SoC02 ELIMU YETU: Bodi ya Mikopo ishirikiane na Vyuo ili wanafunzi wasishindwe kuendelea na masomo

SoC02 ELIMU YETU: Bodi ya Mikopo ishirikiane na Vyuo ili wanafunzi wasishindwe kuendelea na masomo

Stories of Change - 2022 Competition

Nyontoka

Member
Joined
Aug 17, 2022
Posts
7
Reaction score
0
Elimu ni tendo la kupata maarifa, ujuzi na maadili anayorithishwa mtu au watu kutoka katika mazingira yanayo mzunguka, kutoka kizazi kimoja hadi kingine .Enzi za mkoloni nchini elimu dhumuni lake hasa kubwa ilikuwa ni kupandikiza mila na desturi za kimagharibi na kudidimiza mila na desturi za mwafrika au mtanzania kwa wakati ule.Elimu nchini Tanzania baada ya mkoloni imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo athari ya elimu ya mkoloni ambayo ilikuwa ya kinadharia zaidi na si vitendo. Elimu nchini imekuwa ni chombo pekee kinachotegemewa katika kuandaa na kupata wataalamu katika nyanja mbalimbali za kijamii mfano katika siasa,uchumi,afya,miundombinu nk, . Hivyo ni muhimu kufanyika maboresho katika mfumo wa elimu ambayo baadhi ni haya ambayo imekuwa ni tatizo kwa elimu nchini Tanzania.

Matumizi ya lugha ya kiswahili Kama lugha ya kufundishia kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu, hii ni moja ya mapendekezo ambayo hata bungeni mara kadhaa wamekuwa wakilijadili ,wadau wa elimu wasiogope kufumua mfumo wa elimu uliopo kwa sasa hasa mtaala na kufanya kiswahili kitumike kwani hata "mafanikio ya Kobe ni pale anapotoa kichwa chale nje kwenye gamba lake',"Jackson Makweta katika mapendekezo yake alizungumza kuhusu hili mwaka 1982" nchi nyingi za magharibi wamekuwa wakitumia lugha zao katika kufundishia Jambo ambalo wameendelea zaidi kwani uelewa wa wanafunzi inakuwa ni rahisi kuliko kutumia lugha ambayo ni ngeni kwa hapa nchini (kingereza) matumizi ya lugha ya kingereza shuleni yanashusha elimu ya Tanzania.

Maboresho katika elimu ya juu na bodi ya mikopo, hizi ni taasisi ambazo zimekuwa zikijihusisha na kuandaa wataalamu wa baadae ambao wao wanakwenda kusaidia nchi, dhumuni la bodi ya mikopo ni kuhakikisha wanafunzi ambao hawana uwezo wa kulipa ada wasaidiwe ili kuendesha masomo Yao wakiwa chuoni ,lakini hapa Kuna changamoto kubwa kwani wanafunzi wengi wenye sifa za kupata mkopo hukosa na hatimaye kushindwa kuendelea na masomo .Hivyo iundwe tume ya watu kutoka bodi ya mikopo ambao watatembea Kila chuo kukutana na wanafunzi ambao wapo kwenye hati hati ya kushindwa kuendelea na masomo na wameomba mkopo hawajapata ili wakusanye taarifa zao na kuwapatia msaada wa haraka kwani inaumiza kuona mwanafunzi ametumia muda wake mwingi miaka 16,17 darasani kisha kuishia njiani tena akiwa chuo kikuu.

mfano;

inbound8577888679272461770.jpg

Kielelezo hapo juu ni Mimi mwenyewe na Wanafunzi wenzangu tukiwa chuoni mwaka 2017 Leo kupitia jamii forums nimeona nilisemee hili kuokoa wengine huku serikali ikiwa haifanyi lolote kujua hawa wanafunzi wameishia wapi na hatma Yao ni ipi .Hivyo bodi ya mikopo kwa kushirikiana na vyuo vikuu wahakikishe kusaidia wale wanaoshindwa kulipa ada wanapata mwongozo sahihi wa kumfanya mwanafunzi kuendelea na masomo mpka anamaliza.

Teknolojia (tehama katika elimu), kutoka na na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika jamii ya Sasa inapaswa serikali kufanya mabadiliko katika miundombinu ya madarasa na vifaa vya kufundishia katika mfumo mzima wa elimu ,mwalimu wa kisasa anatakiwa aandaliwe kwenda kutumia teknolojia katika kufundishia ,aweze kutumia vifaa Kama kompyuta,projekta na jinsi ambavyo mtandao unaweza kusaidia katika kuinua elimu yetu nchini Tanzania, mtaala ubadilishwe uweze kuendana na mabadiliko ya jamii na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Changamoto za ajira na kustaafu, katika Sheria za ajira kijana anapaswa kuajiriwa akiwa na miaka 25 mpaka 33 kwa makampuni mengi lakini mfumo wa elimu nchini Tanzania umekuwa ukipoteza muda mwingi sana kumkalisha mwanafunzi darasani ,mfano mwanafunzi anahitimu chuo akiwa na mika 26 huyu ataajiriwa lini kwa soko la ajira la Sasa zaidi atajikuta yupo nje ya muda ,hivyo elimu inayotolewa ilenge zaidi kuwaandaa wanafunzi kujiajili na si kuajiriwa Kama ambavyo wameanza hivi Sasa baada ya ongezeko la wanafunzi na wahitimu wengi kutokea, kutokana na matokeo ya BIG RESULTS NOW(BRN)ya mwaka 2013. Laikini pia umri wa kustaafu upunguzwe kwani unasababisha mlundikano wa wasioajiriwa kuwa, mkubwa ikienda sambamba na kupunguza miaka ya kukaa darasani ili kutoa fulsa kwa vijana wengine kuajiriwa.

Kugawa wanafunzi katika makundi mawili yaani Sanaa na sayansi, mfumo wa elimu kwa sasa umekuwa unachanganya wanafunzi anayesoma Sanaa huyohuyo asome na sayansi kwa wakati mmoja ,uwepo utaratibu kubaini mwanafunzi ambaye anapenda sayansi basi asome masomo hayo tuu na fani yake anayoitaka Kama ni daktari basi asome masomo yanayotakiwa kumfanya au kumuandaa kuwa daktari mzuri badae ambaye amekuwa akisoma tangu akiwa shule ya msingi Jambo ambalo litapelekea ufanisi mkubwa katika taaluma zetu nchini na si kuchanganya mambo alisoma Sanaa badae anakuwa muuguzi na aliekuwa anasoma sayansi amekuwa mwalimu wa kiswahili, Jambo hili linarudisha nyuma elimu yetu.

Ili kuweza kuendana na soko la ajila kwa sasa nchini ni lazima mfumo wote wa elimu ufunuliwe upya utazamwe upya ,kwani uliopo kwa sasa unalenga kumfanya mwanafunzi kuwa tegemezi na si kujitegemea katika ajila ,pia bado mfumo una dhana ya kinadharia tu na si vitendo na mtazamo wake bado umekaa ukoloni zaidi hadi Sasa .
 
Upvote 0
Jee? Mfumo wa Sasa wa elimu unamsaidia kijana /mhitimu wa ngazi Fulani ya masomo nchini ?
 
Back
Top Bottom