Heavy Metal
JF-Expert Member
- Feb 7, 2017
- 881
- 2,077
Utangulizi
Hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea bila na elimu bora ambayo ndiyo chimbuko la teknolojia mbalimbali zitumikazo viwandani. Teknolojia bora ndiyo msingi wa kuifanya nchi ipige hatua kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla. Kadri unavyokua na viwanda vingi ndivyo unavyoweza kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii. Lakini ili uwe na viwanda vinavyoweza kukabiliana na changamoto hizo lazima watu wako wawe ni wabunifu na watafiti bora zaidi ili kuweza kuzalisha teknolojia mbalimbali zitumikazo viwandani na kuvifanya viwanda viendelee. Kwa upande mwingine, kasi ya ukuaji wa miji duniani umesababisha changamoto nyingi na kuongezeka kwa mahitaji mbalimbali ya kibinadamu kama vile chakula, nishati safi ya kupikia, maji safi na salama, huduma bora za kiafya, huduma za usafiri na miundombinu yake, makazi bora na kadhalika. Mabadiliko na ongezeko la mahitaji ya kibinadamu yanailazimu sekta ya viwanda kubuni teknolojia bora na rahisi ili kutatua changamoto hizi. Kwa nchi zilizoendelea imekua rahisi kwao kwasababu ya kuwa mbele kiteknolojia kiasi ambacho wamekua haraka katika kubuni tatuzi mbalimbali za changamoto zinazoisumbua jamii katika nyanja zote baadhi nikizielezea hapo juu. Hii ni kwasababu ya uwekezaji mkubwa walioufanya kwenye sekta ya elimu kupitia tafiti na bunifu mbalimbali.
Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini duniani ikiwa pia nyuma sana kwenye sekta ya viwanda kwasababu ya mfumo mbovu wa elimu yetu ambayo ina mapungufu mengi ikiwamo kukosekana kwa ubunifu wenye kuweza kuzalisha teknolojia mbalimbali ambazo zingeweza kuwa chachu ya maendeleo ya viwanda.
Yafuatayo ni mapendekezo ya mabadiliko ya kimfumo katika sekta ya elimu ambayo yanaweza kuifanya nchi yetu iwe miongoni mwa mataifa yaliyoendelea kwenye sekta ya viwanda
1. Uboreshaji wa ya elimu ya msingi na sekondari
(i) Kwanza Elimu ya msingii iboreshwe kwa kuboresha miundombinu ya maabara ili kuruhusu elimu ya vitendo zaidi kuandaa kizazi cha utafiti na ubunifu.
(ii) Pili shule zote ziwe na karakana za ndogo ndogo za kiufundi zinazoweza kuruhusu wanafunzi kufanya majaribio ya kisayansi, ubunifu na utafiti
(iii)Tatu shule ziwe zenye uwezo wa kubeba wanafunzi wachache ambao wataendana na miundombinu iliyopo.
2. Uboreshaji wa elimu ya sekondari
Elimu ya kidato cha tano hadi cha sita iondolewe badala yake elimu ya sekondari hadi kidato cha nne iboreshwe zaidi ili kumfanya mwanafunzi awe na uwezo wa kujiunga na vyuo vya ufundi vya kati na vyuo vikuu moja kwa moja. Uboreshaji huu uhusishe kurudisha mfumo wa zamani wa shule za ufundi lakini kwa sasa shule za sekondari zote ziwe na karakana na masomo ya ufundi na elimu itolewe kwa kuzingatia sera ya elimu kwa vitendo
3. Uboreshaji wa maslahi ya kada ya ualimu
(i)Kwanza ualimu kwa ngazi ya msingi na sekondari lazima Mwalimu awe na elimu ya shahada ya kwanza ya chuo kikuu yani bachelor degree.
(ii) Maslahi ya walimu yaboreshwe na yaendane na ugumu, uzito, umuhimu na unyeti wa kazi yao.
(iii) Taaluma ya ualimu wa sayansi itolewe kwa kuzingatia sera ya viwanda
(iv) Walimu waboreshewe mazingira ya kazi na ya kuishi ili kuzalisha kizazi bora chenye moyo wa uzalendo na taifa lao.
