Elimu yetu inatusaidiaje kung'amua fursa na kuzitumia?

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
2,968
Reaction score
8,139
Na Thadei Ole Mushi.

Huwa nacheka sana ninapoona mawaziri wetu wakikimbizana na Ruge mikoani kuzindua kitu kinachoitwa Fursa. Najiuliza pale Mlimani wanafundisha nini? Najiuliza pale SUA wanafundisha nn? Najiuliza shule zetu za A Level wanafundisha nn? Huku ngazi za chini kunafundishwa nini?

Ni dhahiri sasa kinachofundishwa na ngazi tofauti tofauti za elimu Nchini content zake hazina maana kwa wahitimu na zimeshindwa kuwafanya wajiajiri. Je tunakumbuka falsafa yetu ya elimu inasemaje?

Trend ipo hivi wanaomaliza Darasa la saba asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda sekondari, wanaomaliza form 4 asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda form six wanaomaliza form six asilimia 100 wanawaza kujiunga na vyuo vikuu.

Wakimaliza vyuo vikuu wote asilimia 100 wanawaza kwenda kuajiriwa na serikali au makampuni binafsi.

Hii ndio trend ya elimu yetu tuliyonayo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Hatuna clear Philosophy inayotuongoza katika elimu yetu. Mwalimu Nyerere alituachia ya Education for Self reliance.

Katika hili Mwalimu alilenga mtu atakayehitimu hata darasa la Saba aweze kujitegemea kwa kutumia fursa zinazomzunguka.

Tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni Content nyingi tunazofundisha au kufundishwa mashuleni kushindwa kutafsiri fursa tulizonazo.

Shule zetu zilizokuwa zinafundisha fani mbalimbali za Ushonaji, Upishi, uashi nk tumeendelea kuziua na hata wanafunzi hawazitaki tena hizo fani.

Ibn Khladun Mwanafalsafa wa Tunisia aliwahi kusema kuwa elimu isiwe ni ya kukaririsha watu mambo ya zamani kwa Lengo la kuwapatia vyeti.

Kwake yeye content zilizokuwa zikifundishwa zilikuwa nyingi ni za kukaririshwa na aliyeweza kukariri kwa ufasaha ndiye aliyetunukiwa cheti

Hiki ndicho tunachokiona leo katika jamii yetu, atakayeweza kukariri content za physics, Kemia, history na kadhalika huyu ndiye tuanyemgrade kuwa ana akili.

Tunampatia cheti na kumwambia songa mbele hawa ambao hawana uwezo wa kukariri, Content zetu hazijaandaliwa kuwapima uwezo wao mwingine walionao tunawagrade kuwa mmefeli na wanafeli kabisa hadi maisha.

John Dewey huyu ni mwanafalsafa wa kiamerika yeye anatuambia tufundishe kwa kutumia Experience inayomzunguka mwanafunzi.

Hiki mdicho kinachofanyika kwa wenzetu wazungu, wanatemgeneza mitaala yao kulingana na kinachowazunguka ili mwanafunzi aweze kuibua fursa na vipaji alivyonavyo.

Sisi tumengangania kufundisha na kakaririshana colonial Rule toka 1961 hadi sasa na akili zetu zimeacha kutafsiri ni aina gani ya udongo tulionao Tanzania, tumeacha kujifunza tunawezaja kuhamisha maji pale victoria yaje Shinyanga kwenye ukame, hatuwezi kutafsiri chochote.....

Je tutaendelea kuona Boda boda ndiyo fursa pekee?

Je jukumu la kufundishwa content zenye tija ni la nani? Au ni mpaka tumwachie Ruge aje awaokote huko mtaani na kuja kuwafundisha Fursa?

Ukiona semina za kufundishana Fursa kama hizi zikishamiri sana katika nchi fahamu kuwa Nchi haina falsafa ya Elimu na hatujui shule zina Jukumu gani.

Mikopo yote ya kujisomesha tumewapa wale walioweza kukariri vizuri ngazi za chini, wale waliokuwa na vipaji na Talent nyingine tumewaambia waende nyumbani na hawa ndio haswa tuliopaswa kutambua tallent zao na kuzipatia mikopo ya kuziendeleza.

Ukiangalia Site zetu zetu kubwa kubwa makampuni yanayosimamia miradi utakuta ni wachina wanazisimamia, Juzi tulienda kuomba watu toka Uganda kuja kutafiti kama tuna mafuta nchini.

Dunia kwa sasa inawekeza katika Technolojia yaani watu wanawaza kuuza Technolojia zaidi kuliko Korosho na wanatengeneza fedha.

