Ukisoma biblia mamajusi(wanajimu) watatu kutoka mashariki walisoma na kuifuata nyota kutoka mashariki iliyowaongoza kutoka mashariki walipokuwepo hadi Bethlehemu alipozaliwa mfalme wa Wayahudi(Yesu Kristo).
Je ni sawa kwa mkristo kushiriki kwa namna yoyote katika usomaji nyota(unajimu)?
sio sawa. Mamajusi wa mashariki walikuwa wapagani tu. Mungu anataka tumwendee yeye kwa kumwamini, sio kwa kuchunguza-chunguza. Pia soma KUMBUKUMBU LA TORATI 18
Kumbukumbu la Torati 18 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁰ Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
¹¹ wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
¹² Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
¹³ Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.