The Grace
New Member
- Oct 15, 2020
- 1
- 1
Ukweli uko wazi sasa na sio swala la siri tena. Maisha yetu yanategemea asilimia 30 akili ya darasani na asilimia 70 juhudi zetu na akili zetu za kuzaliwa. Nikiwa kama mwanafunzi wa elimu ya juu kuna mambo nimekuja kujifunza japo kwa kuchelewa ila nina imani ilikua wakati sahihi. Nikiwa kama mwanafunzi wa kike, niliamini chuo ni sehemu ya kujionesha zaidi (sio kifursa) yani kuishi yale maisha ya kujitanua. Lakini haikua hivyo na baada ya kupoteza mwaka mmoja chuo, nlipoteza kwa sababu sikuenda kufanya kile nilichopaswa kufanya. Lakini yafuatayo ni mambo ambayo ninawiwa kuyasema kwa manufaa ya mtu mwingine ambae hii inaweza kuwa msaada kwake.
Ukiwa chuo kwanza jaribu kukubali hali ya ulikotoka. Hii itakusaidia sana kuacha kutafuta 'focus' kwenye mambo mengine na badala yale utakua na mambo machache huku jambo kuu likiwa kupata maarifa mapya.
Jichanganye na watu halafu epuka kuwa na marafiki wengi wasio na faida. Kujichanganya na watu sio mpaka awe rafiki yako, hapana, hii kwa neno la lugha ya kiingereza tuiite 'connecting'. Sasa unapojichanganya na watu mbali mbali lengo kuu ni kupata 'new knowledge, experience and skills', hizi zitadaidia kujifunza kutoka kwa wengine na kupata maoni ya wengine juu ya unachosomea, mipango yako ya baadae n.k. Epuka kutaka kuwa rafiki wa kila mtu au kila mtu awe rafiki yako kuna mambo yatakua sio ya lazima kwako ambayo utajikuta unaanza kuya - adapt.
Jifunze kuwa na nidhamu ya pesa kuanzia chuo. Nidhamu ya pesa ni kukubali kutumia pesa kwa uchache kwa wakati huu ili kuleta faida kubwa ya baadae. Sio lazima utoke kila weekend, sio lazima utumie simu mpya kila mwaka na wala sio lazima uwe mtu wa fasheni mpya kila mwezi. Upatacho (kikubwa au kidogo) anza kujifunza kuhifadhi kwa ajili ya baadae. Ule msemo wa maisha yenyewe mafupi... utakuponza ukijikuta umebarikiwa kuishi maisha marefu na hukuyatendea haki kwa wakati sahihi.
Hudhuria matukio na semina mbalimbali zinazoandaliwa chuoni au hata na mashirika mengine kwa lengo la kujifunza zaidi nje ya darasa. Huko utakutana na watu pamoja na fursa mbalimbali watakao/zitakazo kujenga kwa namna fulani.
Soma kwa bidii, shiriki kazi za makundi na mijadala ya darasani. Kama ni mtu wa michezo, onyesha kipaji chako pia maana huwezi jua njia ya kutokea ni ipi.
Kubwa kabisa, usisahau imani yako. Shiriki ibada na utii yale ambayo imani yako inahubiri. Hii itakuongoza kwa hatua zote upitiazo na hata kukupa nguvu pale ambapo mambo utakapoona yanakua hayaendi.
Ajira ni ngumu sana sio serikalini wala kwa watu binafsi. Elimu pekee haitoshi kumshawishi mwajiri haswa kwenye sekta binafsi. Ukipata sehemu ya kujifunzia kwa vitendo wakati bado uko chuoni ni vyema kushiriki ili kujiongezea 'experience' na ujuzi.
Nina amini kwa hizi dondoo fupi kuna kijana au binti ataweza kubadilisha mtazamo wa maisha akiwapo chuoni.

Upvote
1