Salma Bahame
New Member
- Jun 16, 2024
- 1
- 4
TANZANIA TUITAKAYO.
SEKTA YA ELIMU.
Katika sekta ya elimu serikali ya Tanzania ina fanya jitihada katika kuiboresha sekta hii muhimu ya kadri siku zinavyo zidi kwenda mfano; kwa kutoa elimu bure ngazi ya msingi hadi sekondari kuongeza madarasa kwa sehemu zenye uhitaji mjini kwa vijijini,vifaa vya kufundishia kama vitabu. Lakini hatuja fikia malengo katika elimu yetu nchini Tanzani kuna madhaifu ambayo yamejitokeza kufanya tusifikie ama tusiwe katika nchi zilizo endelea. Madhaifu yaliyopo ni kukosekana kwa elimu ya kujiamini na kujiajiri.
Kujiamini: ni kitu muhimu katika maisha inaweza kua katika kile unachokifanya ama kuyafanya, kujiamini kwa mtu hufanya watu wengine kupata mawazo mazuri pia kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Elimu ya kujiamini inakosekana katika mitaala yetu ya elimu wanafunzi hawafundishwi katika kuamini wayafanyayo hii humsababishia kuwa muoga nakuona ayafanyayo si sahihi. Mwanafunzi anapokosa uwezo wakujiamini darasani kwa kunyosha mkono na kujibu swali hupata madhara kama yafuatayo kile ambacho anakifikiria kichawani ana amini hakitoshi cha mtu mwingine kinatosha jambo lingine kuogopa kusema kitu au jambo kwa sababu ana amini mtu mwingine akiongea atakua bora kumzidi humteneneza yeye kuwa tegemezi kusubiri wengine waseme.
Mfano mimi nikiwa na soma elimu ya msingi mwaka 2010-2016 katika moja ya shule za msingi jijini Dar-es -saalam sikua na uwezo wa kusimama na kuzungumza mbele ya darasa hata kitendo cha kujibu maswali ilikua ni changamoto kwangu. Pasi na shaka walikuwepo walio kama mimi na desturi ilikua ni kukaa nyuma ya darasa na kupisha walio na uwezo wa kujibu mawali kwa kujiamini. Tofauti ilikua kubwa kati ya sisi tusio jiamini na wale waliokua wakijiamini kitaaluma walikua vizuri. Pia swala lakutojiamini hua tatizo katika elimu ya juu watu husindwa kuzungumza wakati wa kuwakilisha kazi zao mbele ya darasa ili ni tatizo. Swali ni je kutokujiamini kwa wanafunzi ni vipi tutapata viongozi au walimu wa badae?
Kujiajiri: Elimu ya Tanzania haimuandai mwanafunzi kujiajiri bali kuajiriwa baada ya kumaliza masomo, na baadala yake humfanya kuzunguka na bahasha ya kaki pamoja na kumaliza bando kwa kufanya maombi ya kazi sehemu tofauti toofauti kwa kutumia mitandao ya kijamii bila mafanikio yoyote. Takwimu ya vyuo vikuu kutoka Wizara ya Elimu sayansi na teknolojia inaonyesha mwaka 2022/2023 idadi ya wanafunzi walio sajiliwa ni 240,523 ambapo vyuo vya umma vimesajili wanafunzi 162,553 na vyuo binafsi 77,970.
Idadi hii yote ya wanafunzi haiwezi kupata ajira kwa pamoja elimu ya kujiajiri ina hitajika katika mfumo wa elimu wa Tanzania, huu ni udhaifu uliopo katika sekta ya elimu. Katika nchi zilizo endelea huangalia mtoto ana penda nini na ndipo huanza kumuwekea jitihada katika hicho anachokipenda huku akiendelea kupata elimu ya kwaida darasani. Lakini Tanzania mtoto atanza madarasa yote msingi atafika sekondari atakapo ingia chuo kikuu ndipo hupata nafasi ya kuchaua nini anataka kusomea.
Hakuna chenye mwanzo kisichokua na mwisho, yafuatayo yafanyike ili kutatua changamoto hizi na kufuta madhaifu haya katika sekta ya elimu Tanzania katika swala la kujiamini kujiajiri:
Kwanza kabisa mtaala wa elimu wa Tanzania unatakuwa kubadilishwa kwa kumpa nafasi mwanafunzi kuanza kusoma au kujifunza nini anapenda kwa mfano mwanafunzi anaependa mitindo kama akiendelea kujifunza huku anasoma huyu akimaliza na kukosa ajira atajiajiri mwenyewe. Hatakua anasubiri ajira serikalini.
Kuwapa wanafunzi wote nafasi ya kushiriki darasani kwa kujibu maswali kuanzia ngazi ya elimu ya msingi kwani samaki mkunje angali mbichi. Mazoea hujenga tabia kwa mtindo huo mwanafunzi atakapo endelea kusoma atakua na uwezo wa kuzungumza bila kuwa na uoga. Kwa namna hii sekta ya elimu ya Tanzania itazalisha vijana wa somi ambao ndio viongozi wa badae watakao simamia misimamo ilio sahihi mbele za watu kwa kujiamini bila kuogopa chochote. Pia viongozi watakao ipigania nchi yetu kokote waendako na kuitangaza na kuzungumza mazuri kuhusu Tanzania, vilevile wanafunzi hawa watakao kuwa viongozi wataweza kutetea haki za wanyonge katika jamii kwa kuwa wanaharakati pia wabunge.
Pia wizara ya elimu na sayansi na teknolojia nchini Tanzania ina paswa kuweka mfumo wa elimu ya kujiajiri kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kila mwaka idadi kubwa ya wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya umma na binafsi humaliza kwa pamoja si rahisi kila mtu atakae mliza kupata ajira serikalini ama taasisi binafsi. Mwanafunzi anapo pewa elimu ya kujiajiri humfanya anapo maliza kwenda kutafuta chakufanya na sikuaa mtaani kusubiri ajira. Elimu hiyo inaweza kuwa biashara, kuwapa elimu juu ya mitandao ya kijamii inavyo welimueza kuwa fursa kwao na kutengeneza pesa watakazo kua wana pata kupitia biashara zao.
Vile vile elimu ya kujiajiri haitakua na faida kwa mwanafunzi tu atakae maliza ya chuo kikuu huenda kuwa msaada kwa serikali ya Tanzania kwa ujumla kwa sababu wale watakao maliza na kupata chakufanya wataweza kurejesha ile mikopo ambayo wamepatiwa na serikali na serikali kuwapatia wanafunzi wengine, kwa namna hii serikali itakua imepunuza mzigo mkubwa. Tofauti na watu kumaliza na kukaa bila kupata kazi ya kufanya itakayo wapatia kipato na kurejesha deni hilo katika bodi ya mkopo.
Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kufanya marekibisho hayakatika sekta ya elimu juu ya kujiamini na kujiajiri. Tutapata mabadiliko makubwa ndani ya miaka mitano kwani tutazalisha wafanyakazi wengi Zaidi walio ajiriwa na kujiajiri. Yale maneno ya kua hakuna ajira yatapotea, matukio ya kialifu kama wizi yatapotea kwa sababu kila mtu atakae maliza elimu yake ya chuo kikuu atakuwa makini kwenye kuchapa kazi kwa bidii na kutafuta cha halali.
Elimu bora na si bora elimu.
Tanzania Tuitakayo

Upvote
5