MPIKUSASA
Senior Member
- Mar 26, 2013
- 112
- 6
Muenendo wa Elimu ya Tanzania unavyoendelea unatia shaka, kutokana hali halisi ya namna elimu nchini inavyozidi kushushwa na kupoteza maana kabisa. Elimu ya Tanzania kwa ngazi yeyote imepoteza hadhi yake na kugeuka kuwa ujinga. Kibaya zaidi elimu yetu mhimu imekuwa siasa, kias kwamba ile dhima hasa ya elimu imepotea kabisa. Miaka michache iliyopita ilikuwa ukisikia mtu fulani ni Dr, Profesa, unajua ni mtu wa aina fulani ya kipekee katika uwezo wa kifikra,mtizamo, na uelewa wa mambo mbalimbali katika nyajna nyingi. Watu hawa walikuwa ni mhimu na walkuwa wachache sana kulingana na mkutadha wenyewe wa kile walichotakiwa kutokana kwacho. Watu hawa walikuwa ni watu mhimu katika taifa lolote lile liliotaka kuendelea kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, hawa kwa lugha nyingine tungewaita roho, kitovi, dira ya Taifa lolote diniani. Mataifa yote makubwa yaliyoendelea yamechangiwa sana na watu hawa ambao kwa kweli wamekuwa kichocheo cha maendeleo pamoja na uzalendo katika mataifa yao. Leo hii taifa letu limekuwa na utitiri wa doctrines na profesa lakini cha kushangaza hakuna mchango wa kuonekana ukilinganisha na ukubwa wa idadi tuliyonayo swali hapa tunapata je hawa wenzetu wamepata hizi shahada mbalimbali kihalali? je kama hatuwezi kuona mchango wa hawa tunaowaita Dr na profesa wa moja kwa moja kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa hawa walitengenezwa na nani kwa manufaa ya nani? Elimu yetu tanzania imegeuka shimo la kuwazika watanzania kiuchumi, kisiasa, na kiutamaduni.