platyhelminthesis
Member
- Jun 5, 2019
- 43
- 61
Kilimo ni sayansi ya mifumo ya uzalishaji mimea, ufugaji wa wanyama , na uvuvi wa samaki. Mara nyingi kilimo cha mimea kinaenda sambamba na ufugaji wa wanyama, sababu kuna kutegemeana kati ya mimea na wanyama. Wanyama hutoa mbolea katika ukuaji wa mimea na mimea hua ni chakula cha wanyama.
Andiko langu linagusia uboreshwaji wa elimu ya kilimo kwa wananchi wa Tanzania ili iwe kwa vitendo zaidi na sio kubukua darasani au kua na elimu ya nadharia kwa wingi vichwani. Elimu bora ya vitendo itamfanya kila mtu atakayeipata atamani kujiajiri katika kilimo na kupunguza wimbi kubwa la ukosefu wa ajira mtaani.
Tumeshuhudia serikali ikitoa elimu ya shamba darasa maeneo kadhaa ila bado mfumo huo hauwanufaishi wananchi wengi.
Elimu bora ya vitendo iwe katika maeneo haya yafuatayo;
1. Elimu bora ya kilimo vitendo katika vyuo vya kilimo.
2. Elimu bora ya kilmo vitendo katika kambi za jeshi kwa vijana wanaojitolea kama JKT.
3. Elimu bora ya kilimo vitendo katika magereza ya wafungwa nchini.
4. Elimu bora ya kilimo vitendo kwenye maeneo mbalimbali nchini yenye ardhi kubwa isiyokaliwa na watu.
Sababu za kuanzishwa mfumo huu;
Kutokana na janga la wasomi na wasiokua wasomi kukosa ajira mtaaani na hii ni sababu ya kua wanakosa kuboreshewa fursa za kujua elimu vitendo ya kilimo na hivyo kuona ni ngumu sana kufanya kilimo.
Elimu bora ya kilimo vitendo itasaidia wananchi wa rika mbalimbali kufanya kilimo kwa bidii kwa maana fursa zitaonekanika kwa wingi na itainua wigo la pato kwa wananchi na nchi kw aujumla.
Nchi yetu imebarikiwa sana katika hali nzuri ya kua na rasilimali rafiki kwa kilimo mfano, ardhi yenye rutuba na vyanzo vingi vya maji. Rasilimali zote hizi zina msaada mkubwa katika sekta ya kilimo kwa ujumla.
Maeneo mengi nchini hayakaliwi na watu na ni mapori ambayo hayana msaada mkubwa kwa wananchi katika kuongeza vipato vyao na yangewezwa kutumika kwa kilimo.
Dhana za jamii mtaani
Jamii nyingi mtaani zinaamini kua kazi ya kilimo ni kazi dhalili ambayo anafanya mwananchi asiye na kipato na hivyo haipewi heshima kubwa kama kazi inayowezwa kuchukuliwa kama kitega uchumi cha kumfanya mwnanchi awe tajiri.
Uhalisia ni kua katika nchi yetu ya Tanzania jamii hufanya kilimo kwa ajili ya mahitaji ya chakula na kutatua shida ndogondogo na sio bihashara, Jamii nyingi inafanya kilimo dhalili cha kutegemea mvua na hivyo mapato hua ni kidogo wapatayo kuliko muda waliotumia kuwekeza.
Nini kifanyike kwa kila eneo la kufundisha kilimo vitendo?
1. Elimu bora ya kilimo vitendo katika vyuo vya kilimo
Vyuo vya kilimo nchini vinafundisha kilimo katika misingi ya nadharia kwa wingi kuliko vitendo. Andiko langu linagusia ukweli kwamaana nimesoma shahada ya sayansi ya chakula na teknolojia katika chuo cha kilimo cha SUA. Katika chuo hiki na vyuo vingi vya kilimo, hakuna mfumo wa kua na mashamba makubwa ambayo wanafunzi wangeingia kujifunza, toka mwaka wa kwanza mpaka mwaka wa mwisho wa masomo yao. Kimsingi mitihani ingepswa iwe shambani. Wanafunzi au kila darasa liwe na shamba kubwa ambapo mazoezi ya vitendo yanapaswa yafanyike ndan yake. Ni aibu kwa vyuo vya kilimo kuteemea ruzuku serikalini na badala yake ingetakiwa vyuo hvi ndo vitoe gawiwo la faida serikalini.
