Wadau!
Najiuliza hapa pamoja na utajiri tulionao Tanzania kuanzia MADINI, GESI, MALIASILI (Mbuga za Wanyama, Mlima Kilimanjaro na vitu vingine vya kuvutia duniani, mf. Zanzibar) kama kweli Elimu yetu inawaanda wazawa kuja kuendesha kwa ufanishi rasilimali hizi au ndo ndo Wawekezaji wataendelea kuwaajiri wa Kenya, Afrika Kusini, Wachina, Wahindi na watu toka ulaya & Marekani. Kwa mfano tuna watalaamu wa kutosha wa GESI ASILIA? kwa mfano WAHANDISI (Petroleum/Gas Engineers), je Wanasheria wetu wamebobea kwenye mikataba hiyo au ndo wanasain tu bora liende? Sheria zetu za Kodi zinasemaje kuhusu hawa wawekezaji kulipa kodi stahili?