Elimu ya ujamaa na kujitegemea ni Kwamba haiwezi kurudishwa ili kukiokoa kizazi cha Sasa?

Elimu ya ujamaa na kujitegemea ni Kwamba haiwezi kurudishwa ili kukiokoa kizazi cha Sasa?

Mageuzi92

Member
Joined
Jan 14, 2023
Posts
6
Reaction score
3
Nilikuwa sijawa mwanafunzi kipindi Cha Nyerere na nilikuwa Bado sijazaliwa . Tukijaribu kuangalia product za elimu ya Nyerere ambao wengi wao ni wazazi wetu utagundua Kuna utofauti mkubwa kiutendaji (nikimaanisha product Zina skills nyingi za kujitegemea kuliko tulivyo Sasa hivi).

Vya kale dhahabu sio mbaya kama tukivurudia.
 
Nyerere au mkoloni?

Ebu kaa sawa sawa endelea kumuuliza mzee wako ni ana umri gani?
 
Unadhani hata wazee wa zaman kwenye game la sasa wangetoboa? Kumbuka na dunia imebadilika
 
Tatizo sio kukosa elimu ya kujitegemea na ujamaa, tatizo ni ubora wa elimu umeshuka.

Miaka ya zamani fursa za elimu zilikuwa chache lakini elimu ilikuwa bora, tumejaribu kupanua fursa lakini tumeshindwa kuhakikisha ubora haushuki.

Zamani hospitali inaweza kuwa na madaktari watano, wote ni wazuri kweli kweli tena wanafanya kazi bila vifaa vya kisasa, siki hizi madaktari 20 lakini 15 tia maji tia maji.

Hata ukienda vyouni utaona tofauti ya wafadhili wale wazee wa zamani na hawa vijana wapya. Kwa hawa vijani ni mchanganyiko wa wababishaji wengi na wazuri wachache.

Wengi hawajui tu, kupata zero form four halikuwa jambo ka kawaida huko zamani, lakini siku hizi tumeshazoea.
 
Elimu ya kulamba asali ndio Inatakiwa Kwa sasa
 
Tupo kwenye ubepari kwa sasa kwahiyo jipambanie wewe na uwapendao. Hizi ni enzi za unyama. Mwenye nacho huongezewa. Ubapari ni unyama yaani hakuna huruma. Ukitaka elimu nzuri inauzwa.
 
Mkuu, kwa kukumegea kidogo tu ni kwamba, enzi hizo za mwl Nyerere tulikuwa tunasoma (tunasomeshwa) kwa lengo la kulitumikia taifa, taifa kwanza, mimi baadae; sasa hivi mnasoma kwa manufaa ya mtu binafsi. Si unajua tena enzi za Cuba na Urusi!
 
Back
Top Bottom