Technolojia hizi hatuwezi kuzivumbua kama tutafundisha Kinjekitile Ngwale kuanzia msingi hadi chuo Kikuu. Kuna haja ya kutengeneza Model mpya ya elimu yetu. Kwamba kama ni historia basi tufundishe labda darasa la ngapi tu miaka mingine inayobaki mtoto afundishwe mambo mengine yatakayomsaidia baadaye.

Elimu yetu ndio chombo pekee cha kutufikisha tunakokutamani vinginevyo tutakuwa tukihangaika kila mahali kutafuta wawekezaji.

Hizi Reli tunazojenga na Barabara zinakuja kuwarahisihia wawekezaji wa nje kupeleka malighafi zao pale bandarini bado. Sisi tutabaki kisafirishia huko gunia mia za Korosho au Karanga. Vinginevyo tutabaki tunasubiri abiria huku njiani kuwauzia pipi, saa na headphones.

Naamini sisi tunaozunguka na viti maofisini na kujidai wenye akili tulibarikiwa tu uwezo wa Kukariri, kuna ambao tuliwaacha mtaani walikuwa na uwezo wa kuyatafsiri mazingira kuliko sisi. Bahati yao mbaya elimu yetu haiwatambui.

Swala la msingi la Kujiuliza tutaanza Kubadilika Lini?
 
Tutabadilika tu endapo alieanzisha mfumo huu akitubadilishia mfumo yan update
 
vijana wa leo ni wavivu sana kutumia bongo zao kufikiria, sawa system ni mbovu lkn tumepewa ubongo wa kufikiri kila mtu kivyake na kwa upande wake kulingana na mazingira yake,

hakuna kinachoshindikana basi tu hiki kizazi cha sasa hivi ni kufatilia umbea na mambo yasiyo na msingi mitandaoni.
 
Kuna kauli imesemwa sana kwamba Elimu yetu haituandai kwa ajili ya kujiajiri ila kwa ajili ya kuajiriwa

Ingekuwa kwenye mitaala yetu kuna somo la Financial education na contents za somo hilo zionyeshe jinsi ya kuona fursa na kuzitumia sio tena kukaririshana na iwe kwa ngazi zote za elimu kama ilivyo somo la civics kwa Olevel, General studies kwa advance na DS kwa ngazi ya chuo, labda lingesaidia watu kujiandaa na kuchangamkia fursa za kiuchumi. Ila ukifikiria tena kama sio suluhisho kwa sababu wapo wanachuo wanaosoma finance lakini wanasubiri ajira za mabenki.
 
Hii imekuwa ni changamoto kubwa sana kwetu vijana
 
sawa, lkn hiyo haimaanishi hao graduate kushindwa kutumia uwezo wao wa akili za kuzaliwa kuendana na mazingira yanayo mzunguka..

hili swala elimu halipingiki ni kweli kabisa lkn je mbona wapo wengi wamesoma elimu hizo hizo lkn wameweza kuangalia upande mwingine wa shilingi na kuweza kufanikiwaa!!

mm naamini bado watu hawajishughulishi ipasavyo...
 
Yeah tatizo watu wengi wanafikiria kuajiriwa na sio kuangalia upande wa pili
 
ndio tatizo hilo, we unafikiri ni kwanini wabunifu huko TZ ni wachache hakuna wagunduzi na wavumbuzi wa vitu tofauti na mataifa mengine!!

ni hayo mambo ya kutaka kuajiliwa, badala ya kutumia elimu yake kufanya mabadiliko ya kutatua au kuongeza kitu kwenye jamii yake.
 
Na Thadei Ole Mushi.

Huwa nacheka sana ninapoona mawaziri wetu wakikimbizana na Ruge mikoani kuzindua kitu kinachoitwa Fursa. Najiuliza pale Mlimani wanafundisha nini? Najiuliza pale SUA wanafundisha nn? Najiuliza shule zetu za A Level wanafundisha nn? Huku ngazi za chini kunafundishwa nini?

Ni dhahiri sasa kinachofundishwa na ngazi tofauti tofauti za elimu Nchini content zake hazina maana kwa wahitimu na zimeshindwa kuwafanya wajiajiri. Je tunakumbuka falsafa yetu ya elimu inasemaje?

Trend ipo hivi wanaomaliza Darasa la saba asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda sekondari, wanaomaliza form 4 asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda form six wanaomaliza form six asilimia 100 wanawaza kujiunga na vyuo vikuu.

Wakimaliza vyuo vikuu wote asilimia 100 wanawaza kwenda kuajiriwa na serikali au makampuni binafsi.

