Elimu ya tanzania inalenga kumjengea mwanafunzi uwezo wa kupambana na mazingira yakee ?

Elimu ya tanzania inalenga kumjengea mwanafunzi uwezo wa kupambana na mazingira yakee ?

ABBY MAGWAI

Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
22
Reaction score
0
Elimu kwa ujumla ni uwanja mpana wa kufikiri na kutenda.Tunapozungumzia uwezo wa kupambana na mazingira ni
ile hali ya kutumia maarifa aliyojifunza kijikwamua na hatimaye kujijengea utu na uwezo katika maisha.
Jambo moja la kujuliza ni namna wanafunzi wananyorithishwa maarifa mashuleni ,kweli elimu ta Tanzania kwa kuzingatia hili ina uwezo wa kumwezesha muhitimu kupambana akitumia ujuzi wake ? [ Education for liberation ]
 
Ndio. Na hii inaoneshwa katika mtaala (curriculum), na pia tukumvuke kuwa mtaala uliopo sasa umetengenezwa katika mfumo ambao ni competence-based. Tatizo lililopo no katika uwashilishaji na utahini.

Kwa bahati mbaya au makusudi, waalimu hawajaandaliwa vya kutosha katika kuutekeleza mtaala huu na hata walioandaliwa bado wanafunza kwa mazoea zaidi ya kutumia mbinu mbadala na za kisasa. Pia tatizo kubwa lililop la namna mitihani inavyotungwa na kusahihishwa. Isipokuwa kwa somo la English Language kwa O Level sioni kama kumefanyika uboreshaji wowote katika content ya mitihani.

Senti zangu hamsini!
 
Tatizo lipo pande ya sisi wanafunzi na serikali. Wanafunzi tunapenda spoon feeding na wengi wetu ni wavivu wa kufikiri na kusoma. ingawa inaweza kuchangiwa na malezi na lishe zetu.

Serikali haina mbinu na miundo mbinu bora ya kufundisha na hata kutoa elimu yenyewe. Inakaririsha watoto. Tunatakiwa kuwa na vifaa vya maabara, mashamba darasa ya kutosha, kutumia case studies nyingi zinazoizunguka nchi yetu na pia iwe inalenga kukomboa uchumi wetu. Ila hizo mbinu hazitumiki kuanzia shule za msingi hadi vyuo vyetu viko hivyo. Pia, tulikosea sana kada ya waalimu kuwa ndiyo inayolipwa maslahi madogo, pia wengi wao ndio tuliofanya vibaya mashuleni na hili ndio bomu tunaloliiona.
 
kila waziri wa elimu anaanzisha mfumo wake bila ya kufanya tafiti ya mahitaji,unategemea nini?
 
Elimu ya sasa inafanya hvyo,tofauti na ile ya 05 kurudi nyuma. Sasa hive sylabus na mitihani zinapima uelema(competence),
 
Back
Top Bottom