ladyreen7
New Member
- May 29, 2021
- 2
- 1
Elimu ya fedha, uhuru wa kiuchumi
Na Binti Msakuzi
Kwa kipindi kirefu mazungumzo kuhusiana na suala la fedha yamekuwa ni gumzo baina familia mbalimbali za kiafrika. Ukimya huo uliyotamalaki juu ya mazungumzo hayo yamesababisha maswali magumu kuhusu fedha kuendelea kubaki bila jawabu.
Ikiwa maswala mengine mbalimbali kama dini, elimu na afya yakipewa kipaumbele katika kutafuta mwenza, kujenga familia na kulea watoto, ufahamu wa fedha na uchumi binafsi umekuwa mada nzito kuzungumziwa katikati ya ngazi ya familia hata kitaifa.
Ukweli kuhusu hilo unathibitika kupitia Aziza Kiana mwenye umri wa miaka 23, mhitimu wa shahada ya uchumi katika chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Maswali hayo yaliendelea kumuumiza kichwa baada ya kushindwa kuelewa mienendo i ya kiuchumi na usimamizi wa fedha ndani ya familia yake.
“Nimekuwa nikishuhudia jinsi gani baba yangu anavyojituma na kufanya kazi kwa bidii. Alijikita katika biashara ya urandaji thamani za ndani na maofisini. Alikuwa akijituma kwa bidii kubwa lakini sehemu kubwa ya kile alichokipata ilitumika zaidi kunisomesha mimi. Kadiri muda ulivyoenda mafanikio yake yalikuwa yakipungua badala ya kuongezeka.” Alisema.
Aziza alieleza namna biashara ya baba yake ilivyopata mtikisiko wa kiuchumi mnamo mwaka 2016 akiendelea kusukuma biashara hiyo kusimama imara. Pigo la UVIKO 19 nalo liliendelea kurudisha jitihada zake za kiuchumi nyuma.
“Licha ya mafaniko aliyoyapata katika kipindi cha nyuma mwaka 2010 hadi kuweza kupata faida ya kufikia thamani ya dola za kimarekani miasaba na kwenda China kununua gari ya kubeba mizigo kwa ajili ya uchumi. Alipitia changamoto ambazo kwa kipindi hizo zilikuwa kizingiti kwa biashara nyingi kukuwa nchini hasa UVIKO 19. Kilichonistaajabisha ni kwamba kuna baadhi ya watu waliweza kujizolea faida kede katika uwekezaji wao kipindi hicho ambacho wengi walifilisika.” Alieleza.
Hapo ndipo safari ya kutafuta uhuru wa kifedha ilipoanza kwa Aziza. Alianza kutafuta maarifa tofauti kuhusu fedha, jambo liliomhamasisha kusoma uchumi katika ngazi ya chuo kikuu. Kwa kupitia kusoma vitabu mbalimbali kama vile Rich dad Poor Dad, Richest Man in Babylon pamoja na 8 new rule of money alipata maarifa ya namna ya kutengeneza, kutunza na kuendelea kuzalisha fedha na kugundua makosa kadhaa ambayo yamekuwa yakifanywa na watu wengi kama tabia ya kila siku.
“Watu wengi tumekuwa tukijivunia umiliki mali kama nyumba, viwanja na mashamba kama sehemu ya ufahari pekee wa vile tulivyovimiliki. Baba angu aananyumba takribani nne, lakini hakuna hata nyumba moja inayomuingizia kipato. Niliwahi mwambia rafiki yangu mmoja kwamba baba yangu anamiliki nyumba nne, aliniuliza hizo nyumba nne zote zimemuingizia kipato gani¬¬, nilishtuka kwa ukweli ule ambao ulikuwa ni mgumu kukabiliana nao.”
Jua lilikuwa limeshazama kurekebisha makosa yaliyofanywa na baba yake katika kurekebisha uchumi wake, lakini ilikuwa ni mwanzo mpya wa kuwakomboa wengine kuangukia katika shimo hilo. Aziza aliendelea kutafuta maarifa juu ya uzalishaji na usimamizi sahihi wa fedha na kuazimia kutoa maarifa hayo kwa watu wengine kuweza kujifunza zaidi.
