Tatizo lipo pande ya sisi wanafunzi na serikali. Wanafunzi tunapenda spoon feeding na wengi wetu ni wavivu wa kufikiri na kusoma. ingawa inaweza kuchangiwa na malezi na lishe zetu.
Serikali haina mbinu na miundo mbinu bora ya kufundisha na hata kutoa elimu yenyewe. Inakaririsha watoto. Tunatakiwa kuwa na vifaa vya maabara, mashamba darasa ya kutosha, kutumia case studies nyingi zinazoizunguka nchi yetu na pia iwe inalenga kukomboa uchumi wetu. Ila hizo mbinu hazitumiki kuanzia shule za msingi hadi vyuo vyetu viko hivyo. Pia, tulikosea sana kada ya waalimu kuwa ndiyo inayolipwa maslahi madogo, pia wengi wao ndio tuliofanya vibaya mashuleni na hili ndio bomu tunaloliiona.