SoC02 Elimu

SoC02 Elimu

Stories of Change - 2022 Competition

Zinah krishna

New Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Elimu ni kitu muhimu sana kwetu sisi sote katika nchi yetu na dunia nzima kwa ujumla wake, kupitia elimu tunaweza kua na uwezo wa kufanya vitu vingi vyenye kuleta tija katika jamii zetu maana hata ukiwa na talanta ya kufanya kitu flan itabidi ukapate elimu juu ya hyo talanta yako ili uje ufanye hicho kitu kwa usahihi zaidi na ufanisi wa hali ya juu kabisa, mfano unaweza ukawa na kipaji kikubwa cha kutangaza na hauna elimu ya utangazaji hivyo basi utakua hujui misingi, maadili na sheria katika utangazaji itakubidi sasa ukasomee hata kama ni kwa mda ufupi ili usije ukaenda nje ya maadili ya utangazaji au kuvunja sheria pia na kujikuta matatizoni maana vipo vitu vya kuvizingatia katika utoaji wa taarifa, mbali ya utangazaji pia fani zingine zote zilizobaki inabidi uzifanye kwa kufata maadili ya hicho kitu bila kuvunja miiko ya fani husika.

Elimu kwa watu wote ni jambo ambalo limekuwa likiimbwa mara zote na serikali ya nchi yetu ila tumeonekana kutokutia maanan jambo hilo sababu wazazi wamekua hawatoi ushirikiano mzuri kwa serikali hadi kupelekea jambo hili kutokufanikiwa kwa asilimia kubwa na hata ikitokea wameenda shule kupata elimu basi ni kwasababu tu wameshinikizwa ila wazazi hata watoto wenyewe wamekua hawajui na hawaelewi umuhimu wa elimu matokeo yake inakua ni kazi bure, muda mwingine maisha magumu ya baadhi ya wazazi hupelekea wazazi kutokutilia maanani suala la elimu kwani huwatumia watoto wao kama chanzo cha kujipatia kipato, mfano wazazi wamekua wakiwapatia watoto wao bidhaa mbalimbali kwenda kuuza mtaani ila wengine huenda mbali zaidi na kuwapeleka majumbani kwa watu wenye uwezo kimaisha kwa ajili ya kuwa watumishi wa pale hali ya kua umri wao unakua hauruhusu ndio maana wimbi la watoto wengi wenye umri mdogo mtaani limekua kubwa haijalishi wanafanya biashara au wapo to na hiyo hupelekea watoto kujiunga katika makundi yasiyofaa ambayo yanakuja kuleta shida mtaani na jamii kwa ujumla mfano mkubwa ni (PANYA ROAD) na makundi kama hayo mara nyingi husababishwa na vijana wengi kutokua na elimu, na tunajua usipokua na elimu basi kupata ajira inakua ni ndoto hivyo basi vijana huamua kuunda makundi ambayo yatawafanya kujipatia kipato katika njia isiyofaa.

Elimu kubwa inatakiwa itolewe kwa wazazi na watoto pia juu ya umuhimu wa kupata elimu , japo imekua ikitolewa ila nguvu kubwa inatakiwa iongezeke katika utoaji wa elimu angalau kuwepo na ufuatiliaji wa kila baada ya miezi mitatu ili kuhakikisha watoto wanakwenda shule kama hiyo haitoshi mzazi yoyote atakaeonekana kukaidi jambo hilo hatua kali ichukuliwe dhidi yake, kwa kufanya hivyo kutasaidia kuhakikisha angalau asilimia 95 ya vijana wanakua na elimu angalau ya sekondari.

Msingi mzuri wa baadae wa taifa letu utajengwa na vijana ambao wana Elimu, na pia ili kufikia pale tunapopataka lazima tuwe na mtaji wa maarifa katika vichwa vya waTanzania ambao unatokana na Elimu ambao ndo chachu ya maendeleo katika taifa letu.

Na;ZIDATH JUMA
zidathjuma7@gmail.com
 
Upvote 1
Back
Top Bottom