SoC04 Elimu ya kidijitali na nafasi ya vijana katika Tanzania tuitakayo

SoC04 Elimu ya kidijitali na nafasi ya vijana katika Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Apr 19, 2024
Posts
7
Reaction score
4
Utangulizi

Jamii ya watanzania tunaelekea katika mambo yanayobeba mustakali wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. kipindi cha mwaka 2024-2025 tutashiriki mambo makuu matatu ambayo yatabeba hatma zetu kama taifa kuanzia miaka 5 na kuendelea, yaani miaka25. Kwanza mchakato wa kupata dira ya maendeleo ya taifa, itakayotuongoza kufika Tanzania tunayoitaka 2025-2050, pili uchaguzi wa serikali za mitaa, October 2024 na uchaguzi mkuu mwakani 2025.

Vipo vipaumbele ambayo vitakavyotuvusha kuelekea nchi ya ahadi. Katika Karne ya 21 tumeshuhudia mabadiliko ya kiuchumi, na kiteknolojia Ambapo dunia imekuja na ubunifu wa akili bandia katika shughuli zilizokua zikifanywa na binadamu, na kuifanya kazi kwa ufanisi, hivyo ni budi kwa taifa letu kuweka kipaumbele hili katika dira yetu huku tukiakikisha ubunifu huu unazalisha nafasi za ajira nyingi. Hivyo ni mapinduzi ya kiteknolojia au matumizi ya dijitali iwe moja ya vipaumbele katika dira.

Ni ukweli usiopingika kwamba bila taifa lenye weledi wa teknolojia tutatupwa mbali na mataifa mengine na kubaki maskini tukitumikishwa. Ni budi taifa liweke mkazo kuelekea haya mapinduzi

a; kuwapa fursa diaspora (watanzania wanaoishi ughai buni)Kuwekeza viwanda vya kiteknolojia na kutengeneza mitambo saidizi kwenye shughuli za kiuchumi mfano kilimo, ujenzi sanaa, vifaa vya nyumbani,nk.

b; Kuwekeza katika masomo ya mtandaoni application nyingine zitakazotoa elimu ya kuwafaa vijana wengi wamekua watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii, wakitumia muda wao mwingi mtandaoni na ndio sababu vijana wengi kujifunza tamaduni zisizo na maadili. Hivyo uwepo wa mitandao ya mafunzo itawasaidia na kuwapa fursa ya ajira.

c; Kuwekeza kwa masoko mtandaoni kwa bidhaa mbalimbali, ili kuwapa fursa vijana ya kujiajiri kupitia mtandao ndani na nje ya nchi. Mfano soko la bidhaa za nyumbani, kwa kutumia app mteja atalipa na kupata mahitaji yake ya kila siku akiwa nyumbani kwake ( delivery) kwa ngazi ya mtaa

d; Kuwashika mikono wabunifu wa kiteknolojia kwa kuwapatia miundo mbinu endelevu kwa kuwapatia vifaa, elimu zaidi hasa kwa nchi zilizoendelea kiteknolojia ili kuboresha ubunifu wao katika matakwa ya kimataifa na kuitangaza Tanzania na kutumika katika maisha ya kawaida.

e; Serikali ifanye tafiti za kuzalisha ajira mpya zitakazopunguza kero ya ukosefu wa ajira, mfano kurasimisha Kuboresha huduma ya uzoaji taka sehemu za mjini kwa kutumia mashine za kidijitali katika uzoaji na uchakataji taka ili kutengeneza bidhaa nyingine. Kisha kuwapatia vijana.

f; Kutoa elimu ya mafunzo mafupi mtandaoni (short course) hasa elimu ya mtandao matumizi na njia za kuzuia udukuzi katika akaunti za watu.

g; Uwepo wa program zitakazozuia matumizi ya picha na video chafu, wizi wa mtandaoni, na madhara mengine yanayotokea kutokana na mtandao.

h; Serikali iweke bayana matumizi ya teknolojia yaani akili bandia kwa wananchi ili wanachi wapate kufahamu umuhimu wa AI na kuondoa sintofahamu katika utumiaji, mfano uwasilishaji wa mipango ya kimaendeleo na upokeaji wa mahitaji au kero kwa kidijitali.

I; Kuwekeza teknolojia kwa wanafunzi wa ngazi ya chini yaaani msingi ili kuwa na wataalamu bobezi na wabunifu wenye ujuzi watakaoenda sambamba na soko la kimataifa.

j; Kuwekeza elimu ya Uzalendo na uongozi kwa vijana kwa kuangalia mazingira ya tamaduni zetu ili kuandaa viongozi wazalendo mfano wale waliopigania uhuru wa kisiasa, kwani sasa tunapigania uhuru wa kiuchumi, kuishi bila kutegemea misaada kwa asilimia kubwa.

k; Kuandaa kozi au fani ya uandisi na teknolojia za ujenzi wa miundombinu kidijitali, mfano ujenzi wa madaraja makubwa, barabara.

L; Kuanzisha taasisi itakayovumbua bunifu za vijana walio pembezoni au vijijini na Kuwasaidia kuimarisha bunifu zao.

Hitimisho
Namaliza kwa kusema tusiyatazame mapinduzi ya kidijitali kama adui wa maslahi yetu, mfano kazi bali tuitumie kama kisaidizi ili kufanikisha utendaji wa ufanisi, la sivyo tutabaki nyuma tutawaliwe kiuchumi.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom