadilisha ufundishaji na kuangalia kwa sasa dunia inataka nini.
  • Kila university kuwe na research team ya kuangalia course zilizopo kama zinakidhi mahitaji ya soko na pale wanapogundua washauri chuo husika kufanya mabadiliko endelevu ambayo yatasaidia taifa kuwa na matokeo chanya.
  • Pia nashauri wizara ya elimu kuruhusu watu kusoma masomo wanayoyaka haijalishi alisoma nini elimu ya sekondari. Mfano mtu anaweza akawa amesoma EGM lakini alipomaliza secondary akatamani kwenda kusoma ufamasia kama ana uwezo aruhusiwe kusiwe na mipaka kwa kuwa hakusoma chemistry au biology hawezi kusoma ufamasia. Au mtu amesoma HGL anataka kusoma engineering aruhusiwe kufanya maana juhudi zake zitamsaidia kuelewa mambo mengi katika course husika. Wenzetu Ulaya mtu anaruhusiwa kusoma chochote anachotaka muhimu awe na juhudi na utayari na watu wanafanya vizuri. Sasa wizara isiwe kikwazo.
 
Upvote 2
Pia vyuo vya Tanzania wanaweza wakawa na walimu hao hao wenye GPA kubwa lakini wakaongeza tu kuwaarika watu wanaofanya kazi wanazozifundisha kufanya case study ambayo inaendelea kwenye soko la sasa.
Wakifanya hivi watabalansi shule kubwa na mambo ya mtaani.

Wote wana nafasi. Elimu ya nadharia na ya walio kwa ground/field. Tuking'angania sana wa mtaani ndio kila siku itakuwa kufundisha ujanjaujanja tu badala ya sayansi ya biashara.


Pia nashauri wizara ya elimu kuruhusu watu kusoma masomo wanayoyaka haijalishi alisoma nini elimu ya sekondari. Mfano mtu anaweza akawa amesoma EGM lakini alipomaliza secondary akatamani kwenda kusoma ufamasia kama ana uwezo aruhusiwe kusiwe na mipaka kwa kuwa hakusoma chemistry au biology hawezi kusoma ufamasia. Au mtu amesoma HGL anataka kusoma engineering aruhusiwe kufanya maana juhudi zake zitamsaidia kuelewa mambo mengi katika course husika.
Mmmmmmh!!! Hiii mazee sasa msingi atautoa wapi? Au ndiyo atasomaga yote hapohapo.
 
Tuking'angania
Hapa nilimaanisja MWALIMU wa nadharia afundishwe nadharia yake lakini atafute mtu ambaye Yuko kwa field aje aelezee Nini kinafanyika sokoni ili kuweza kuoanisha nadharia na VITENDO ili wanafunzi waweze kujua hii elimu wanayoisoma inafanyeje kazi mtaani. Lakini kujifunza nadharia bila VITENDO havimjengi mwanafunzi.
 
Wakifanya hivi watabalansi shule kubwa na mambo ya mtaani.

Wote wana nafasi. Elimu ya nadharia na ya walio kwa ground/field. Tuking'angania sana wa mtaani ndio kila siku itakuwa kufundisha ujanjaujanja tu badala ya sayansi ya biashara.



Mmmmmmh!!! Hiii mazee sasa msingi atautoa wapi? Au ndiyo atasomaga yote hapohapo.
Mimi naamini katika kujifunza mtu akiwa na Nia atasoma vitu vya ziada kwa sababu ana Nia na anaweza kufanya vizuri kupita yule mwenye msingi. Kuwa na utayari tu
ni msingi wenyewe.

Ninamjua mtu alisema HGM hakuwahi soma hesabu ngumu chuo akaja kusoma economics na alikuwa anakuwa wa kwanza darasani kuliko wale walisoma EGM au PCM au ECA ambao hesabu kwao zilikuwa ni kitu Cha kawaida. Kwa kuwa alikuwa na utayari aliweza kufanya vizuri nadhani akitoka na GPA ya 4.7 au 4.8
 
Back
Top Bottom