Hii ndio trend ya elimu yetu tuliyonayo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Hatuna clear Philosophy inayotuongoza katika elimu yetu. Mwalimu Nyerere alituachia ya Education for Self reliance.

Katika hili Mwalimu alilenga mtu atakayehitimu hata darasa la Saba aweze kujitegemea kwa kutumia fursa zinazomzunguka.

Tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni Content nyingi tunazofundisha au kufundishwa mashuleni kushindwa kutafsiri fursa tulizonazo.

Shule zetu zilizokuwa zinafundisha fani mbalimbali za Ushonaji, Upishi, uashi nk tumeendelea kuziua na hata wanafunzi hawazitaki tena hizo fani.

Ibn Khladun Mwanafalsafa wa Tunisia aliwahi kusema kuwa elimu isiwe ni ya kukaririsha watu mambo ya zamani kwa Lengo la kuwapatia vyeti.

Kwake yeye content zilizokuwa zikifundishwa zilikuwa nyingi ni za kukaririshwa na aliyeweza kukariri kwa ufasaha ndiye aliyetunukiwa cheti

Hiki ndicho tunachokiona leo katika jamii yetu, atakayeweza kukariri content za physics, Kemia, history na kadhalika huyu ndiye tuanyemgrade kuwa ana akili.

Tunampatia cheti na kumwambia songa mbele hawa ambao hawana uwezo wa kukariri, Content zetu hazijaandaliwa kuwapima uwezo wao mwingine walionao tunawagrade kuwa mmefeli na wanafeli kabisa hadi maisha.

John Dewey huyu ni mwanafalsafa wa kiamerika yeye anatuambia tufundishe kwa kutumia Experience inayomzunguka mwanafunzi.

Hiki mdicho kinachofanyika kwa wenzetu wazungu, wanatemgeneza mitaala yao kulingana na kinachowazunguka ili mwanafunzi aweze kuibua fursa na vipaji alivyonavyo.

Sisi tumengangania kufundisha na kakaririshana colonial Rule toka 1961 hadi sasa na akili zetu zimeacha kutafsiri ni aina gani ya udongo tulionao Tanzania, tumeacha kujifunza tunawezaja kuhamisha maji pale victoria yaje Shinyanga kwenye ukame, hatuwezi kutafsiri chochote.....

Je tutaendelea kuona Boda boda ndiyo fursa pekee?

Je jukumu la kufundishwa content zenye tija ni la nani? Au ni mpaka tumwachie Ruge aje awaokote huko mtaani na kuja kuwafundisha Fursa?

Ukiona semina za kufundishana Fursa kama hizi zikishamiri sana katika nchi fahamu kuwa Nchi haina falsafa ya Elimu na hatujui shule zina Jukumu gani.

Mikopo yote ya kujisomesha tumewapa wale walioweza kukariri vizuri ngazi za chini, wale waliokuwa na vipaji na Talent nyingine tumewaambia waende nyumbani na hawa ndio haswa tuliopaswa kutambua tallent zao na kuzipatia mikopo ya kuziendeleza.

Ukiangalia Site zetu zetu kubwa kubwa makampuni yanayosimamia miradi utakuta ni wachina wanazisimamia, Juzi tulienda kuomba watu toka Uganda kuja kutafiti kama tuna mafuta nchini.

Dunia kwa sasa inawekeza katika Technolojia yaani watu wanawaza kuuza Technolojia zaidi kuliko Korosho na wanatengeneza fedha.

Technolojia hizi hatuwezi kuzivumbua kama tutafundisha Kinjekitile Ngwale kuanzia msingi hadi chuo Kikuu. Kuna haja ya kutengeneza Model mpya ya elimu yetu. Kwamba kama ni historia basi tufundishe labda darasa la ngapi tu miaka mingine inayobaki mtoto afundishwe mambo mengine yatakayomsaidia baadaye.

Elimu yetu ndio chombo pekee cha kutufikisha tunakokutamani vinginevyo tutakuwa tukihangaika kila mahali kutafuta wawekezaji.

Hizi Reli tunazojenga na Barabara zinakuja kuwarahisihia wawekezaji wa nje kupeleka malighafi zao pale bandarini bado. Sisi tutabaki kisafirishia huko gunia mia za Korosho au Karanga. Vinginevyo tutabaki tunasubiri abiria huku njiani kuwauzia pipi, saa na headphones.

Naamini sisi tunaozunguka na viti maofisini na kujidai wenye akili tulibarikiwa tu uwezo wa Kukariri, kuna ambao tuliwaacha mtaani walikuwa na uwezo wa kuyatafsiri mazingira kuliko sisi. Bahati yao mbaya elimu yetu haiwatambui.

