Chachata
JF-Expert Member
- Apr 29, 2011
- 201
- 134
Vijana waliohitimu darasa la sabu wamechaguliwa kuendelea na masomo ya sekodari, waliochaguliwa wamefurahi, wapo wale ambao hawakuchaguliwa, hao wamenuna, mioyo yao imesononeka. Tafakuri Je Ni kweli kwamba hao waliochanguliwa kuendelea na elimu ya kizungu (kikoloni) wapo kweye mkondo mzuri wa maisha kuliko wale ambao hawakuchaguliwa au wameepukana na elimu hiyo ya kikoloni? Mwalimu nyerere aliwahi kusema 'Elimu lazima imuwezeshe binadamu kupambana na mazingira yake. Kwa kuzingatia maana hiyo tunaamini kuwa walimu wa shule za misingi, sekondari vyuo na vyuo vikuu ndiyo watu wanaojihusisha na elimu katika maisha yao ya kila siku, hao ndiyo shina na chemichemi ya elimu. Hao tunategemea wawe kioo, wayamudu mazingira yao,wayatumie kubadili ulimwengu wao na wengine wafuate nyuma. Bahati mbaya walimu ambao ndiyo wadau wakuu wa elimu ndiyo kwanza wamechoka, wanadai mapunjo na nyongeza ya mishahara kila siku. Wameshindwa kuyamudu mazingira yao wanategemea vyeti (makalatasi waliyopewa) yawakomboe. Hata pale ambapo haiwakomboi wao wanaendelea kusisitiza elimu ndiyo msingi wa maisha. Msingi ambao kwao umeshindwa kufanya kazi, wamekuwa wakihubili na kufundisha mambo ya uongo ambayo kwao hayafanyi kazi. Kwa msingi huo ndiyo maana nashawishika kuwapongeza wale ambao wemefauru kuepuka elimu hii ya makarasi ya kikoloni ya uongo kwani ni imani yangu kuwa hao wataenda kujifunza mazingira ya kweli, watayamudu mazingira ya kweli, watapambana na elimu ya kweli na wataishi katika mazingira ya kweli ya Tanzania.Hao hawatategemea elimu ya vyeti wala karatasi. kwa moyo mweupe nawapongeza hao ambao wameepuka elimu ya kikoloni. VIVA WASHINDI WA KWELI, TAFAKURI