SoC03 Elimu

SoC03 Elimu

Stories of Change - 2023 Competition

IsaacKedymon

New Member
Joined
Jul 24, 2023
Posts
2
Reaction score
0
Elimu

Ni ipi hatima ya maendeleo chanya kwa Tanzania ya leo hususani katika ulimwengu wa utawandawazi sayansi na teknolojia ? Yote haya ni maswali muhimu ambayo endapo yakijibiwa kwa ufasaha uwenda ikasaidia kutatua kero na changamoto mbalimbali katika jamii yetu.

Tanzania ni taifa ambalo limejizolea sifa na umarufu mkubwa haswa katika ukombozi wa wa nchi za Kiafrika dhidi ya udhalimu na utawala wa wakimabavu kutoka kwa wakoloni,_lakini je,.. kwanini Tanzania imeshindwa kupiga hatua chanya katika sekta mbali mbali husani sekta ya Afya, Miundombinu Elimu na hata kilimo, ukilinganisha na baadhi ya mataifa ambayo taifa hili limeyasaidia kupata uhuru?.

Ukichunguza kwa umakini utakuta tatizo sugu linaloikwamisha Tanzania kupiga hatua stahiki katika nyanja mbali mbali ususani katika Uchumi Maendeleo na Utawala bora ni mfumo mbovu wa elimu uliopo. Elimu Tanzania imekuwa ni suala lisilo zingatiwa wala kupewa kipaumbele.

Mwananchi wakawaida anaposhindwa kutambua haki zake za kimsingi ni kutokana na kutokuwa na elimu yakutosha kujua namna gani anaweza kuiwajibisha serikali yake pale inapokosea au kwenda kinyume na matarajio yake. “Elimu ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi”.

Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa kimaksudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine. Kwahivyo ni dhahili kwamba elimu isipotiliwa mkazo hata jamii yetu itakosa maadili , maarifa na hata ujuzi autokuwepo.

Sasa ili kuinusuru jamii yetu kutoka katika ufinyu wa kifikra ni kuhakikisha mfumo wetu wa elimu unaboreshwa na kupewa kipaumbele kwani pasipo kufanya hivyo Watanzania tutabaki wasindikizaji wa maendeleo, sayansi na teknolojia kwa mataifa jirani.

Mwaka 2015 pale jangwani Mh: Edward Lowassa akiwania uraisi alipohojiwa ni ipi itakuwa sera yake katika kampeni zake za uchaguzi Alijibu na nukuu “Elimu,Elimu,Elimu “ Watanzania tulimcheka na kusema mzee huyu kazeeka na Akili yake imeharibika atoweza kutuvusha_Lakini je, kama mtu aliyekuwa serikalini nakushika nyazifa za juu kabisa kwa miongo zaidi ya mitatu anaposema tatizo sugu la Tanzania ni Elimu, basi ni dhahiri mfumo wetu wa elimu ni mbovu istoshe aukidhi vigezo kutatua changamoto zilizopo hususani katika ulimwengu huu wa utandawazi, sayansi na teknolojia.

Tunazungumzia deplomasia ya uchumi wakati atuboreshi mifumo yetu ya elimu, sasa hapo utawajengea vipi wanadiplomasia wako kuwa na ushindindani katika medali za kimataifa ? Mengi ni maswali ambayo majibu yake yapo waziwazi ingawaje walioshika usukani wamekuwa ni wabinafsi kukubali ukweli kwamba Tanzania ya leo inahitaji mabadiriko haswa katika sekta ya Elimu ili kuvuka hapa tulipo, yatupasa kufanya mabadiriko.

Watanzania wanashabikia masuala yasiokuwa na tija kabisa. Utakuta vijana kwa wazee wanashabikia mechi za simba na yanga wakati mataifa kama China, Japan na India wanawekeza mda wao kufanya tafiti uvumbuzi na uundaji wa mitambo, machine, magari ili kurahisisha shughuri zao viwandani, mashambani na hata kuongeza pato la taifa_lakini sisi hata zinapotokea fursa tunashindwa kuzitumia kwasababu tuko busy kufuatilia udaku mitandaoni nakusikiliza miziki ya singeli.

Tuipe elimu kipaumbele aiwezekani miaka zaidi ya sitini ya uhuru maadui zetu ni wale wale ujinga, umasikini na maradhi wakati wenzetu mataifa mengine wapo katika viwango vingine kimaendeleo tahaluma teknolojia mpaka kimifumo. Mwisho niitimishe kwa kusema “Elimu,Elimu,Elimu”.

Asanteni
 
Upvote 0
Back
Top Bottom