Elimu yetu inakidhi matakwa ya karne hii?

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
“Ukweli ni kuwa ni asilimia 1.5 tu ya Watanzania ndio waliobahatika kuunda tabaka la wasomi.”
Wasomi wengi wa Tanzania ni matunda ya vyuo vya Magharibi, ndiyo maana hata wazazi wengi wenye uwezo huwasomesha watoto wao nje ya nchi.
Ukweli ni kuwa ni asilimia 1.5 tu ya Watanzania ndio waliobahatika kuunda tabaka la wasomi.
Hiki ni kiwango kidogo sana, kwa taifa linalolenga kujijengea uchumi wa kati katika karne hii ya teknolojia na ushindani mkubwa unaoletwa na utandawazi.
Katika nchi zilizoendelea, mathalani Finland, msomi aliye tayari kwa maana ya kuandaliwa vizuri na mfumo wa elimu uliotukuka, kujiingiza kwenye dunia ya ajira ni yule mwenye elimu ya juu ya kiwango cha shahada ya pili (yaani shahada ya uzamili). Nchi ya Finland hutoa elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi ngazi ya elimu ya juu.
Finland ni nchi ambayo haitegemei teknolojia ya mataifa mengine katika mambo yao ya maendeleo, wanajitengenezea teknolojia yao wenyewe inayowawezesha kumudu changamoto za mahitaji waliyonayo kama taifa.
Siri kubwa ya mafanikio yao ni ubora wa mfumo wa elimu walionao, ni moja ya nchi zenye elimu bora duniani, hasa ile ya msingi. Wana vyuo vikuu na vyuo vya ufundi stadi vya kutosha kutoa wataalamu waliobobea kwenye kila sekta.
Wakati Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali nyingi kama vile madini, gesi asilia, mafuta na vivutio vya utalii, bado tunategemea wataalamu na watafiti kutoka nje kuja kutushauri namna ya kumudu sekta hizi muhimu. Mfumo wetu wa elimu haujaweza kutoa wataalamu wa kutosha wa kuzifanya sekta hizi kuwa endelevu na za manufaa kwa jamii.
Tatizo kubwa tulilonalo ni kuwa mfumo wa elimu tulionao ni wa Ukasuku. Tunajifunza kwa kukariri, siyo kwa kumwezesha mwanafunzi kufikiri. Upungufu uliopo kwenye sekta ya elimu ni wimbo unaoimbwa kila kukicha na mamlaka zinazohusika zinausikia.
Ni kweli kwamba jitihada za kuboresha hali ya elimu zipo, hasa kutoka kwa wananchi kwa njia ya kujitolea, na wadau wengine wa elimu hasa mashirika yasiyo ya kiserikali, jitihada hizi hazitoshi na siyo endelevu.
Kwa hivi sasa Serikali iko kwenye mchakato wa kuandaa sera mpya ya elimu yenye lengo la kutengeneza jamii ya kisomi ili kujenga taifa lenye uchumi wa kati unaoweza kumudu ushindani wa kimataifa. Ili lengo hilo litimie, mfumo wa elimu unatakiwa uwe na uwezo, kiutendaji na kiutekelezaji, wa kutengeneza wasomi wenye uwezo mkubwa wa kifikra na ubunifu.
Tukiwa na wasomi wengi wa aina hii tutapunguza utegemezi wa kuagiza teknolojia na wataalamu kutoka nje kwa ajili ya mahitaji yetu muhimu. Tutabuni teknolojia zetu wenyewe kulingana na ukubwa na aina ya mahitaji yetu wenyewe na mazingira yetu. Wakati sisi bado tunasuasua na mfumo mbovu wa elimu tulionao, wenzetu tayari wana wasomi waliobobea katika nyanja zote na hivi sasa wanang’ang’ana kuwaanda wahitimu wao kuwa tayari kutumika katika mazingira yoyote duniani.
Dhana hii inalenga zaidi katika kuwaweka tayari wahitimu kuweza kumudu mazingira yoyote ya kikazi yanayoletwa na changamoto za utofauti wa kitamaduni. Utandawazi hauji tu na ushindani wa kibiashara bali pia unatengeneza changamoto za kimawasiliano ambazo zinahitaji uzoefu wa muingiliano wa kimawasiliano baina ya watu wa matabaka na tamaduni mbalimbali.
Hivyo basi, mbali na kuwa na mfumo bora wa elimu, ni lazima kuzingatia namna ya kumuandaa muhitimu kuweza kutumia maarifa na ujuzi alioupata kikamilifu katika jamii yenye utamaduni ulio tofauti na mazingira aliyoyazoea.
Chanzo: MCL
 
Tumekosa viongozi makini wanaotambua kwamba elimu ndio msingi wa maisha katka dunia hii ya .com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…