SoC01 Elimu ya juu na Umasikini

SoC01 Elimu ya juu na Umasikini

Stories of Change - 2021 Competition

Mswahili mahiri

New Member
Joined
Jul 31, 2021
Posts
1
Reaction score
6
Habari wanajukwaa leo nitazungumzia suala la Elimu ya juu na umasikini hasa kwa vijana.

Tunaelewa kua elimu ilipewa maana mbalimbali wwngine wakijaribu kusema kua elimu ni mwanga, Elimu ni ufunguo wa maisha na wengine wamefika mnali na kusema elimu ni kichocheo cha maendeleo.

Nimevutiwa kuandika andiko hili nikiwa ni moja ya vijana wengi wa kitanzania ambao nimepata elimu kwa ngazi ya shahada lakini kwa bahati mbaya nimekua muhanga wa tatizo la ukosefu wa ajira.

Kutokana na ukosefu wa ajira taaluma tulizo zipata vijana wengi zinaishia kuozea katika makabati na kushindwa kujua tufanue nini.
Zipo dhana mbali mbali kwamba vijana wengi walio bahatika kupata elimu na kukosa ajira wanaishia kua masikini na ombaomba kutokana na uvivu,uoga,kutokujitambua, kutokujituma na kutokuzitumia taaluma zao vizuri.

Kwa upande mmoja au nyingine hoja hizo zinaweza kua za kweli au zinaweza kukosa mashiko kutokana na uhalisia wenyewe ulivo.

Suala kubwa la kujiuliza ni kua;

1) mifumo yetu ya elimu imejengwa katika nadhalia ya kumiwezesha muhitimu kijitegemea!?

2) mifumo yetu kifedha inaweza kuwatambua wasomi hawa na kuwakopesha mitaji!?

3)Je mifumo yetu ya kisiasa inawajenga vijana hawa kulitumikia taifa vyema na sio vijana kutumika ovyo hovyo!?

4)Je taaluma zinazotolewa katika vyuo zinaweza kutumika na kijana bila usimamizi,au mtaji mkubwa.

Kimsingi maswali ya kujiuliza ni mengi sana naengi ya maswali haya mala nyingi hujibiwa na watu walioko kwenye mamlaka husika kisiasa au kiitikadi mfano mzuri ni kua kuna baadhi ya wanasiasa wamewahi kusema "selikalini hakuna ajira nanvijana wajiajiri" sasa Swali la kujiuliza mwanasiasa huyu yeye yuko selikalini na amekaa kwa zaidi ya miaka 40 akifanya kazi na kulipwa kodi za walalahoi baba za hawa watoto wanaolia kukosa ajira anakuja na dhihaka kua vijana waache uzembe,uvivu na kujiajiri.

Ninachokiamini wimbi la vijana kukosa ajira linatokana na mfumo mbovu wa kisekta,na kimikakati kama selikali na wadau mbali mbali wangeweka mikakati imara ajira lisingekua suala la kupiga kelele katika kipindi hiki.

Kwani mikakati hiyo ingeanzia katika

1)kuboresha mitaala ya elimu itolewayo iendane na uhitaji wa sasa

2)kuboresha miundombinu ya kiuchumi mfano mikopo isiyo nanmasharti magumu na hata mikopo inayo himilika

3)kuweka masharti himilivu kwa wawekezaji ili waweze kuwekeza kwa wingi na kutoa fulsa za ajira kwa vijana.

4)Kupunguza kodi na masharti magumu kwa vijana wanaojiajiri mfano ni wengi walijiajiri katika sekta ya tehama hasa kufungua blogs,youtube channels, na platform zingine lakini wameshindwa kuendelea kutokana na masharti magumu yaliyo wekwa na mamlaka zilizopo kwa kisingizio cha kukusanya mapato.

5)lakini poa selikali na wadau wengine waone namna ya kuijenga jamii inayoweza kuendana na wakati uliopo ikiwa ni pamoja na kunufaika nanrasilimalil zinazo patikana katika maeneo yao husika.

Hayo ni baadhi ya maoni yangu kuhusu namna tunaweza kuliondoa tatizo la vinana wasomi wengi kubakia kua maskini

Lakini vijana wengi walitaman kuona walau hata selikali na wadau wengine wanashirikiana kutoa mikopo.hapa kwenye mikopo nieleze wazi kwasababu vijana wengi hatuna ardhi tunazo miliki wala hatuna vitu au mali zisizo hamishika kitu pekee tunachokua tunamiliki baada ya kutoka chuo ni cheti.

Katika hili ningependekeza mikop itolewe pia kwa vijana kama mimi tusio na mali lakini tunavyeti na tunaweza rudisha mkopo huo

Ahsanteni kwa kusoma Ahsante
#Naomba_Muipigie_Kura hii
 
Upvote 1
Back
Top Bottom