Elimu ya Historia Ni elimu muhimu sana kwetu

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
540
Reaction score
507
ELIMU YA HISTORIA: Ni elimu muhimu sana kwetu Bindamu.


Hapa nina lengo moja tu, nalo ni elimu ya Historia na umuhimu wake kwa sisi binadamu. Hapa simaanishi kuwa kila mmoja asome somo la Historia mpaka chuo Kikuu la hasha!!. Nataka kuonyesha kwa ufupi umuhimu wa sisi binadamu kujielimisha na kujua mambo ya kihistoria.


Historia ni mafunzo yanayohusu maendeleo ya mwanadamu. Ni kupitia elimu ya historia sisi tunajua ni kwa jinsi gani mwanadamu aliweza kutawala mazingira yake,akili na uwezo wa kupambanua mambo kulingana na changamoto zilivyojitokeza. Kwa hiyo naweza kusema,elimu ya Historia ni Mama na Baba wa mambo karibu yote Duniani.


Elimu ya Historia ni elimu inayoelezea mambo ya msingi kabisa kwetu binadamu na ni lazima tuyafahamu kinaga ubaga. Kupitia elimu ya Historia tunaelewa kwa undani kabisa maswali kama;
a) Ni nani walikuwepo?
b) Sehemu gani? Na muda gani?
c) Walikutana na changamoto gani na walizitatua vipi?
d) Je njia walizotumia zilikuwa sahihi kutokana na muda ule?


Elimu ya Historia ni elimu inayotoa picha nzuri kuanzia kizazi kilichopita, cha sasa na kizazi kijacho. Mfano,vizazi vilivyopita vilikabilianaje na mambo ya kipuuzi tunayoyashadadia leo kama rushwa,ushoga,ubinafsi wa hali ya juu, lazima utakuta kuwa walipambana na hawakutaka kabisa mambo ya kipuuzi kama haya, na kizazi kilichopo basi mnayakataa wazi wazi. Vilevile,mnaweza kujifunza kuwa hawa watu walifanya hivi lakini kwa sasa tunatakiwa tuenende katika njia hii kutokana na mazingira yetu ya sasa hivi.


Elimu ya Historia ni elimu peke yake inayoweza kumfanya mtu awe mwanazuoni kweli kweli. Ni elimu pia inayowafanya watu kuwa wazalendo na wenye kudhamini Taifa lao. Elimu hii itatufanya tujue na kujiuliza mambo ya misingi kabisa, kama Taifa hili lipo kwa sababu kuna kizazi kilipigana ili kulinda heshima na utu wa mwanadamu. Mwanazuoni na Mwanahistoria maarufu Prof. Mazrui aliwahi kunena;


"Naam,hebu nirejee yale niliyowahi kusema-tunajifunza historia ili tujielewe. Lakini pia inatubidi tuisome ili tuwe na busara zaidi,ubinadamu zaidi,ili tuupunguze ujinga,na hakika tuupunguze ukatili,na mara nyingi kwa kuangalia mustakabali wetu".


Nitawapeni mifano kuntu hapa kidogo. Unaweza ukaiona midogo lakini ni ya maana sana katika elimu ya Historia na maisha ya mwanadamu kwa ujumla.


Moja,ebu uumwe na uende kituo chochote kinachotoa huduma ya afya,na ufike daktari ukupime na kutaka kukuchoma sindano au kukupa dawa ya kunywa,nini unajua kitatokea.Lazima uhoji uhalali wa kukupima na kuanza kukutibu bila ya kuhoji Historia ya ugonjwa wako!!.maana atakupta dawa ambazo zinaweza hata kukuzuru vibaya sana.


Pili, kwa mfano, huwezi kutatua tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa bila kujua chanzo chake,ukifanya hivi ni ngumu kutatua changamoto hii.


