Elimu ya Sheria ya Ndoa itolewe kuanzia ngazi ya chini kabisa

Elimu ya Sheria ya Ndoa itolewe kuanzia ngazi ya chini kabisa

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Katika utafiti wangu mdogo nilioufanya katika mtaa ninaoishi na hata maeneo mengine wanandoa wengi wanaishi bila kujua taratibu za kisheria.

Mfano unakuta Mwanaume huyu awali alikuwa na mke wake wakazaa watoto watatu huku wakiwa na mali walizochuma pamoja.

Lakini mwanaume anaamua kuhama na kuamua kwenda kuishi na mwanamke mwingine bila utaratibu wowote na kuanzisha familia nyingine.

Changamoto inayoweza kujitokeza hapo ni mtu huyu atakapofariki kesi zinaanza wapi atazikwa, mgawanyo wa mali zake utakuaje hapo ndipo ugomvi mkubwa huibuka.

Wengi sana wanaishi bila kufuata taratibu ni muhimu elimu ya sheria ya ndoa itolewe kuanzia ngazi za chini kabisa ili kupunguza migogoro.
 
Back
Top Bottom