Elimu ya kutosha itolewe kuepusha vifo vitokanavyo na ulaji wa kasa

Elimu ya kutosha itolewe kuepusha vifo vitokanavyo na ulaji wa kasa

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
413
Reaction score
471
Si mara ya kwanza hapa nchini kusikia watu wamepoteza Maisha kwa kula samaki aina ya KASA, na hivi majuzi tena tumesikia watu saba kutoka Kijiji cha Bweni na Kanga Wilayani Mafia mkoani Pwani wamefariki dunia kwa kula samaki huyo anayesadikiwa kuwa na sumu.

Matukio haya yanapaswa KUWAAMSHA na wahusika waanze kutoa elimu kwa umma,Ili jamii iepuke matumizi wa samaki huyo ambaye ni nyara ya Serikali na kupunguza athari kwa wananchi.

Ni jambo la kushangaza wananchi wanaendelea kupoteza maisha, huku wahusika wakiwa wamekaa kimya bila kuchukua hatua za kuwanusuru kuepukana na changamoto hiyo.

Pamoja na hayo, ni muhimu wavuvi kusisitizwa kuzingatia kanuni na sheria za uvuvi, ikiwemo kutovua au kula kasa.

.
Untitled design (17).jpg
 
Ni ngumu kusikia wavuvi wamekufa ila wananchi hawajui hao samaki wanajilia tu...Hayo samaki wa baharini hawaeleweki wengine ni sumu .

Kama nyama au samaki una mushkeri nayo usile kabisa ...
 
Ni ngumu kusikia wavuvi wamekufa ila wananchi hawajui hao samaki wanajilia tu...Hayo samaki wa baharini hawaeleweki wengine ni sumu .

Kama nyama au samaki una mushkeri nayo usile kabisa ...
Sahihi, wavuvi hawali lakini wao ndio wanawavua
 
Unakula nyara ya serikali aalafu unataka elimu ni sawa na ukawape elimu wawindaji haramu wa tembo namna gani zile pembe zinatumika. Nyara acha iwauwe
 
Muache uroho mbona mrembo hivyo jamani
 
Huyu sio samaki ni kobe maji. Samaki anasifa zake hadi kuitwa samaki. Huyu ni kobe na ndio maana mayai yake hutagia nchi kavu.
 
Back
Top Bottom