Elimu ya magonjwa ya mbwa (LEPTOSPIROSIS) 01

Elimu ya magonjwa ya mbwa (LEPTOSPIROSIS) 01

Tulip22

New Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
4
Reaction score
5
Habari wa kuu, naomba kushea pamoja nanyi maarifa juu ya ugonjwa wa mbwa ambao hua haupewi kipaombele sana na wafugaji wengi. Lakini unaweza pelekea kupoteza maisha ya mbwa endapo hatua stahiki hazitachukuliwa.

Aidha nitakua nikitumia jukwaa hili kushea nanyi taarifa mbali mbali zinazo husu mifugo na ufugaji kadri muda utavo kua ukiniruhusu. Karibu tujivunze sote.

Leptospirosis ni ugonjwa unao sababishwa na bacteria walio ndani ya kundi la Leptospira.
Ugonjwa huu una wapata mbwa wa umri wowote, pia binadamu na wanyama wengine wanaweza kupata ugonjwa huu. Hivyo ni muhumu kwa familia kuchukua tahadhari stahiki kuepuka kupata ugonjwa huu.

Dalili za ugonjwa: Ugonjwa huu unaathiri figo na maini ya mbwa na kupelekea vishindwe kufanya kazi Kama kawaida yake. Dalili za jumla za ugonjwa huu ni : Mbwa kukonda ghafla, mbwa kuchoka na kukosa nguvu, kutapika, maumivu ya tumbo.

Dalili za mwishoni kabisa, mbwa hubadililka rangi sehemu za ufizi (gums) na sehemu za ndani ya mapaja na kua na unjano Zaidi (jaundice in gums and medial thigh).

Pia mbwa huonesha mabadiliko ya kitabia Kwa upande wa kunywa maji na haja ndogo, ambapo mbwa ataonesha dalili za kua anakunywa maji kwa wingi kuliko kawaida yake na anakojoa mara Kwa mara/hakojoi kabisa.

Maambukizi: Ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa mbwa mmoja kwenda kwa mwingine, Mbwa hutoa bacteria anapokua anakojoa na kusambaza kwenye mazingira ambapo wanyama wengine (ikiwepo na binadamu) wanaweza kupata maambukizi.

Kinga: Leptospirosis ni ugojwa unao weza kuzuiliwa kwa kuwapa mbwa chanjo. Kwa nchi zetu Africa, mara nyingi chanjo hii imechanganywa na chanjo nyingine 4 za mbwa yaani Parvo virus infections, Canine distemper, Hepatitis, Parainflueza complex (DHLPP). Chanjo hii inampa mbwa kinga kwa muda wa mwaka mmoja, hivyo ni muhimu mbwa wako akapata chanjo hii kila mwaka kwa usahihi.

Hata hivyo mbwa wanaweza kuugua hata kama wamechanjwa chanjo hii. Hii inaweza kutokaea endapo mbwa atakutana na aina tofauti ya bacteria na ile iliopo kwenye chanjo, lakini tafiti zinaonesha mbwa aliechanjwa hua haonyeshi dalili kali za ugonjwa na anapoma mapema akianzishiwa matibabu.

Matibabu: kwa hatua za awali za ugonjwa mbwa hua wanatibiwa na kupona, japo matokeo sio mazuri kwa mbwa walio chelewa kufanyiwa matibabu. Hivyo wafugaji wa mbwa wanashauriwa kuwasiliana na mtaalamu wa mifugo alie karibu, mapema kabisa pindi waonapo dalili za huu ugonjwa.

Brown, Moses M,
Daktari wa Mifugo,
Morogoro Tanzania,
+255 766 348 089
 
Sema wabongo hawanaga muda na tiba za pet animals. Ni wachache sana wanaofikiria kutafta tiba za mbwa na paka. Very few!
 
Sema wabongo hawanaga muda na tiba za pet animals. Ni wachache sana wanaofikiria kutafta tiba za mbwa na paka. Very few!
Japo kuna baadhi hua hawako responsible na utunzaji wa mbwa. Ila wengi sasa hivi wanatunza mbwa vizuri kama mwana familia.

Imagine umenunua mbwa wako 300k - 500k akiwa puppy now amekua ndo umpoteze kizembe. Sizan kama utakubali.

Yote kwa yote tuendelee kupeana elimu tu, hopefully in the future people will be responsible.
 
Moderator ulie edit uzi wangu sijui ulikua na maana gani. Ila sijapenda umepoteza maana ya kichwa cha uzi wangu 🙄🙄
 
Back
Top Bottom