Elimu yetu:

frankg

Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
25
Reaction score
1
:yo:NDUGU watanzani hebu tukae tujiulize wapi tuendako. Wahengana walisema ukitaka kumtawala mtu vizuri usimpe vitu mhimu viwili ambavyo ni elimu na chakula, leo hii tunaona taifa linavyoandaa wajinga wengi, hali hii ilianza pale mh. mmoja alipoingia madarakani na kuondoa baadhi ya masomo kama vile sayansi kilimo shule za msingi na kuondolewa somo la Agriculture sekondari. Lakini katika elimu hiyohiyo tunaona majengo yasiyo kuwa na ubora kujengwa kwa wingi sana bila kuangalia ubora wake.
Wanajamii f kuna mambo ambayo ningependa kuyaongelea;
1. Ualimu ni zaidi ya kufundisha, kuandaa maazimio na maandalio. mwalimu anaweza kufanya hayo yote lakini kama mazingira ya kazi si mazuri hivyo vyote si tija katika elimu

2. Mazingira ya kazi (vituo kuwa na migogoro kutokana na wakuu wa shule wao kujiona kuwa wao si sehemu ya walimu) pia maafisa elimu nao kukaa ofisini bila kuzungukia vituo vya kazi na kujua migogoro iliyopo vituoni

3. Mimi ningependekeza hawa wakuu wa shule wateuliwe/wachaguliwe na walimu walioko katika kituo husika na kupeleka majina kwa afisa elimu wa mkoa na kupitisha majina ili hawa wakuu wa shule wawe wawakilishi sahihi wa walimu ili kutatua matatizo yao, si kama ilivyo sasa wao wanakuwa ni wakandamizaji wa walimu kupitia D.E.O

4. Walimu wa sayansi waboreshewe mazingira ya kufundishia ikiwa ni pamoja na kuongeza vifaa vya maabara hata kama hakuna maabara madarasa yatengwe ili kuwafundisha vijana kwa vitendo. Maana tunakoelekea walimu wa sayansi hawatapatikana serikali isipochukua hatua madhubuti haraka.
 

Kwa kuongezea mabadiliko ya elimu yasiwe yanafanyika bila kushilikisha wadau wa elimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…