Elimu ya kidato cha sita inatusaidia nini watanzania

Elimu ya kidato cha sita inatusaidia nini watanzania

Mwambetania

New Member
Joined
Apr 8, 2011
Posts
2
Reaction score
0
Ninavyo itazama elimu hii ninaona kama inamaliza kipato cha Watanzania {wazazi na walezi} na pia inawapotezea muda vijana wa kitanzania [Wanafunzi].
Kwa nini naiona hivyo?
Elimu hii imeshindwa kuwaanda wanafunzi kuweza kuitumia katika jamii inayowazunguka (unapplicable), na hivyo kuwaacha vijana hawa kuwa tegemezi na kuzidi kuiongezea jamii mzigo mzito wa kuwalea vijana hawa. Tukizingatia umri wa wengi wao ni zaidi ya miaka 18, umri ambao nchi inasema ni umri wa nguvu kazi ya taifa.
Nini kifanyike?
Ili kupunguza huu mzigo kwa jamii, ni vizuri tukafuta elimu ya kidato cha sita na kuazisha mtaala wa kusoma "diploma", kwani elimu ya "diploma" inaweza kuwaandaa vijana kuweza kuitumia elimu yao katika jamii. Na hivyo kupunguza mzigo huu mkubwa kwa jamii.
 
Back
Top Bottom