Shahaa
New Member
- Jul 19, 2022
- 2
- 2
Na Shafii Hamisi Athumani
Safari ya elimu imekuwa ikianza kwa matumaini makubwa ya mwanafunzi kuanza shule kwa furaha na kuhitaji kufikia malengo makubwa hapo baadae akiungwa mkono na kila mtu kwenye jamii na taifa lake haswa familia kwa hali na mali inakuwa ni tegemeo kubwa, hii inatoa hamasa kwa mwanafunzi kusoma kwa bidii sana kutimiza si tu malengo yake bali ni ya familia, jamii yake na taifa kwa ujumla.
Familia inapambania kusomesha mtoto kwa hali na mali, inafika kipindi kila kitu wanauza kufanikisha kumpeleka mtoto shule, inafika mahali hakuna kilichobaki nyumbani hali inayopelekea majonzi baada ya kuhitimu kwa maan anageuka mzigo na kukutana na kashfa nyingi kumaliza mali bila mafanikio yeyote, hali hii inaumiza sana.
Hatimae anafaulu vzuri katika elimu ya msingi na secondary katika hali kujiamini kukiwa na upendo kwake na familia yake,
Changamoto inaanzia pale panapokuwa na mitazamo hasi kwa wasomi wa leo kutoka kwa jamii zao kulingana na dhana ya pesa mbele kuliko kusoma mpaka elimu ya juu, hii inatokana na kupungua kwa ajira na kipato cha wahitimu kinakuwa kidogo kulinganisha na baadhi ya wasioenda shule katika muda ambao mhitimu anaanza maisha upya huku akipokea kashfa mbalimbali kutoka kwenye familia yake na jamii kwa ujumla akionekana ni mzigo mkubwa ilihali hana kosa lolote!
Mitazamo hii inafanya wahitimu kuwa na msomgo wa mawazo kuweza kufuta dhana hizi potofu kuonekana sio kitu mbele ya jamii kwakuwa wana maarifa ya kutosha , inashusha pia hali ya ufaulu na inakatisha tamaa hasa pale anbapo serikali inatoa ajira kwa idadi ndogo kulingana na wahitimu waliopo mtaani , elimu inakuwa majonzi kwa hali ya hii , wahitimu hawana mitaji, wamekuwa watu wazima wanaonekana mizigo na wametoka katika familia za hali ya chini, fursa ni ngumu.
Utatuzi unaweza kufanyika kwa vijana hawa wahitimu kutojutia elimu yao basi kwa mambo kadhaa yafuatayo:
¡》Fursa mbalimbali zitolewe kwa kuwapa vipaumbele wahitimu, ikitokea fursa basi wapewe wahitimu kwenye kada tofauti tofauti ili kujikwamua na kujipatia kipato. Mfano uwepo wa sensa mwaka huu wahitimu wanapaswa kuwa mbele katika kuhesabu watu.
¡¡》Serikali izidi kutoa ajira ili kuweka umuhimu wa kupata maarifa kwa wahitimu kuepukana na dhana za kukatisha tamaa, unakuta familia imeuza kila kitu kusomesha mtoto anarudi amehitimu anakuwa mzigo tena!
¡¡¡》Mwisho kabisa, wahitimu wasiwe watu wa kujutia na kukata tamaa, wamtegemee mungu na ipo siku basi watafanikiwa na kuonesha thamani ya elimu yao walioipata na kubadili mitazamo ya watu mbali mbali kwenye jamii.
Karibuni kwa mijadala