Elimu ya Mlipa Kodi Yaendelea Kutolewa Chalinze Mkoa wa Pwani

Elimu ya Mlipa Kodi Yaendelea Kutolewa Chalinze Mkoa wa Pwani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MHE. SUBIRA MGALU ATOA ELIMU YA MLIPAKODI CHALIZNE MKOA WA PWANI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mhe. Subira Mgalu ambaye ni Balozi wa kuhamasisha kulipa kodi tarehe 2 Mei, 2023 aliwahamasisha wafanyabiashara wa eneo la Mdaula Wilayani Chalinze kuhusu masuala mbalimbali ya kodi wakati wa Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi Mlango Kwa Mlango inayoendelea mkoani PWANI.

Mhe. Subira Mgalu amesema yeye kama Balozi wa kuhamasisha kulipa Kodi anahamasisha viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika mikutano na wanawake wote wahamasishe masuala ya kudai Risiti wanapofanya manunuzi kwani wanawake ni wanunuzi wakubwa wa bidhaa mbalimbali na kwa kufanya hivyo wataisaidia Serikali kupata mapato stahiki kupitia TRA.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, amekutana na waandishi wa habari na kutangaza rasmi uzinduzi wa "Kampeni ya Tuwajibike" inayolenga kuwahamasisha walipakodi na wananchi kwa ujumla kuhusu wajibu wao wa kutoa na kudai risiti sahihi za EFD. Mkutano huo umefanyika leo tarehe 2/5/2023 katika ofisi za TRA jijini Dar es Salaam.
 

Attachments

  • FvHeygRX0AEGEWW.jpg
    FvHeygRX0AEGEWW.jpg
    122.8 KB · Views: 5
  • FvHezgDWIAAVay2.jpg
    FvHezgDWIAAVay2.jpg
    156.5 KB · Views: 3
  • FvHezD5XgAAicfJ.jpg
    FvHezD5XgAAicfJ.jpg
    103.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom