Elimu ya tanzania sasa ni ya majaribio

Elimu ya tanzania sasa ni ya majaribio

mwajama

Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
10
Reaction score
0
Habari wana JF! ninajambo naomba mlitolee mawazo na mada hii ni kwa mara ya pili naiweka mezani ni ili tu kupata mawazo na ufumbuzi toka kwenu juu ya jambo hili, kabala ya kulisema ngoja nikupeni picha ya elimu yetu. ni kwa muda sasa nimekua nikifuatilia mtaala wa elimu yetu toka nipate ufahamu na uelewa wa kuchambua Pumba na Mchele! kama tuna kumbuka sote miaka michache iliyopita kuna wazir mmjo wa elimu alipo pewa wizara ile alitangaza kuwa CHEMISTRY NA PHYSICS yachanganywe pamoja baadae ilionekan hailet tija ikabadilishwa YAONEKANA ALIKUWA ANAFANYA MAJARIBIO. Miaka hiyohiyo ya karibuni lakini kwa Waziri mwaengine alitangaza kuwa mtihani wa darasa la nne na kidato cha pili ifutwe wanafunzi wavuke kidato bila kutahiniwa lakini pia baadae ilionekana haileti tija ikarudishwa tena pia YAONEKANA ALIKUWA ANAFANFA MAJARIBIO. Hivi karibuni Muundo waliotumia kufaanyia mtihani darasa la saba mwaka uliopita ulikuwa wa kiteknolojia wanavyosema lakini hii ilishawahi fanyika mika hihi ya 2000s pia ilikua ya KIMAJARIBIO (Kumbuka majaribio haya yanafanyika ktk maisha ya mwanadamu namaanisha MTANZANIA). SASA KIMBEMBE KIPO HAPA! Tanzania kunavyuo ambavyo viwango vya ufaulu vinatofautiana, kunaambavyo ufaulu wao wa alama 'C' unaanzia 40%, lakinini kuna vyuo vingine alama 'C' inanzia 50%, "NAOMBA MNIELEWE HAPA" Hawa ambao ufaulu wao wa alama C unaanza na 50% baada ya kuhitimu shahada zao yasemekana hivi(sina uhakika nalo hili) kwa wale wanohitaji huenda TCU Kubadilishiwa alama zao ( to convert) ILI ZIENDANE NA WALE AMBAO ALAMA C 40% na hii ni kutokana na changamoto wanazokumbana nazo katika SOKO LA AJIRA. Suala hili la kubadilishiwa vyeti mwaka huu limefanya TCU wavitangazie vyuo vyote Tanzania ufaulu wa wa alama C ulingane kwa vyuo vyote TANZANIA. sasa baada ya tangazo hil kunavyuo vinasema vitabadilisha pale semista ilipo wakuta wahusika wa vyuo namaanisha walio ktk system na si kuanzia semista ya kwanza inamana CHETI kitakuwa na " two discription" ndani ya chet kimoja na hii pia ni MAJRIBIO. MIMI CJAJUA CHETI CHA AINA HII KIMATAIFA KIPO? SWALI LANGU Je! hawa ambao wako kwenye system wamefanya mitihani ya alama C ya 50% na sasa wanafanya mitihani ya alama C ya 40% wahitimu hawa katika soko la ajira halitawaasumbua? lakini pia hawa wanauwanja mpana wa aijira kimataifa watakapo kwenda nje ya Tanzania na cheti hichi wataweza kuajiriwa? kulingana na GPA kitka chet hiki "with two discription" ndani ya cheti kimoja hakutakuwa na mkanganyiko wa ubora wa vyeti vyao? naombeni msaada wenu wa mawazo wadau PLIZ
 
Back
Top Bottom