Kwangu Mimi,elimu ya Historia ni elimu inayowakuza vijana wetu kuwa WAZALENDO katika Taifa letu na jamii zetu kwa ujumla na hata Bara letu la Afrika. Na ni elimu kupitia elimu hii,tunaelewa kwa undani kabisa dhambi upumbavu wa binadamu na kujifunza kutofanya tena. Mfano, elimu ya Historia inawafanya binadamu wasiwe wabaguzi au wasiwabague watu kutokana na dini zao,rangi zao,maeneo wanakotoka.


Ni elimu inayosisitiza haki,utu,na ustashi wa jamii zetu kwa ujumla. Elimu hii inakufanya uchukie dhuruma bila kujali nani ameifanya,uchukie rushwa kutoka moyoni mwako.


Na kusema kweli elimu ya Historia lazima tuikumbatie maana inajenga watoto wetu,vijana wetu,watu wazima,ili waendelee kujua na kukumbuka umuhimu wa mambo yafuatayo;
a) Historia tujifunze uridhi wetu na faida zake zote
b) Kuwa na moyo wa upendo kwa watu wote hapa duniani,
c) Linatufanya tuwe na uwezo dhabiti wa kufikiri katika masula mbalimbali
d) Ni elimu inayoamusha hisia za kimaendeleo
e) Elimu inayotufundisha kuwa WAZALENDO wa kweli.
f) Tunajifunza jinsi ya kuheshimu MIIKO ya. Taifa letu,
g) Kuwakumbuka, kuwaenzi, na kuwaheshimu watu wote waliofia wakilinda heshima na utu wa mwanadamu katika Taifa letu,
h) Elimu inayoonyesha wapi tulikotoka,tuko wapi,na tunaelekea wapi,
i) Elimu inayotufanya tuwe viongozi imara na tusioteteleka kiurahisi.


Hitimisho


Tusipojua tunakotoka hakika hatuwezi kujua tulipo sasa na tunakoelekea kama Taifa. Kwa hiyo elimu ya Historia ni elimu ya msingi na muhimu sana katika ujenzi wa Taifa letu na Bara letu la Afrika.
 
Weka utofauti kati ya elimu ya historia na somo la historia ili hoja iwe na mashiko na mimi niunge mkono hoja

.made in mby city.
 
Elimu ya Historia namaanisha kujifunza au kujielimisha mwenyewe bila hata kwenda darasani kuhusu mambo ya kale ili yaweze kukusaidia katika wakati wa sasa na ujao.

Nimetumia Elimu ya Historia na siyo Somo la Historia kwa sababu somo la Historia mara nyingi linaendana au linahusishwa na kujifunza darasani na si kujielimisha wewe mwenyewe. Mfano,unaweza kuwa Injinia na ukagombea ubunge au URAISI,pale lazima ujielimishe mwenyewe, jamii yako imetoka wapi,iko wapi na inaenda wapi na hii ndiyo elimu ya Historia ninayomamaanisha.
 

"Education is not the learning of the facts but it is the training of the mind to think"

Naunga mkono hoja

.made in mby city.
 
upo sahihi mkuu, historia ndio mama wa taaluma zote, kila taaluma iwe ni sanaa, sayansi au biashara ndani yake imebebwa na historia
 
naunga mkono hoja ya mtoa mada. nimekuwa nikijiuliza hawa wenzetu waliobobea masuala ya historia wanakuwa wapi kusaidia kufafanua masuala kadhaa ya yanayoibuka katika uhai wa taifa hili - tunashuhudia ukimya. vyuo vikuu vinatusaidia vipi katika hili.

kwa vyuo vikuu sio historia tu - hata masuala ya uchumi - absolute silence ndo tunaishuhudia.

isipokuwa tungehitaji pure history sio ile iliyochanganyika na siasa ambayo nayo ina sehemu yake.

huwa najiuliza sana nikisoma vitabu vya modern history za europe na britain - ya kwetu tanzania iwapi? huenda from my sheer ignorance!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…