Elimu ya Msingi kwa miaka sita: Je, tumejiuliza mambo haya?

Elimu ya Msingi kwa miaka sita: Je, tumejiuliza mambo haya?

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
Kwanza kabisa nimshukuru Mungu kuniwezesha kupata elimu bora kabla siasa za nchi yetu hazijashika hatamu katika ELIMU.

Tunaposema tunataka elimu ya MSINGI iwe miaka sita, kusiwe na mtihani darasa la sita, wanafunzi wote wanaomaliza darasa la sita waende sekondari. je tumejiuliza mambo yafuatayo?

1) Nini maana ya mtihani. Ni nani anatakiwa kufanya mtihani?

2) Je, tangu uhuru changamoto zinazoikabili elimu yetu zimetatuliwa? Mfano, uhaba wa madarasa ( msingi na sekondari), vifaa vya kufundushia na kujifunzia vimewahi kutosheleza? Uhaba wa walimu, nyumba za walimu, na mbaya zaidi madeni ya walimu na malalamiko mbalimbali ambayo yamekuwa yakishusha morali ya walimu.

3) Je, elimu yetu kwa sasa Ina dosari gani zinazotakiwa kushughulikiwa?
4) Je, mfumo wetu wa elimu wa sasa ni Bora au ni Bora elimu.
5) Je, huu ni muda muafaka kufanya haya mabadiliko?
6) Nini maana ya elimu msingi na Nini maana ya elimu sekondari?
7) Je, Serikali imejindaa kuwaandaa walimu kwa ajili ya mfumo huu mpya? Hii ni pamoja na kutoa kozi fupi na ndefu pamoja na semina. Je, gharama hizi serikali itaweza kuzibeba?

MAONI BINAFSI
a) Serikali isikurupuke na utafiti usiozingatia mila, desturi, na utamaduni wa mtanzania. Utafiti usiozingatia mazingira, mfumo wa maisha ya watu, vipaumbele vya jamii, na haki ya mlengwa katika utafiti.

b) Utabiri wangu ni kuwa kamwe mfumo mpya hautaleta tija sababu huu wa sasa ambao unatoa muda mrefu kwa serikali kujiandaa na kutatua changamoto mbalimbali katika ELIMU serikali imeshindwa kuzitatua.

c) Elimu bora sio tu kujenga madarasa mapya ni pamoja na kuboresha miundo mbinu, kuwa na walimu bora waliopikwa kisawasawa, na kuwa na vitendea kazi toshelezi

d) Km darasa la sita wote wataenda sekondari, tutarajie elimu mbovu kuliko tuliyo nayo sasa. Tukumbuke, walimu na vitendea kazi havijawhi kutosheleza sekondari Wala msingi na haitatokea kwa karine hii hili liwezekane. Sababu tangu uhuru bado wanafunzi wana Kaa chini.

e) Tusifanye elimu kama daraja la majaribio katika kuyafikia maisha bora ya Watanzania. Ukichezea elimu ni sawa na kuchezea nyeti za mwanaume ambazo ndio zimebeba sifa ya kuitwa mwanaume kwani uhai wa mwanaume upo hapo

f) Mifumo hii inapobadilishwa, basi sera, sheria, na miongozo ya elimu nayo ibadilishwe ili watoto wa viongozi wote wa serikali iwe lazima kusoma shule za serikali tena za kata. Viongozi wetu waone umuhimu wa kuyaishi maisha yale wanayo hubiri. Kwani hujadili kwa ajili ya nani.

g) Inatupasa kujua maana ya elimu msingi na elimu sekondari na manufaa yake.

h) Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi. Kuwa na wanafunzi wengi waliohitimubelimu ya sekondari haimaanishi hiyo ndio elimu bora.

Watanzania tujisahihishe, hatujachelewa.
 
Back
Top Bottom