Elimu ya Tanzania haijawahi kuwa bora ila ni mbovu miaka yote

Mshinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
3,532
Reaction score
1,126
Since so then in 1960s our education has remained worthless and nothing.

Wazee wanaisifia elimu ya enzi zao kuwa ilikuwa bora zaidi lakini mimi nasema hapana maana haikufanikiwa kabisa kulikomboa taifa . Nachoweza kusema ni kwamba ilikuwa angalau kuliko sasa.

Wale wa makamo nao wanasifia enzi zao wakisema elimu ilishia mwanzoni mwa 2000. Lakini nasema bado hatukuwa na cha maana cha kujivunia kwa kuwa elimu na walioelimika hawakuonyesha ubora wowote wa kukomboa taifa.

Ìkaja elimu ya lika langu miaka ya 2000 na kuendelea kabla ya shule za kata, na sisi tunajidai kuwa ile ndio ilikuwa elimu hasa. Nasema hapana na hakuna cha maana kwa elimu ile maana haijakomboa taifa.

Ikaja elimu hii ya kata ambayo ndio pekee inasemwa na wengi kuwa ni mbovu.

Sasa tumeingia BRN nayo ni mbovu kuliko kipindi kingine chochote.

KIFUPI NI KWAMBA KWA MIAKA YOTE ELIMU YETU NI MBOVU YAANI ZERO EDUCATION NA KINACHOTOKEA NI KWAMBA ULE UBOVU UNAONGEZEKA SIKU HADI SIKU LAKINI HATUJAWAHI KUWA NA ELIMU BORA.

kitendo cha watu karibia 11,000 wenye degree kujitokeza kusailiwa kwenye nafasi 70 ni ushahidi tosha hizi degree zetu hapa ni hazina tofauti na zero maana haingii akilini hawa wote hawana ajira na wamekosa kutumia elimu yao kujitajirisha wenyewe ila wanatafuta kazi kwenda kunyonywa na kutumikishwa

nchi zenye elimu bora watu wenye elimu ndio hugeuka kuwa mamillionea kwa kuitumia elimu wao wenyewe na kufanya kitu cha kipekee.

Hata mainjinia wetu nao wapo bussy na bahasha wakitafuta kazi huku wao walipaswa kubuni na kuibua kazi kupitia utaalamu wao
 
nakuuunga mkono!!!!!!

asante maana tumeshindwa kuendelea na tunajipa matumaini hewa kuwa tuna elimu bora ama tumewahi kuwa nayo huku matunda yake hayajawahi kuonekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…