Elimu ya Sasa Imepoteza Muda Wa Maisha kwa Vijana.

Elimu ya Sasa Imepoteza Muda Wa Maisha kwa Vijana.

PCGAMES

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
782
Reaction score
1,157
Ni muhimu kuzingatia muda katika suala zima la elimu kwani inaonekana elimu za kutumia vitendo zinachukua muda mfupi kueleweka zaidi kuliko nadharia mfano Wanafunzi wanaosoma VETA wanachukua muda mfupi kufunzwa lakini wanakuwa na uwezo mzuri wa kufanya kazi aidha kwa kujiajiri au kuajiriwa. Tofauti na mtu anayefaulu darasa la 7 na kwenda kushindwa kidato cha 4 au 6, anapoteza muda na huwa anarudi uraiani akiwa hana a wala z, halafu anakuja kuanza moja kujifunza fani baada ya kushindwa. Sasa kutokana na kuonekana muda mwingi vijana huwa tunaupoteza kwenye elimu hasa ya kidato cha 4 na 6 ningependekeza katika mchakato uliopo sasa wa kuboresha shule zetu za sekondari kuwe na mafunzo ya vitendo kwa wingi tena ikiwezekana hayo mafunzo yaanzishwe tangu shule za msingi hadi elimu ya sekondari ili pale vijana au wanafunzi wanapoitimu katika hizo nafasi basi anaporudi uraiani aje kuanza kujiajiri au kuajiriwa moja kwa moja. Hii itawasaidia hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kujiendeleza au kuendelea kusoma vyuoni. Pia itasaidia kurudisha kidogo uwiano wa aliyenacho na asiyenacho maana asiyenacho atakaposhindwa kuendelea kimasoma atakuwa amepata ujuzi fulani kulingana na muda aliosoma kuanzia shule ya msingi lakini sio kama sasa ilivyo mtu anamaliza hadi kidato cha 6 lakini hana ujuzi wowote wa kifani. Huu ni upotezaji wa Muda wa maisha ya sisi vijana.
 
Back
Top Bottom