La3
Member
- Jul 29, 2022
- 17
- 17
Elimu ya msingi ni eneo nyeti sana katika safari ya maisha ya mwanafunzi au mtu yeyote.
Ni katika elimu ya msingi tu ndipo mtu anafundishwa kujua kusoma, kuandika na kuhesabu ambayo ni mambo muhimu mno kwenye maisha. Kwa hiyo ni muhimu sana kuwekeza kwenye elimu ya msingi zaidi kwa kuwa huku ndiko mahali ambako kukiharibika, safari nzima inaharibika. Ukiwekeza vizuri huku utawapunguzia mzigo walimu wa sekondari ambao wamekuwa wakipata taabu kufundisha wanaunzi.
CHANGAMOTO ZINAZOKABILI ELIMU YA MSINGI:
1. Kukosekana ushirikiano wa karibu kati ya mwalimu na mzazi. unakuta mtoto yuko darasa la tatu, la nne lakini hajui kusoma na kuandika. Ni kweli kuna uzembe mkubwa sana kwa walimu kiasi kwamba unajiuliza huyu mwanafunzi ameweza vipi kuvuka madarasa hayo yote?
Pamoja na uzembe huo wa walimu, wazazi nao ni wazembe zaidi, Unakuta mtoto haandiki, mzazi hapekui daftari za mtoto wake, mzazi hafuatilii maendeleo ya mtoto, yuko bize na mambo yake. Mtoto anahitimu bila kujua kusoma na kuandika mzazi anashangaa, lakini mzazi huyu huyu hajawahi fuatilia maendeleo ya mtoto, hakagui daftari, hana mawasiliano na mwalimu.
2. Mwalimu mmoja kufundisha idadi kubwa ya wanafunzi. Kwa kweli kama wazazi watashindwa kushirikiana na walimu, hali si nzuri kwa sababu ni ngumu mwalimu kumudu kumfuatilia mwanafunzi mmoja mmoja.
3. Mahusiano ya kimapenzi kati ya wanafunzi na wanafunzi, walimu na wanafunzi na mmomonyoko wa maadili ni changamoto nyingine.Watoto hawa wanahitaji malezi makini hasa kwenye zama hizi. Mtoto apewe muda wa kucheza na kusoma .
4. Wazazi au walezi kuzembea katika kuwa makini na watoto wao. Siku hizi kuna matukio ya ubakaji na kulawiti watoto wadogo. Unakuta watoto wanafanyiwa ukatili huu muda mrefu lakini mzazi hajui, Yaani mwalimu ndio anayegundua kitu ambacho sio kizuri. je, mzazi au mlezi kama huyu anaweza kweli kufuatilia maendeleo ya mtoto?
MAPENDEKEZO:
1. Vigezo vya kuwapata walimu viangaliwe upya. Angalau viwango viwe juu kidogo, hii itasaidia kupata walimu wenye wito kwa sababu haitaitwa taaluma ya ya watu wenye ufaulu dhaifu. Zamani ilikuwa ngumu kusikia mwalimu ana mahusiano ya kingono na mwanafunzi lakini siku hizi ni kawaida. Hata uwezo wa walimu wa sasa walio wengi unatia shaka.Hivyo basi kuna haja ya kutazamwa upya vigezo vya ufaulu.
2. Mishahara ya walimu iongezwe ili angalau ifanane na wahandisi au madaktari.Inawezekana watu wanaopenda kuwa walimu wamekimbia kwa sababu ya maslahi yasiyofanana na huduma yao. Hii nayo itachangia kupata walimu wenye wito.
3. Idadi ya wanafunzi iendane na idadi ya walimu .Mwalimu mmoja angalau wanafunzi 45.
4. Upatikanaji wa vitabu shuleni.
5. Miundombinu ya maji iwepo mashuleni ili wanafunzi wasiende mbali kufuata maji.
6. Upatikanaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi na isiwepo siasa katika jambo hili. Kumekuwa na malalamiko mengi, watu hawataki kuchangia, sio vizuri hata kidogo.
7. Maadili ya mwalimu yafuatiliwe kwa karibu, ikiwemo historia zao, wametoka wapi, tabia zao,hasa walimu wa kiume.
8. Ushirikiano kati ya mwalimu na mzazi utasaidia kukuza kiwango cha elimu na kupunguza matukio ya watoto kuhitimu bila kujua kusoma na kuandika. Au mwanafunzi wa darasa la 5,6,7 kushindwa kufanya hesabu ya darasa la 3. Halafu mwisho wa siku huyu mwanafunzi anafaulu kwenda sekondari, baadaye wakifanya vibaya kidato cha nne watu wanakuja na sababu lukuki kwani zamani walifaulu vipi, kumbe sekondari zimejaza wanafunzi wasio na sifa.
9. Walimu wawe makini kufuatilia maendeleo ya wanafunzi ikiwemo mahudhurio, ufaulu wao na sio kupitisha tu.Kutoruhusu wanafunzi wasio na sifa kusonga darasa linalofuata. Ndio maana ya kuwepo darasa la 1 mpaka la 7, mtoto avuke kwa vigezo.
10. Walimu wanaofanya vizuri wapewe motisha.Hii inatia moyo, na huyu ataongeza bidii hata mazingira yawe magumu kiasi gani.
11. Uwezo wa walimu uendelee kuchunguzwa siku zote, maadili, nidhamu ya kazi na tabia zao.Kama ikishindikana hapa, tutarajie mdororo wa taaluma katika nchi yetu.Itasaidia kudhibiti vitendo vyote visivyo na maadili.
12. Ziwepo shule zinazosapoti watoto wenye ulemavu wowote ule kuweza kusoma.Pasiwepo watoto wanaokosa elimu kwa sababu ya ulemavu au uwete.
13. Kuwawajibisha watu wasiopeleka shule watoto wao kwa sababu yoyote ile.
14. Ada inapofutwa na michango pia isiongezwe, ibaki vilevile au nayo ifutwe kabisa.
HITIMISHO:
Mwalimu ni mlezi mkuu kwa sababu ndiye anayekaa muda mrefu na wanafunzi. Anastahili heshima, kupewa ushirikiano.
Wanasiasa waache kutoa matamko yasiyo na afya kwa walimu hasa kuhusu michango mbalimbali hasa ya chakula. Elimu ni sekta isiyohitaji porojo za kisiasa, inahitaji wataalamu. Porojo za siasa zisipewe nafasi kabisa.
Mwalimu ni zaidi ya kiongozi wa dini.
Watu wahamasishwe kutoa sadaka za shukrani kwa walimu pindi watoto wakifaulu kama wanavyotoa kanisani au kwingineko. Unatoa sadaka ya shukrani kanisani mtoto amefaulu, halafu mwalimu unambeza, akili ya wapi? Mambo yakiwa hivi sekta ya elimu itapaa. Mtu anayembeza mwalimu anastahili kuzomewa.

Upvote
1