ELIMU YA KUJITAMBUA KWA BINTI WA KITANZANIA.
Pamoja na juhudi za serikali kuwekeza zaidi katika kumpatia mtoto wa kike elimu ya darasani (shuleni ) lakini bado tunaona kuwa namba ya mabinti walioishia njiani na kukatisha masomo yao kwa miaka kadhaa iliyopita imekuwa ikiongezeka siku baada ya siku.Jambo hili limetokana na ukosefu wa elimu ya kujitambua kwa mabinti wengi wa kitanzania hasa maeneo ya vijijini na hivyo kusababisha ndoto za wengi wao kuishia njia au kuchelewa kukamilika.
Ninapozungumza kwa habari ya elimu ya kujitambua natamani sana tujue maana yake halisi ili iwe rahisi kulielewa jambo hili kwa mapana zaidi,kwanza kabisa tuanze na maana ya elimu.Elimu ni maarifa anayopatiwa mtu ili kumrahisishia kufanya jambo fulani kwa wepesi na kujitambua ni uwezo wa kujua wewe ni nani,unapaswa kufanya nini na kwa wakati gani ili kupata matokeo sahihi kwahiyo kwa ujumla elimu ya kujitambua ni maarifa ambayo yanampa mtu uwezo wa kujua yeye ni nani na thamani aliyo nayo (umuhimu wake) hapa duniani hivyo kumfanya kutumia wakati wake vyema kupata matokeo chanya.
Madhara ya ukosefu wa elimu ya kujitambua .
Kwa jamii nyingi za kitanzania elimu hii imekosekana kwa mabinti ndio maana kumekuwa na idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimba katika umri mdogo.Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2015 mpaka 2019 kuna ongezeko kubwa la wasichana wa shule za sekondari kupata mimba kutokea idadi ya wasichana 3,439 hadi 5,398 (kwa mujibu wa jukwaa la MWANANCHI)
Pia idadi kubwa ya wasichana waliopata mimba kwa miaka hiyo inaonyesha ni kubwa kwa maeneo ya vijijini (mikoani ) kuliko Dar es salaam kwasababu ya ukosefu wa elimu ya kujitambua.Wazazi wengi wa kitanzania wamekuwa wakitumia lugha za kukemea zaidi badala ya kuwaambia mabinti wanachopaswa kufanya hivyo kwasababu ya kutojua wanachopaswa kufanya kwa wakati sahihi mabinti wengi wamejikuta wakipata mimba bila kutarajia .
Kwasababu ya ukosefu wa taarifa sahihi mabinti wamekutana na wanaume waliowalaghai kuwa wakishiriki ngono kwa mara moja na wakaamini na mwishowe wakajikuta kwa kitendo cha mara moja wameangukia kwenye mimba za utotoni .Ni kosa kubwa mno wanalofanya wazazi wa kitanzania kuamini kuwa watoto wao bado wadogo kuwaeleza juu ya elimu ya kujitambua na uzazi kwa ujumla ilihali wameshavunja ungo (wameshakuwa watu wazima).Suala la wazazi kutokuwa wa wazi kwa mabinti zao hasa maeneo ya vijijini na kutumia ukali zaidi imekuwa chanzo kikubwa cha mabinti kuharibikiwa .
Jambo hili limekuwa kilio kikubwa mno kwani ndipo ndoto nyingi za mabinti huzimwa na kushindwa kukamilika kabisa ama kwa wakati,naishukuru serikali ya mama ambayo imeamua kuwarudisha mabinti waliokwama kuendelea na masomo kurudi mashuleni.Ni jambo zuri kwani kwa miaka ya 2021 na kurudi nyuma wanafunzi hawakupata nafasi hiyo .Lakini jambo hilo bado halileti msaada kwa asilimia kubwa kwani hata kama mabinti hawa watarudi shule lakini kuna muda ambao wameshaupoteza mtaani ambapo umesababisha ndoto zao zitimie kwa wakati.
Lakini pia kwasababu ya ukosefu wa elimu ya kujitambua ,mabinti wengi wamekosa kujua thamani waliyonayo hata kutamani kufanana na wanaume.Naamini umeshawahi kukutana na aina hii ya wasichana ambao wanajaribu kujibadilisha kimuonekano kwa kuvaa mavazi ya kiume,kunyoa kama wanaume na hata kuongea na kutembea kama wanaume.Yote hii ni kwasababu wengi kati yao wamekosa elimu sahihi ya kujitambua hivyo kuona kama kuwa msichana si jambo la thamani.
Mabinti wengi tangu wakiwa wadogo wamekuwa wakitamkiwa maneno mabaya kama una sura mbaya,miguu mibaya ,shepu mbaya na mambo mengine yafananayo na hayo hivyo kujikuta wanapoteza uwezo wa kujiamini na kujiona kama wana thamani .
Ukosefu wa elimu ya kujitambua imefanya mabinti wengi kuona kama hawana umuhimu kwenye jamii,hivyo kujikatia tamaa hata ya kupambania ndoto zao.Wazazi na walezi wamekuwa wa kwanza kuwaonyesha mabinti udhaifu wao na hivyo kuwafanya wajione dhaifu na hawawezi kufanya mambo makubwa ya kuleta mabadiliko.
Tunaye raisi wetu wa awamu ya tano mheshimiwa Samia Suluhu,mawaziri wanawake kama Ummy Mwalimu,Joyce Ndalichako,spika wa bunge Tulia Ackson,wote hawa waliwahi kuwa mabinti lakini kwasababu walitambua umuhimu walionao katika kuibadilisha jamii ndio maana wameweza kuzifikia nafasi walizopo.
Vipi kama wangejiona dhaifu,hawawezi, hawana umuhimu wowote !Je tungepata wapi raisi mwanamke leo hii??Hakika tusingempata,hii ni kuonyesha kuwa kama binti akiwa na elimu ya kujitambua ndani yake basi hakika ni rahisi kuzifikia ndoto zake.
Faida ya elimu ya kujitambua
Elimu ya kujitambua inamsaidia binti kufanya uchaguzi /maamuzi sahihi ,kwani atakuwa ameshajua thamani yake na umuhimu alio nao katika jamii hivyo hawezi kuruhusu kufanya jambo litakalomuharibia au kushusha thamani yake.Hata kama binti huyo akiwa katikati ya watu wenye tabia mbaya bado atakuwa na uwezo wa kujisimamia asiharibiwe na tabia zao mbaya.
Pia inampa kuishi maisha borayenye kuleta thamani na heshima kwake katika jamii inayomzunguka.
Nahitimisha kwa kusema kwamba,serikali ilitazame jambo hili kwa upana sana kama tunahitaji kuona mabinti wa kitanzania wanafikia ndoto zao kwa wakati.Elimu ya kujitambua itolewe kwa mabinti mashuleni tena ikiwezekana liwe somo kabisa ili kuwapa uwanja mpana wa mabinti kulielewa jambo hili.
Lakini pia wazazi na walezi wawe wa wazi kwa mabinti zao wanapoona wamefikia umri wa ukuaji ili kuwapa maarifa sahihi yatakayowasaidia kushinda vishawishi na mambo yote yenye lengo la kuua ndoto walizo nazo.
Naamini kabisa kama serikali,wazazi na walezi pamoja na taasisi binafsi zikishirikiana katika kutoa elimu hii kwa ukubwa basi suala la mimba za utotoni (katika umri mdogo) tutaweza kulishinda kwa asilimia kubwa sana.

Upvote
10