“Kwa sasa hakuna kitu ninachoweza kufanya kurejeresha faida na thamani ya biashara ya baba yangu kusimama tena, lakini kupitia kosa hilo nimejidhatiti kuwafundisha watu wengine kuhusu elimu sahihi ya fedha. Kupitia mitandao yangu ya kijamii ya instagram kwa jina la misszayn pamoja na Linkedin kama Aziza Kiana ninaweka maudhui mbalimbali kuhusu elimu ya fedha ikiwa imewalenga zaidi vijana kujikita katika uwekezaji.” Alisema Aziza.
Hii ni sura moja kati ya nyingi nchini inayoathirika kutokana na ukosefu wa elimu ya uchumi. Mtaala wa elimu ya msingi haujaelekeza katika kuwaelimisha watanzania namna ya kuweka akiba ya fedha, kuwekeza na kuongeza thamani ya pesa katika mapato na matumizi ya kila siku.
Halikadhalika umuhimu wa nidhamu ya fedha umetajwa kuwa nguzo muhimu katika safari ya mafanikio ya mtu binafsi. Ni muhimu kuweza kusimamia fedha binafsi ndipo mtu aweze kusimamia fedha ya taasisi, jamii na umma kwa ujumla. Hayo yalibainishwa wazi na Mkurugenzi wa SSC Capital Salum Awadhi.
‘’ Ni muhimu sana kama kijana kuwa na uwelewa wa maswala ya fedha wakati bado una nafasi ya kufanya maamuzi makubwa ukiwa chuo kikuu. Tanzania nzima kuna takribani benki 56 zenye thamani ya uwekezaji unaofikia Tr. 26 lakini ni watu elfu kumi na saba pekee walioajiriwa. Jumla ya vijana milioni moja wanahitimu na kuingia katika soko la ajira kila mwaka. Ajira zilizopo ni chache kwa wote hao kuajiriwa, kiuhalisia sio wote mtakaomaliza mtaajiriwa.’’ Alisema.
Salum alisema kuna hatua kuu saba za kumuwezesha kijana kufikia uhuru wa kiuchumi ambazo ni kuwa na vyanzo mbadala vya mapato, kuzingatia matumizi kwa kufuata kanuni za fedha, uwekezaji, ufahamu juu ya kodi, mpango wa kustaafu na kuweka akiba.
‘’ Vijana wengi mnaamini kuwa uwekezaji ni mpaka uwe na mtaji mkubwa, lakini niwatoe shaka juu ya hilo ya kwamba sio kweli kwa sababu unaweza kuangalia uwekezaji ambao hautakinzana na ratiba yako ya masomo kama vile uwekezaji wa hisa katika makampuni mbalimbali na faida yako ikiendelea kuzalishwa. ‘’ Aliongeza Salum.
Aliweka mkazo juu ya swala la uwekezaji akisema kuwa mjasiriamali ni mtu anaenagalia fursa zilizotokana na changamoto mbalimbali za maisha. Ni muhimu kuangalia fursa katika eneo ambalo unalipenda na umebobea haswa.
‘’ Fikiria tatizo, angalia namna unavtoweza kupata ufumbuzi wa hilo tatizo, hiyo ndio maana ya fursa. Tafuta uzoefu katika eneo unalotaka kubobea ili kupata umahiri, tafuta timu yako ya mapambano maana huwezi kufanikiwa ukiwa peke yako. Watu unaowachagua kuambatana nao katika safari ya mafanikio wanamchango mkubwa katika kukusogeza pale unapotaka kufika.’’ Alisisitiza Salum.
Aziza alieleza matamanio yake ya kufikisha maudhui hayo kwa watu wengi zaidi kuweza kijifunza na kuchukua hatua madhubuti wakati bado wana nafasi ya kufanya mabadiliko. Anaamini kwamba kwa kupitia wadau mbalimbali wa fedha na uchumi kumuunga mkono kufanikisha kipindi hicho kuruka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Anaamini kwamba kupitia elimu sahihi ya uzalishaji na usimamizi madhubuti ya fedha kwa mtu binafsi ni hatua ya kwanza kuweza kufanikisha uchumi wa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Maarifa hayo sahihi yataenda kufungua mijadala na mazungumzo kwa ngazi ya familia kuwa huru kutafuta ukweli na uelewa juu ya fedha.

Upvote
1