Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza katika kuhakikisha linafikisha elimu juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika Jamii imetoa elimu kwa wafanyabiashara na wavuvi wa mwalo wa Mswahili Mkuyuni huku likiwaonya wanaofanya vitendo hivyo kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.
Akitoa Elimu hiyo Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto wilaya ya Nyamagana Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Irene Mayunga amesema viashiria ama vitendo vya ukatili ni pamoja na kunyimwa haki za Msingi kama vile elimu kwa watoto na ukatili wa kiuchumi wanaofanyiwa kina mama na kina Baba katika Jamii akiwataka wavuvi hao kupaza sauti na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi Juu ya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa vitendo vya ukatili vimekuwa vikididimiza haki kwa jamii huku akiwaomba wananchi hao kuchukia vitendo vya ukatili ili kuwa na Jamii yenye furaha.
Vilevile amewaomba kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili eneo hilo liendelee kuwa shwari.