Vyuo vya kilimo mfano wake SUA ina kila aina ya fani kuanzia watafiti wa mbegu, wahandisi wa kilimo, wataalamu wa kilimo. Wahandisi wa umwagiliaji,wataalamu wa usindikaji wa mazao ya kilimo, wataalamu wa bihashara ya kilmo, wataalamu wa uvuvi n.k. Kupitia huu mfumo wa kua na fani zote hizi, chuo kingeweza kuomba mashamba makubwa na fungu kwa ajili ya kufungua viwanda vidogovidogo vingi na kuanza kuwatumia wanafunzi kujifunzia shambani elimu yao na kuzalisha mazao mengi ya kilimo na kusindika. Kadhalika kwa waliosomea biashara ya kilimo itakua rahis kwao kujifunza namana ya kusambaza bidhaa na kutaufuta masoko kwa urahisi.
Kupitia huu mfumo wasomi wengi watakua na uthubutu wa kuwekeza kwenye kilimo kwa urahisi na sio kusubiria ajira.
2. Elimu bora ya kilmo vitendo katika kambi za jeshi kwa vijana wanaojitolea kama JKT
Jeshi la kujenga Taifa JKT linalenga kijana wa kitanzania awe mzalendo kwa kujitolea na kulitumikia taifa lake katika uzalishaji mali ikiwemo kilimo pamoja na kujifunza ukakamavu. Vijana wengi wakitoka jeshini wanashindwa kujiajiri kwa mafunzo waliyopewa jeshini kwa sababu mafunzo yamejenga uzalishaji wa mazao ya kilimo tuu na sio kumpa elimu bora ya kilimo.
Elimu ya kilimo inatakiwa iwe kwa vitendo ila kuwepo pia na ufahamu wa kwanini unalima zao hilo katika sehemu usika kwa kuelezewa kiundani mazingira ya eneo husika yanavyoweza kuathiri kilimo. Kijana lazima awe mwelewa na apate ujuzi wa kilimo na sio kutumia nguvu kazi yake tu.
3. Elimu bora ya kilimo vitendo katika magereza ya wafungwa nchini
Magereza ya nchini Tanzania yana mashamba makubwa ambayo hutumika na wafungwa kwa kuzalisha mazao ya kilimo. Hili ni jambo zuri kwamaana inawafundisha wafungwa kula kwa jasho lao. Lakini wafungwa hawa wengi wakitoka magerezani wanakua hawana elimu yoyote waliyopata wao ili iweze kuwasaidia kujiajiri mtaani hususani kilimo. Hivyo serikali ipeleke wataalamu wa kutosha kufundisha magerezani ili wafungwa wakija uraiani wawe ni wenye manufaa katika kuzalisha mali hususani mazao ya kilimo.
4. Elimu bora ya kilimo vitendo kwenye maeneo mbalimbali nchini yenye ardhi kubwa isiyokaliwa na watu
Nchi ya Tanzania ina maeneo mengi ambayo hayakaliwi na watu. Hivyo basi maeneo hayo yanapaswa kubadilishwa yawe ni maeneo ambayo serikali itawakodishia wananchi na kuwapa elimu kwanza ya kilimo gani cha manufaa na kuwaongoza katika kuwaombea mikopo, pembejeo na masoko ili wananchi wengi waweze kunufaika na ardhi yao. Wnanachi wakipewa maeneo na kuelekezwa shambani kwa vitendo itakua chachu ya watu wengi kupenda kilimo kwa maana nchi itakua na chakula cha kutosha na kuuza nje ya nchi na kukuza pato la taifa.
Hitimisho
Serikali ijitahidi kuboresha elimu ya kilimo kwa mfumo wa vitendo kwa kuhakikisha bajeti inakua inatosheleza mahitaji na mipango ya wizara. Pia kuwepo na mifumo mizuri itakayowezesha fedha za bajeti zitumike ipasavyo na kuleta.

Upvote
2