Elimu ya Josephat Gwajima inatia mashaka

Sifa za kuwa mbunge ya chini awe darasa la Saba ndio maana Tunduma mgombea ubunge wa Chadema Tunduma ambaye pia alikuwa mbunge wa chadema Jimbo Hilo ni darasa la Saba pure anaitwa Mwakanjoka
bila kumsahau yule mbunge wa CCM👹👹👾wa kandaile yakupenda madem weupe anaitwa MSUKUMA cjui yule hata ilo dalasa7 kwake nindoto
 
Sifa za kuwa mbunge ya chini awe darasa la Saba ndio maana Tunduma mgombea ubunge wa Chadema Tunduma ambaye pia alikuwa mbunge wa chadema Jimbo Hilo ni darasa la Saba pure anaitwa Mwakanjoka
Hahaha hivi uki fail form six ukapata zero unakuwa na elimu gani?! A-level au O-level?!

Gwajima O-level ali fail alipata daraja la nne lililo egemea zero, leo ana PhD.
CCM akili zenu mnazijua wenyewe.

Eti kasema anajua kaongea kijapani na kaandika vitabu vya kijapani, mara katuambia anatuletea Ambulance, !!!

Kampeni za hivyo angeenda Koromije.
Kawe Ambulance za nini tuna magari yetu, halafu sisi sio wagonjwa, au anagombea uganga wa zahanati?!
 
Japo umejitahidi kutaka kueleza kitu lakini ukweli ni kuwa umepotoka kabisa.

Shule za dini zina uwezo wa kutengeneza syllabus zao lakini unapofika kwenye Universities, haijalishi chuo hicho kinamilikiwa na dini au Serikali, ili kuweza kutambulika na kukubaliwa, katika kila nchi kuna board ya kuweka vigezo vya kukifanya chuo kutoa degree inayotambulika, na hizi board hufuata miongozi ya kimataifa ya elimu. Bodi hizi ndiyo hutoa ulinganifu wa credits za viwango vya elimu kwa mataifa mbalimbali.

Vyuo vikuu, bila ya kujali kama ni cha dini, serikali au taasisi binafsi, huwa ni taasisi huru ya kimasomo. Ndiyo maana leo hii ukitaka kwenda kusoma degree ya theology au divinity Kent University, UK, unapokelewa kwa kuangalia kiwango chako cha elimu na siyo dini yako. Hata kama huna dini yoyote utapokelewa kama kiwango chako cha elimu kimefikia entry qualifications.

Kwa kuangalia hiyo elimu ya Gwajima, kwa kweli huo ni utapeli mkubwa wa elimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sifa za kuwa mbunge ya chini awe darasa la Saba ndio maana Tunduma mgombea ubunge wa Chadema Tunduma ambaye pia alikuwa mbunge wa chadema Jimbo Hilo ni darasa la Saba pure anaitwa Mwakanjoka
Hujaelewa hata kianachojadiliwa. Tuliza akili, uelewe hoja iliyopo badala kukurupuka kuandika kabla hata ya kuelewa hoja ni nini.

Tatizo la Gwajima siyo kiwango cha Elimu bali uwongo katika utoaji wa taarifa ya elimu yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Asante kwa kutoa hilo darasa. Nilishindwa mjibu huyu mtu sababu niliona ana uelewa duni kwenye mambo haya. Kuhusu Gwajima, mimi nilikuwa napata shida sana kwani elimu yake na matamshi yake niliona haviendani. Nilidhani ni msomi. Sasa, nimejua ukweli hivyo nimekuwa huru na simlaumu tena atakapo sema lolote.
Nimebaki na shida moja tu, nayo ni elimu ya Jiwe. Uelewa wake hauendani na elimu yake.
 
Hii elimu ya Gwajima ni utapeli mkubwa. Sasa nimeelewa kwa nini amekuwa mtu wa kuropoka ovyo ovyo. Mara anafufua misukule, mara nitanunua treni, mara nitawapeleka wakazi wote wa Jimbo la Kawe Marekani - haya siyo maneno yanayoweza kutamkwa na mtu aliyeelimika au hata mwenye akili timamu yeyote, bila ya kujali huyo mtu ana elimu gani.

Ameshindwa kuwapeleka waaumini wake Marekani, halafu eti atawapeleka wajazi wote Marekani. Unawapeleka Marekani kufanya nini! Eti ana rafiki ambaye ni gavana, na anataka wabadilishane watu. Huyu ni mzima kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachojadiliwa siyo haki ya kikatiba, ni uongo na sifa za bandia. Kumbuka mambo hayo yanaweza kuwa ni mwongozo wa tabia yake. Mbona Musukuma anajitambulisha kwa class 7 yake?
 
Sifa za kuwa mbunge ya chini awe darasa la Saba ndio maana Tunduma mgombea ubunge wa Chadema Tunduma ambaye pia alikuwa mbunge wa chadema Jimbo Hilo ni darasa la Saba pure anaitwa Mwakanjoka

wewe mbunge darasa la saba ni CCM (msukuma )
 
Tulieni octoba 28 kitaeleweka,mtafutueni kazi mbadala huyu mgombea wenu mdee
 
Duh....!

Kawe wote mna magari?!
 
pia kupeleka watu marekani
Mkuu hakusema atapeleka watu tu marekani; amesema atapeleka watu "wote" wa Kawe marekani, na atabadilishana na wale watu wa kule marekani ili wao waje Kawe...Kawe yote itakuwa ni miondoko ya watsap niiiga yoyo yoyo, yu no waram seeeing
 
Lawama ziko kwa CCM na maamuzi yao. Walishindwa kuelewa maana ya nafasi ya ubunge. Gwajima alistahili kuangaliwa kwa ubora wake na hata waumini wake. Ubora wake uko chini na hata waumini wake ni wa aina hiyo hiyo! Hili ni tatizo kwa vyma vyote lakini kwa CCM ni kubwa kutokana na ukongwe wao. Ndo maana Bunge linageuka kuwa ni kikao cha watu wabovu na rais anaamua kujipangia matumizi yeye mwenyewe.

Ni kweli haikuwa ajabu mtu anayejiita askofu kujipiga picha akifanya ngono? Bila kujali sababu ya kitendo hicho, hakutakiwa hata kusikilizwa kwenye kura za maoni. Ni mtu mchafu tu! Tamaa ya CCM ni ile ile; kuwa na wabunge wengi bila kujali ubora wao.
 
Mwamposa alipewa PhD baada ya kuua watu kule Moshi ndio hiyo hiyo ya akina gwaji.
 
Kamanda haya ya elimu yake yatatusadia tukomboe jimbo letu? Tuwe na hoja za msingi hali mbaya sana kisiasa tunayo.
 
"...Separation ya dini na serikali..." na sasa mtu huyo huyo anaingia serikalini huku akiwa bado kiongozi kwenye mambo ya kidini.
Usisahau kuteuliwa kugombea ubunge, kigezo kikubwa ni kujua kusoma na kuandika tu... huko mbele kama mtu ana elimu ya majini, katekisimu etc kwao si ishu... cha kuniuliza, JE! ANAJUA KUSOMA NA KUANDIKA..!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…