4. Uboreshaji wa elimu ya vyuo vya ufundi vya kati
Nguvu kubwa ielekezwe kwenye kuboresha mazingira ya vyuo vya ufundi vya kati maana ndiyo vyenye kuzalisha kada tendaji zaidi kwenye sekta viwanda. Kutoka chapisho la shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia maswala ya elimu, sayansi na utamaduni UNESCO la mwaka 1980 limefafanua vizuri namna mifumo bora ya elimu ilivyosaidia nchi kama India, China na Korea kufanikiwa zaidi kwenye sekta ya viwanda. Hivyo vyuo hivi viwe vingi na viwe kisekta zaidi kama vile kilimo, maji, nishati, madini na kadhalika.
5. Uboreshaji wa elimu ya Chuo Kikuu
(i) Madaraja na vigezo vya kuingia chuo kikuu viongezwe ili tuweze kupata zao bora zaidi. Hakuna haja ya kua na wahitimu wengi wa chuo kikuu wasiokua na kazi wala msaada kwa jamii.
(ii) Mazingira ya kujifunzia pia yaboreshwe zaidi yawe ni yenye kuzingatia utafiti, ubunifu na elimu kwa vitendo.
(iii) Kuanzia shahada ya kwanza (Bachelor degree) hadi ya tatu (PhD) vigezo vya kihitimu masomo ya chuo kikuu uzingatie machapisho ya kitaaluma (publications) na bunifu (innovations) alizofanikiwa kufanya mwanafunzi wakati yuko masomoni
6. Tafiti na bunifu za vyuo vikuu
(i) Tafiti zote za vyuo vikuu zizingatie mahitaji halisi ya sekta ya viwanda.
(ii) Tafiti na bunifu zetu zifanyike kisekta kulingana na idara husika
(iii) Chuo na idara husika wakusanye changamoto kutoka kwenye jamii na viwandani ili kuzifanyia utafiti na kuja na suluhisho
(iv) Wanafunzi wasitafute tafiti zao vyuoni bali wafanyie utafiti changamoto za kitaifa kwenye sekta ya viwanda ambazo tayari zimeshakusanywa katika idara zao kulingana fani walizodahiliwa
(v) Wahadhiri wawe na miradi ya tafiti na bunifu ambazo zinaendana na sera ya viwanda lakini pia miradi yao iwe na uwezo wa kudahili wanafunzi ili kupata mwendelezo mzuri wa tafiti na bunifu hizi.
(vi) Vyeo na maslahi ya wahadhiri yaendane na idadi ya miradi wanayopata kupitia wafadhili wa kimataifa kwa kila mwaka lakini pia zao la tafiti na bunifu wanazofanya. Hii itasaidia kukua kwa teknolojia na kuongeza thamani ya taaluma wanayotoa kwa wanafunzi.
7. Uhusiano na ushirikiano kati ya vyuo vikuu na sekta ya viwanda
Tafiti na bunifu zizingatie mahitaji ya viwanda vyetu. Kila chuo Kikuu lazima kiwe na industrial center ambayo itakua inashughulika na utafiti na ubunifu wa kisekta.
Kwa ufupi:
(i) Serikali iwekeze vya kutosha kwenye tafiti na bunifu zinazofanyika kwenye vyuo vikuu na taasisi za utafiti ili tafiti na bunifu ziwe na tija kwa taifa katika kuendana na sera ya viwanda.
(ii) Serikali boreshe mazingira ya vyuo vikuu kwa kujenga miundombinu ya maabara, karakana na vifaa bora kwa ajili ya kufanyia tafiti na bunifu mbalimbali.
(iii) Viwanda vishirikiane na vyuo vikuu kufanya tafiti na bunifu ili kukuza teknolojia katika sekta ya viwanda nchini
8. Mwelekeo wa sera za nchi kuhusu sekta ya viwanda
Serikali iwekeze kikamilifu kwenye sekta ya elimu kuanzia ngazi ya chini kama nilivyoeleza huko juu. Sera ya viwanda itekelezwe kwa vitendo kwa kupeleka wanafunzi na wataalamu mbalimbali nje ya nchi ili kupata taaluma muhimu za kuboresha sekta ya viwanda na kuja na teknolojia mbalimbali zitakayosaidia kuzalisha viwanda vingi ambavyo pia vitasaidia kuboresha sekta zingine zote pamoja na kupunguza tatizo la ajira na umaskini nchini.
Hitimisho:
Tanzania ya viwanda ndani ya miaka 25 ijayo inawezekana kama tutatekeleza kikamilifu maboresho kwenye mfumo wetu wa elimu.
Naomba kuwasilisha.

Upvote
4