Elimu ya Tanzania ni bandia

Elimu ya Tanzania ni bandia

data

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
26,858
Reaction score
23,768
Ndugu wananchi, elimu ya Tanzania ni fake.

Vijana wanaenda shule kuitika majina, watu wanahitimu wanarudi mtaani wameharibika zaidi. Watizameni form four walorejea huko home/mtaani.

Hitimisho
Elimu ya Tanzania ni fake.
 
Ingewekwa mitihani ya bodi kwa waalimu nchini.Tunaweza pata waalimu nchini.
 
Kwenye haya masuala ni lazima uwe na kilinganishio...

Ni feki ikilinganishwa na elimu ya wapi?

Elimu isiyo feki inatoa wahitimu wa kidato cha 4 wa aina gani ili kama inawezekana tukajifunze huko?

Tufanye nini sasa kama ni feki?

Elimu ya mpaka kidato cha nne lengo lake kuu ni kumfanya mwanafunzi ajue, tena kwa juu juu tu, mifumo inayoendesha dunia na mazingira yake kiuchumi, kisiasa, kijamii na hata kisayansi. Na elimu hii inatosha kabisa kumfumbua macho na kama hataki kuendelea zaidi ni sawa. Apatiwe mtaji na kuingia mtaani kwenye ujasiriamali kupambana. Baada ya miaka 10 atakuwa amepiga hatua baada ya kujaribu na kushindwa hapa na pale.

Hebu na tujadili "ufeki" huu wa elimu yetu na jinsi ya kuwasaidia hawa vijana katika mfumo huu wa CCM ambako tumeingia katika mtego huu wa shule nzima kupata divisheni wani za pointi saba saba hata kama wanaozipata hawajui kitu!
 
Watoto wanaharibika kulingana na malezi aliyoyapata kutoka kwa mzazi hiyo haihusiani na mfumo wa elimu tulionao

Mfumo wa elimu unaweza ukawa na kasoro ila katika hizi hoja zako sijaona hoja ambayo inaenda kugusa moja kwa moja eneo lenye madhaifu.
 
Zamani ukisalimia Elimu ni ukombozi shikamooo mwalim Elimu ilikuwa inakomboa Kweli tofauti ya msomi na asiye soma unaiona ila saiv wote sawa Kama Taifa na ccm nasema na ccm maana ndio wenye nchi wanatengeneza bom la wajinga wengi wa Taifa letu mijadala imefanyika mingi na tafiti nying ni wakati kama Taifa tuseme inatosha Elimu yetu isichezewe turudishe mfumo wa pyramid
 
Elimu yetu bado ni ya uswahili uswahili mwingi tu ukiwa unajua kujieleza vizuri na kulielewa swali linataka huyo mtu anayekusahisha umshawishi kwa namna gani unapata maksi nyingi hata kama wewe kwenye vitendo upo tupu, Sasa hivi kwenye mtaala wapo kwenye competence based curriculum lakini ukitizama kwa undani bado wapo kwenye content based curriculum kilichobadilika ni kuzungusha swali na kuweka maneno mengi ila jibu linatoka kwenye content. Mfano swali; mtu amezama kwenye maji ziwani je utamsaidiaje? Jibu: Nitaogelea hadi alipo nitamwambia anishike mguu taratibu nitaogelea hadi nchi kavu. Jamaa anakupa tiki kubwa wakati hata haujui kuogelea.
 
Sasa hivi kwenye mtaala wapo kwenye competence based curriculum lakini ukitizama kwa undani bado wapo kwenye content based curriculum
Hiyo competence inapimwaje ktk piece of paper?
 
Maana ya competence..
Screenshot_20221129-042012.png

Wahitimu ktk level mbalimbali sasa wamehitimu na wako mtaani. Embu tuwaulize wemerudi na uwezo gani.. Au wana special skills gani!?
 
Mfumo wa elimu unaweza ukawa na kasoro ila katika hizi hoja zako sijaona hoja ambayo inaenda kugusa moja kwa moja eneo lenye madhaifu.
Kwa mfano sasa hivi nchini tuna shida kuu mbili..
I. Umeme
II. Maji.

Elimu kazi yake ni kuaddress issues zinazomkabili bidamu na kuzitafutia solutions.

Sasa je! Swali jepesi tu. Embu uliza wahitimu hapo ulipo ktk level yeyote kama wanaweza pendekeza nini kifanyike kutatua shida hizo.

Ukipata watatu tu watakaopendekeza either wapatiwe ujuzi wa kuchimba visima(maji) , kuvuna maji ya mvua..au wapewe ujuzi wa kutengeneza solar pannel(umeme) tafuta soda unywe.

Hivyo basi UFAKE wa Elimu yetu ndo unakuja hapo na kwa vile mtaala ni wa kinadharia mno hakuna mtu anayekuja na mawazo ya kivitendo.
 
🙄🙄🙄🙄 Wacha tupate elimu ya kuchakata mbususu kimasihara
 
Elimu yetu bado ni ya uswahili uswahili mwingi tu ukiwa unajua kujieleza vizuri na kulielewa swali linataka huyo mtu anayekusahisha umshawishi kwa namna gani unapata maksi nyingi hata kama wewe kwenye vitendo upo tupu, Sasa hivi kwenye mtaala wapo kwenye competence based curriculum lakini ukitizama kwa undani bado wapo kwenye content based curriculum kilichobadilika ni kuzungusha swali na kuweka maneno mengi ila jibu linatoka kwenye content. Mfano swali; mtu amezama kwenye maji ziwani je utamsaidiaje? Jibu: Nitaogelea hadi alipo nitamwambia anishike mguu taratibu nitaogelea hadi nchi kavu. Jamaa anakupa tiki kubwa wakati hata haujui kuogelea.
Sijakuelewa... hapo kwenye competence na content hebu rudia
 
Ndugu wananchi, elimu ya Tanzania ni fake.

Vijana wanaenda shule kuitika majina, watu wanahitimu wanarudi mtaani wameharibika zaidi. Watizameni form four walorejea huko home/mtaani.

Hitimisho
Elimu ya Tanzania ni fake.
Uko sahihi.
 
Huenda elimu bandia inakutuma kufanya madili ya ajabu ya kuangamiza nchi ili wachache wanufaike.
 
Back
Top Bottom