Swala la msingi la Kujiuliza tutaanza Kubadilika Lini?
 
ndio tatizo hilo, we unafikiri ni kwanini wabunifu huko TZ ni wachache hakuna wagunduzi na wavumbuzi wa vitu tofauti na mataifa mengine!!

ni hayo mambo ya kutaka kuajiliwa, badala ya kutumia elimu yake kufanya mabadiliko ya kutatua au kuongeza kitu kwenye jamii yake.
Tz wabunifu ni wachache sana na hata hao wachache pia wanakutana na vikwazo mwisho inakua kama hamna ubunifu, hatujawekeza sana sayansi na teknolojia ndio sababu kubwa. Nakumbuka miaka ya nyuma niliangalia kipindi flani kuna kijana alitengeneza taa inayowaka kwa kupiga simu, yani kama umesafiri uko Mwanza na nyumba yako iko arusha, ikifika jioni unapiga namba flani taa za nje zinawaka bila hata kuomba msaada wa jirani nadhani wengi washawahi kuona hii kitu. Kijana yule sijui aliishia wapi ghafla mwaka jana idea ile nimeona imetoka china na bidhaa zao wanauza na kufunga taa hizo kwa bei ghali sana. Kijana yule angepata msaada wa wataalamu wa mambo ya umeme na mitandao angefika mbali.

Angalia leo mtu akamatwe kaunda silaha atawekwa ndani ila kama wangetumia ubunifu wake wakamuwezesha na vifaa na wasomi wampe principles of operation labda tungekua na sisi tunauza silaha mataifa ya jirani hapa na kuongeza pato la taifa.
 
sawa, lkn hiyo haimaanishi hao graduate kushindwa kutumia uwezo wao wa akili za kuzaliwa kuendana na mazingira yanayo mzunguka..

hili swala elimu halipingiki ni kweli kabisa lkn je mbona wapo wengi wamesoma elimu hizo hizo lkn wameweza kuangalia upande mwingine wa shilingi na kuweza kufanikiwaa!!

mm naamini bado watu hawajishughulishi ipasavyo...
Hapa tatizo ni mindset za vijana wetu tangu wakiwa vyuoni, akili zishajiseti kuwa wajifunze kuandika CV vizuri ili wakimaliza waweze kucompete kwenye soko la ajira. Sio wazo baya ila pia ni vyema kuwekeza nje ya ajira ili kujiongezea kipato. Kwenye kitabu cha Robert Kiyosaki-Rich dad poor dad nadhani chapter 5 sina uhakika vizuri na chapter, ameongelea hichi kitu akakipa title ya 'mind your own business'
 
Tz wabunifu ni wachache sana na hata hao wachache pia wanakutana na vikwazo mwisho inakua kama hamna ubunifu, hatujawekeza sana sayansi na teknolojia ndio sababu kubwa. Nakumbuka miaka ya nyuma niliangalia kipindi flani kuna kijana alitengeneza taa inayowaka kwa kupiga simu, yani kama umesafiri uko Mwanza na nyumba yako iko arusha, ikifika jioni unapiga namba flani taa za nje zinawaka bila hata kuomba msaada wa jirani nadhani wengi washawahi kuona hii kitu. Kijana yule sijui aliishia wapi ghafla mwaka jana idea ile nimeona imetoka china na bidhaa zao wanauza na kufunga taa hizo kwa bei ghali sana. Kijana yule angepata msaada wa wataalamu wa mambo ya umeme na mitandao angefika mbali.

Angalia leo mtu akamatwe kaunda silaha atawekwa ndani ila kama wangetumia ubunifu wake wakamuwezesha na vifaa na wasomi wampe principles of operation labda tungekua na sisi tunauza silaha mataifa ya jirani hapa na kuongeza pato la taifa.
serikali mbovu
 
Hapa tatizo ni mindset za vijana wetu tangu wakiwa vyuoni, akili zishajiseti kuwa wajifunze kuandika CV vizuri ili wakimaliza waweze kucompete kwenye soko la ajira. Sio wazo baya ila pia ni vyema kuwekeza nje ya ajira ili kujiongezea kipato. Kwenye kitabu cha Robert Kiyosaki-Rich dad poor dad nadhani chapter 5 sina uhakika vizuri na chapter, ameongelea hichi kitu akakipa title ya 'mind your own business'
3683e11c9f098aa57493375ceb0f346d.jpg
 
Back
Top Bottom