SoC02 Elimu yetu

SoC02 Elimu yetu

Stories of Change - 2022 Competition

Mahja

New Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Jamii yetu inaamini sana kuhusiana na elimu. Mtoto akisoma kwa bidii anakuja kuwa na mafanikio makubwa.

Je, in kweli kwamba watoto wote waliosoma wanafikia malengo yao?
Embu tuingalie elimu yetu nchini.

Kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari mtoto anaenda shule anasoma kwa bidii ili aje afaulu mitihan ya mwisho afike chuo kikuu.

Kwa ufupi elimu imejikita sana kwenye mitihani kulikokipaji alichokuwa nacho mwanafunzi.

Je, vipi sasa huyu aliesoma mpka chuo kikuu lakin bado hana mafanikio yoyote?mpaka Leo bado anahangaika na ajira?

Je, na nivipi uyu aliesoma lakin hakufaulu mitihani yake akaishia kidato cha nne je ndio mwisho wa mafanikio yake?

Kwa hiyo ukiangalia kwa asilimia kubwa mwanafunzi aliesoma mpaka chuo kikuu akakosa kuajiriwa na huyu ambae hakufaulu kidato cha nne wote wanakuwa sehemu moja ndio pale utakuta vijana wengine wanajihusisha kwenye biashara haramu, wengine kwa upande wa wanawake wanaenda uza miili yao ili wapate pesa za kukidhi mahitaji yao, kuenea kwa wezi mitaani,kuenea kwa watoto wa mitaani,bodaboda kuwa wengi.

Hivyo basi elimu kukosa sifa kubwa ya kuwa ufunguo wa maisha.

Je, ni nin kifanyike wote walioenda shule waje kuwa na mafanikio?

1) Shule zote nchini zinatakiwa zifundishe ufundi wa fani tofauti.

Kwa maana hiyo kusiwe tu na shule maalumu kwa ajili ya ufundi kwani watoto wote nchini wanavipaji hivyo wakipewa nafasi naamini wanaweza.

Kwani shule zikiwa zinatoa elimu kwa vitendo kuhusiana na fani mbalimbali kama uchoraji,ushonaji,ujenzi,umeme nk. Kuanzia elimu ya msingi mpaka elimu ya juu, hivyo basi mwanafunzi huyu akirudi mtaani anakuwa haanzi upya katika maisha kwani ametoka na kitu kichwani na anakuwa na uwezo wa kujiajiri yeye mwenyewe.

2) Kuwe na matamasha mbalimbali ambayo yatajumuisha watoto wa shule mbalimbali nchini kuonyesha vipaji vyao hivyo itatoa hamasa kubwa kwa watoto kupenda shule zaidi na kupata fursa mbalimbali.

Kwa maana hiyo wazazi wetu wataona elimu inamanufaa zaidi kwa watoto na watoto wenyewe wataipenda sana elimu.

SHUKRANI SANA

Imeandaliwa na Mas Saidi
 
Upvote 0
Back
Top Bottom