Elimu yetu bado ni ya uswahili uswahili mwingi tu ukiwa unajua kujieleza vizuri na kulielewa swali linataka huyo mtu anayekusahisha umshawishi kwa namna gani unapata maksi nyingi hata kama wewe kwenye vitendo upo tupu, Sasa hivi kwenye mtaala wapo kwenye competence based curriculum lakini ukitizama kwa undani bado wapo kwenye content based curriculum kilichobadilika ni kuzungusha swali na kuweka maneno mengi ila jibu linatoka kwenye content. Mfano swali; mtu amezama kwenye maji ziwani je utamsaidiaje? Jibu: Nitaogelea hadi alipo nitamwambia anishike mguu taratibu nitaogelea hadi nchi kavu. Jamaa anakupa tiki kubwa wakati hata haujui kuogelea.