Tanzania ni moja ya mataifa masikini duniani ikiwa na asilimia kubwa ya watu wanaotegemea kilimo cha kujikimu na shughuli za uchuuzi wa bidhaa hususani chakavu ama zenye viwango duni kutoka nje kwa ajili ya kipato. Hali hii huwaweka katika hali tegemezi kiuchumi kutokana na njia zisizotabirika za mapato.
Matumizi hafifu ya teknolojia, taratibu kwamishi za mitaji pamoja na mikakati duni ya masoko ndio chimbuko la umasikini wa watanzania na nchi za kusini hususani afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Hali hii imesababisha vijana wengi kujikita katika Michezo ya kubahatisha, mikopo umiza pamoja na utapeli wa mitandaoni kama ndio njia nyepesi ya upatikanaji mitaji kwa shughuli ambazo hawana weledi nazo katika mazingira ya soko huria, hali inayozidi kuwapeleka pembezoni kiuchumi.
Hata hivyo Tanzania inatekeleza agizo la Dakar-Senegal, (2000) kuhusu elimu kwa wote (EFA)
ambapo pamoja na kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu pia linasisitiza kutoa maarifa na ujuzi wa kazi kwa vijana na watu wazima. Lengo ni kuwawezesha kushiriki shughuli zenye tija kiuchumi kama ilivyo katika azimio namba 8 na namba 9 la maendeleo endelevu (SDGs) 2030 la ajira zenye tija kwa wote pamoja na Kupunguza tofauti kiuchumi na kijamii.
Katika kutekeleza hayo Tanzania imekuwa ikifanya mapitio na mabadiliko ya sera ya elimu kadiri inavyohitajika. Sera ijayo inapendekeza elimu ya lazima kuwa kidato cha nne ikitolewa bila malipo kwa elimu ya Msingi kuwa miaka sita na elimu ya sekondari kuwa ya lazima kuwa miaka minne. Hili ni Jambo la kupongezwa kwa sababu kwa hesabu za haraka kama mtoto ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka saba maana yake atamaliza elimu ya lazima akiwa na miaka kumi na saba. Hii itamwepusha na ndoa pamoja na ajira za utotoni ambazo ni hatari kwa mtoto na kwa taifa pia.
Pamoja na mazuri haya bado naziona changamoto kubwa mbili katika utekelezaji wa mfumo huu.
Kwanza ni utayari wa rasilimali za utekelezaji. Hapa namaanisha vyumba vya madarasa na idadi ya walimu sambamba na ongezeko kubwa la wanafunzi katika elimu ya sekondari. Hali hii inaweza kuathiri ubora katika utoaji wa elimu. Ni wazi sasa tunalipeleka kundi kubwa kutoka elimu ya Msingi kwenda sekondari.
Pili ni utayari wa baadhi ya wanafunzi kupata elimu ya sekondari. Mfumo huu utamlazimisha mwanafunzi nini ajifunze kulingana na matakwa ya serikali (Centralized education ) katika umri muhimu wa mtu kuibua na kuendeleza kipaji chake.Matumizi hafifu ya teknolojia, taratibu kwamishi za mitaji pamoja na mikakati duni ya masoko ndio chimbuko la umasikini wa watanzania na nchi za kusini hususani afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Hali hii imesababisha vijana wengi kujikita katika Michezo ya kubahatisha, mikopo umiza pamoja na utapeli wa mitandaoni kama ndio njia nyepesi ya upatikanaji mitaji kwa shughuli ambazo hawana weledi nazo katika mazingira ya soko huria, hali inayozidi kuwapeleka pembezoni kiuchumi.
Hata hivyo Tanzania inatekeleza agizo la Dakar-Senegal, (2000) kuhusu elimu kwa wote (EFA)
ambapo pamoja na kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu pia linasisitiza kutoa maarifa na ujuzi wa kazi kwa vijana na watu wazima. Lengo ni kuwawezesha kushiriki shughuli zenye tija kiuchumi kama ilivyo katika azimio namba 8 na namba 9 la maendeleo endelevu (SDGs) 2030 la ajira zenye tija kwa wote pamoja na Kupunguza tofauti kiuchumi na kijamii.
Katika kutekeleza hayo Tanzania imekuwa ikifanya mapitio na mabadiliko ya sera ya elimu kadiri inavyohitajika. Sera ijayo inapendekeza elimu ya lazima kuwa kidato cha nne ikitolewa bila malipo kwa elimu ya Msingi kuwa miaka sita na elimu ya sekondari kuwa ya lazima kuwa miaka minne. Hili ni Jambo la kupongezwa kwa sababu kwa hesabu za haraka kama mtoto ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka saba maana yake atamaliza elimu ya lazima akiwa na miaka kumi na saba. Hii itamwepusha na ndoa pamoja na ajira za utotoni ambazo ni hatari kwa mtoto na kwa taifa pia.
Pamoja na mazuri haya bado naziona changamoto kubwa mbili katika utekelezaji wa mfumo huu.
Kwanza ni utayari wa rasilimali za utekelezaji. Hapa namaanisha vyumba vya madarasa na idadi ya walimu sambamba na ongezeko kubwa la wanafunzi katika elimu ya sekondari. Hali hii inaweza kuathiri ubora katika utoaji wa elimu. Ni wazi sasa tunalipeleka kundi kubwa kutoka elimu ya Msingi kwenda sekondari.
Hali hizi zitaathiri ubora wa elimu itakayotolewa pamoja na kuwa na matumizi yasiyo na tija kwa jamii kutokana na kugharamia elimu kwa baadhi ya wanafunzi ambao hawapo tayari kuipokea wakiona kama wanapoteza muda katika kufikia maono na matarajio yao. Ushahidi wa hili ni utoro na utukutu wa baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari kwa sasa.
Kwa kuwa mahitaji ya taifa ni ujuzi na maarifa ya kazi kupitia nguvu kazi muhimu ya vijana, basi vijana waachwe huru kuamua ni ujuzi gani wanahitaji kulingana na vipaji na mapendekezo binafsi. Hivyo badala ya kuwalazimisha kwenda sekondari basi wakifika darasa la sita wachujwe wale ambao wanastahili kuendelea na elimu ya sekondari (Centralized education) na wale wanaohitaji ujuzi fulani (Decentralized education) basi wapelekwe vyuo vya ufundi stadi FDC na VETA pamoja na Shule maalumu kwa ajili ya michezo na Sanaa kwa miaka hiyo hiyo minne na bila malipo.
Halikadhalika kwa kidato cha nne, mtazamo usiwe kupeleka kidato cha tano bali vyuo vya kati kwa ajili ya kuvuna mapema vipaji na nguvu kazi muhimu kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya kiuchumi. Kama ni suala la kujiendeleza basi mtu atajiendeleza kupitia taaluma yake. Hali hii itatusaidia kama taifa kuwa na mtazamo wa kutoa elimu kiuchumi zaidi kuliko matakwa ya kisiasa. Hii ni kwa sababu tuna kundi kubwa tunaloligharamia elimu ya chuo kikuu ambalo halina mrejesho wa kiuchumi na kuwa mzigo mkubwa kwa walipa kodi.
Tunashauri pesa itakayookolewa katika mapendekezo hayo itumike kukopesha wahitimu wa FDC na VETA kwa miradi ya uzalishaji ili taifa liingie katika uchumi wa viwanda unaochochea ajira na kipato kinachotabirika.
Lengo ni kuhakikisha kila kijana anashirikishwa kukiandaa na kukitumikia kipaji chake kikamilifu (Decentralization) kwa sababu elimu bora ni ile inayolenga kuibua na kuendeleza kipaji cha mtu (A learner centered individualized approach within a potential School age leading to creativity and innovation).Kwa kuwa mahitaji ya taifa ni ujuzi na maarifa ya kazi kupitia nguvu kazi muhimu ya vijana, basi vijana waachwe huru kuamua ni ujuzi gani wanahitaji kulingana na vipaji na mapendekezo binafsi. Hivyo badala ya kuwalazimisha kwenda sekondari basi wakifika darasa la sita wachujwe wale ambao wanastahili kuendelea na elimu ya sekondari (Centralized education) na wale wanaohitaji ujuzi fulani (Decentralized education) basi wapelekwe vyuo vya ufundi stadi FDC na VETA pamoja na Shule maalumu kwa ajili ya michezo na Sanaa kwa miaka hiyo hiyo minne na bila malipo.
Halikadhalika kwa kidato cha nne, mtazamo usiwe kupeleka kidato cha tano bali vyuo vya kati kwa ajili ya kuvuna mapema vipaji na nguvu kazi muhimu kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya kiuchumi. Kama ni suala la kujiendeleza basi mtu atajiendeleza kupitia taaluma yake. Hali hii itatusaidia kama taifa kuwa na mtazamo wa kutoa elimu kiuchumi zaidi kuliko matakwa ya kisiasa. Hii ni kwa sababu tuna kundi kubwa tunaloligharamia elimu ya chuo kikuu ambalo halina mrejesho wa kiuchumi na kuwa mzigo mkubwa kwa walipa kodi.
Tunashauri pesa itakayookolewa katika mapendekezo hayo itumike kukopesha wahitimu wa FDC na VETA kwa miradi ya uzalishaji ili taifa liingie katika uchumi wa viwanda unaochochea ajira na kipato kinachotabirika.
Hivyo naishahuri serikali kwamba utoaji wa elimu uzingatie mahitaji ya mabadiliko ya kiuchumi kwa taifa kwa kutoa kipaumbele katika kuvuna vipaji mapema zaidi ili kuwahi kushiriki katika kutumikia uchumi wetu kuliko ilivyo sasa.
Tunahitaji elimu inayotumikia uchumi wetu na siyo uchumi kutumikia elimu kama ilivyo sasa.